Na Friday Simbaya, Iringa
MRATIBU wa kampeni wa Jimbo la Iringa Mjini, Salvatory Ngelela, amesema wananchi wa Kata ya Kitwiru na maeneo mengine ya jimbo hilo wana kila sababu ya kuichagua CCM katika uchaguzi mkuu Oktoba 29 kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi iliyopita.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kitwiru, Ngelela alisema:
“Kile tulichokiahidi tumetekeleza kwa asilimia kubwa. Ndiyo maana tunaomba ridhaa ya miaka mitano mingine ili tuendelee pale tulipoishia. Wapo wagombea wa vyama vingine waliokimbia uchaguzi kwa kuhofia kura za wananchi,” alisema.
Aliongeza kuwa Rais na Mgombea Urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, amefanya mambo makubwa kwa taifa kwa muda mfupi.
“Utekelezaji wa ilani unaonekana kwa vitendo. Tunawaomba mjitokeze kumpa kura za kishindo ili aendelee kutuletea maendeleo,” alisema.
Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Iringa Mjini, Fadhili Ngajilo, aliahidi kushughulikia haraka miradi inayosubiri utekelezaji.
“Nitafuatilia kwa karibu kuanza kazi kwa Kituo cha Afya Kitwiru, ujenzi wa daraja la Kitwiru linalounganisha Kata ya Isakalilo, na nitapigania ujenzi wa soko jipya la mazao,” alisema Ngajilo huku akiomba wananchi kumpa kura.
Ngajilo pia aliahidi kushirikiana na mamlaka husika kutatua changamoto za maji na kuimarisha mikopo kwa makundi mbalimbali.
“Naomba wananchi wa Iringa Mjini mnipatie ushirikiano na kura zenu. Tukishirikiana, maendeleo ya jimbo letu yataharakishwa,” alisema.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa, Said Rubeya, alikumbusha wananchi kuhusu miradi iliyotekelezwa.
“Shule ya Msingi Uyole, Sekondari ya Kwavava na Kituo cha Afya Kitwiru ni miongoni mwa ahadi zilizotekelezwa. Sasa tunakuja tena na ahadi mpya za maendeleo kwa miaka mitano ijayo,” alisema Rubeya.
Kwa upande wake, Mgombea Udiwani wa Kata ya Kitwiru, Rahim Kapufi, aliahidi kuwasemea wananchi ndani ya baraza la madiwani.
“Nitahakikisha kituo cha afya kinakamilika, wanawake na vijana wanapata mikopo ya kuwawezesha kiuchumi, makazi yanasajiliwa rasmi na barabara za mitaa zinaboreshwa,” alisema K
No comments:
Post a Comment