Saturday, 13 September 2025

JASMINE NG’UMBI: NITAIBUWA FURSA ZA MAENDELEO KWA VIJANA NA WANAWAKE



Mbunge Mteule wa Viti Maalum Vijana Taifa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka mkoa wa Iringa, Jasmine Ng’umbi, ameahidi kutumia nafasi yake bungeni kuhamasisha na kusukuma mbele miradi inayowagusa moja kwa moja vijana na wanawake, ili kuongeza fursa za maendeleo kwa makundi hayo.

Akizungumza leo wakati Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, akizindua kampeni za wagombea ubunge na udiwani katika majimbo ya Kalenga na Iringa Mjini, Jasmine alisema anaingia bungeni akiwa na dhamira thabiti ya kuhakikisha vijana na wanawake wanapata nafasi kubwa zaidi kiuchumi na kijamii.

“Nitashirikiana na Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan na wabunge wenzangu kuhakikisha tunatunga na kusimamia sera zenye kutoa matokeo chanya kwa vijana na wanawake, kuanzia upatikanaji wa mitaji midogo, ujuzi wa kisasa, hadi ushiriki kwenye miradi mikubwa ya maendeleo,” alisema.

Jasmine aliwataka wananchi wa Iringa na Watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanampa kura za kishindo Dkt. Samia, wabunge na madiwani wa CCM, akisisitiza kuwa chama hicho kimeonesha kwa vitendo uwezo wake wa kuwaletea maendeleo watu wote bila ubaguzi.



“Rais Samia ameonesha mfano wa uongozi wa vitendo. Sasa ni jukumu letu kuendeleza kasi hiyo kwa kuhakikisha CCM inaendelea kupewa ridhaa ya kuongoza, ili vijana, wanawake na Taifa kwa ujumla waendelee kufaidika,” alisisitiza.

Iringa Regional Commissioner Calls On Kilolo Leaders To Strictly Supervise Government Projects

IRINGA – The Iringa Regional Commissioner, Kheri James, has urged leaders of the Kilolo District Council—particularly those in the secondary...