Thursday, 2 October 2025

Iringa Regional Commissioner Calls On Kilolo Leaders To Strictly Supervise Government Projects


IRINGA – The Iringa Regional Commissioner, Kheri James, has urged leaders of the Kilolo District Council—particularly those in the secondary education, engineering, and procurement departments—to exercise diligence and professionalism in supervising government projects to ensure they bring real benefits to citizens.

Mr James made the remarks yesterday during an inspection tour of development projects in the district, including the construction of two dormitories for A-Level students at Ifingo Secondary School in Kising’a Ward, Kilolo Division through Secondary Education Quality Improvement Project for Tanzania (SEQUIP).

SEQUIP is to increase access to secondary education, provide responsive learning environments for girls, and improve completion of quality secondary education for girls and boys. .

During the visit, the Regional Commissioner expressed dissatisfaction with both the pace and the supervision of the project after finding that, despite the release of funds through SEQUIP, one dormitory remained incomplete.




“I am not satisfied with the supervision of these dormitories. The funds have not been used appropriately and some of the structures are already falling into disrepair. We will not tolerate anyone who misuses government money,” Mr James stressed.

He further noted that Kilolo District has lagged behind in implementing social projects due to poor supervision, lack of professionalism in engineering and procurement, and delays that leave residents without essential services.

“Every project in Kilolo is scrutinised by TAMISEMI and TAKUKURU, yet challenges remain enormous. This is sheer negligence, which is unacceptable, because this district has sufficient economic potential,” he added emphatically.

In the same tour, the Regional Commissioner also inspected other projects, including Nyalumbu Health Centre, Iringa Regional Girls’ School (Lugalo Girls’ High School), Kilolo Secondary School, Lukosi Secondary School, and Ruahambuyuni Health Centre.




CALL TO IRINGA RESIDENTS

Meanwhile, Mr James called on residents of Magulilwa Ward, Mlolo Division, Iringa District, to safeguard the infrastructure of Mlanda Health Centre so that it can continue to provide quality services for years to come.

He stressed that the success of development projects depends not only on government and experts but also on the active participation of the community in protecting and maintaining them.

“This centre belongs to all citizens. It is our responsibility to protect it from any form of damage. We require strong oversight from professionals as well as cooperation from the community,” said the Regional Commissioner.

He also urged council experts to discharge their duties with professionalism and integrity, ensuring that value for money is visible in every project undertaken.

The visit formed part of the Iringa Regional Government’s strategy to closely monitor the implementation of development projects and guarantee that essential services such as education and healthcare reach citizens at the expected standards.

Ends



 

RC IRINGA ATAKA VIONGOZI KILOLO WASIMAMIE KIKAMILIFU MIRADI YA SERIKALI

 







Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amewataka viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, hususan idara ya elimu sekondari, uhandisi na manunuzi, kusimamia kwa umakini na weledi miradi ya serikali ili kuhakikisha inaleta manufaa kwa wananchi.

RC James alitoa kauli hiyo jana baada ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo, ikiwemo ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Ifingo, Kata ya Kising’a, Tarafa ya Kilolo, kupitia mradi kuboresha mazingira elimu sekondari (SEQUIP).

Katika ukaguzi huo, Mkuu wa Mkoa hakuridhishwa na kasi ya utekelezaji pamoja na usimamizi wa mradi huo, baada ya kubaini kuwa licha ya fedha kutolewa, bweni moja bado halijakamilika.




“Sijaridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa mabweni haya. Fedha hazijatumika ipasavyo na baadhi ya majengo yamebaki magofu. Hatutamvumilia mtu yeyote atakayechezea fedha za serikali,” alisisitiza RC James.

Amesema Wilaya ya Kilolo imekuwa ya mwisho katika utekelezaji wa miradi ya kijamii kutokana na upungufu wa usimamizi, ukosefu wa weledi katika uhandisi na manunuzi, hali inayosababisha miradi mingi kuchelewa kukamilika huku wananchi wakikosa huduma stahiki.

“Kila mradi Kilolo unachunguzwa na TAMISEMI, TAKUKURU, lakini bado changamoto ni kubwa. Huu ni uzembe usiokubalika kwa kuwa wilaya hii ina uwezo wa kiuchumi wa kutosha,” aliongeza kwa msisitizo.

Katika ziara hiyo, RC James alikagua pia miradi mingine ikiwemo Kituo cha Afya Nyalumbu, Shule ya Wasichana ya Mkoa wa Iringa (Lugalo Girls High School), Shule ya Sekondari Kilolo, Shule ya Sekondari Lukosi na Kituo cha Afya Ruahambuyuni.

WITO KWA WANANCHI IRINGA

Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliwataka wananchi wa Kata ya Magulilwa, Tarafa ya Mlolo, Wilaya ya Iringa, kulinda na kutunza miundombinu ya Kituo cha Afya Mlanda ili kiweze kutoa huduma bora kwa muda mrefu.





Alisema mafanikio ya miradi ya maendeleo yanategemea sio tu serikali na wataalamu, bali pia ushirikiano wa wananchi katika kuitunza na kuilinda.

“Kituo hiki ni cha wananchi wote. Ni wajibu wetu kukilinda dhidi ya uharibifu wa aina yoyote. Tunahitaji usimamizi madhubuti kutoka kwa wataalamu na ushirikiano kutoka kwa jamii,” alisema RC James.

Aidha, aliwataka wataalamu wa halmashauri zote kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu, sambamba na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwenye kila mradi unaotekelezwa.

Ziara hiyo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Mkoa wa Iringa katika kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha huduma za msingi kama elimu na afya zinawafikia wananchi kwa ubora unaostahili.

Mwisho


Iringa Regional Commissioner Calls On Kilolo Leaders To Strictly Supervise Government Projects

IRINGA – The Iringa Regional Commissioner, Kheri James, has urged leaders of the Kilolo District Council—particularly those in the secondary...