Iringa. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), ameomba wananchi wa kata ya Lyamgungwe, Wilaya ya Iringa,
kumpa tena ridhaa ya kuendelea kulitumikia jimbo hilo katika uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Akizungumza
na wananchi na wanachama wa CCM wakati wa kampeni, mgombea huyo alisema kipindi
cha miaka mitano iliyopita kilikuwa cha kujifunza, huku akieleza kuwa endapo
atapewa nafasi nyingine, ataendeleza miradi ya maendeleo aliyoianzisha.
Alibainisha
kuwa moja ya changamoto zinazowakabili wananchi ni ukosefu wa vyumba vya kuhifadhi
maiti katika vituo vya afya, na kuahidi kushirikiana na Serikali kuhakikisha
kila kituo kinakuwa na huduma hiyo ili kupunguza gharama za kupeleka maiti
katika Hospitali ya Tosamaganga.
Aidha,
alitaja mafanikio aliyoyapata katika kipindi chake cha ubunge ikiwemo
kufanikisha ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mgama, hatua ambayo imesaidia
kurahisisha usafirishaji wa mazao na huduma muhimu.
“Chama
Cha Mapinduzi ndicho chama pekee chenye uwezo wa kudumisha amani na usalama wa
nchi hii. Tuendelee kukiamini na kukipa kura zetu ili maendeleo yawe endelevu,”
alisema.