Sunday, 21 November 2010

MAMBO MSETO


 KWAYA  kutoka Maposeni High School-Peramiho (PERASECO) ambao ni sehemu ya umoja wa vijana wanafunzi wakikatoliki Tanzania (Tanzania Youth Catholic Students) wakitumbwiza katika Parokia ya Mjimwema Jimbo la Songea katika ziara yao leo Jumapili asubuhi na mapema Mjini Songea.


 Mary Ndunguru wanafunzi wa Kidato cha Tatu (Fomu 3) katika Shule ya Sekondari Sapientia Mjimwema Songea Mjini alikutwa akikinga maji kutoka kwenye kisima kilichopo karibu ya mabweni ya wasichana ya shule hiyo leo. Asilimia kubwa ya wakazi wa maeneo ya Mjimwema na kwingineko Mjini Songea hutumia maji ya visima kutokana na kutokuwepo huduma ya maji ya bomba kutoka Idara ya Maji-Songea. (Picha. Friday Simbaya)

 BAADHI ya waumini wakifuatilia misa takatifu kwa nje ya Kanisa la Mjimwema baada ya kanisa hilo kufurika watu katika Parokia ya Mjimwema Jimbo la Songea, ambapo misa hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Paroko msaidizi Flowini Tindwa Mjini Songea leo.

RAIA wa kigeni akikata kiu ya maji kutokana na Jua kali lililokuwa likiwaka mchana wa leo, kutoka kwenye kisima kilichopo karibu na mabweni ya wasichana Shule ya Sekondari Sapientia ya Kanisa Katoliki liliopo  karibu na kanisa ya Parokia ya Mjimwema Jimbo la Songea.

Iringa Regional Commissioner Calls On Kilolo Leaders To Strictly Supervise Government Projects

IRINGA – The Iringa Regional Commissioner, Kheri James, has urged leaders of the Kilolo District Council—particularly those in the secondary...