Thursday, 16 December 2010

UCHAWI NA MAJINI NINI?

 Mwandishi wa kitabu kidogo cha Uchawi na Majini Nini? Padre Geogory Mwageni OSB ana kwa ana na mmliki wa blog hii akipitia baadhi ya vitabu alivyoandika leo katika Duka la Vitabu la Peramiho, Songea mkoani Ruvuma. Kitabu hicho kilichapishwa na Benedictine Publication Ndanda-Peramiho. Pata nakala yako sasa iliujue kwa undani masuala ya uchawi na majini kama kunahusiano au la.

"Nimezaliwa Ubena mnamo mwaka 1922 wakati jamaa zangu wote walipokuwa wapagani. Nilijifunza dini ya kikristo, shuleni tu. Mwaka 1935 niliingia seminari ndogo ya Peramiho, Ungoni. Baadaye nikaishi Kigonsera, tena Peramiho, mwishowe nikaingia utawa Liganga. Tangu kupata upadre mwaka 1954 hadi kuingia utawa nalihudumia katika Umatengo. Tangu 1960 naishi Hanga katika nchi ya Undendeule katika Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma"

Iringa Regional Commissioner Calls On Kilolo Leaders To Strictly Supervise Government Projects

IRINGA – The Iringa Regional Commissioner, Kheri James, has urged leaders of the Kilolo District Council—particularly those in the secondary...