Saturday, 5 November 2016

HOTUBA YA KAMATI YA BUNGE KUHUSU MUSWADA WA HABARI


HOTUBA YA KAMATI YA BUNGE KUHUSU MUSWADA WA HABARI

MAONI, MAPENDEKEZO NA USHAURI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA

HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII KUHUSU MUSWADA WA SHERIA WA

HUDUMA ZA HABARI WA MWAKA 2016

(THE MEDIA SERVICES BILL, 2016)

Friday, 4 November 2016
____________________

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kuwasilisha Maoni, Ushauri na Mapendekezo ya Kamati kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa Mwaka 2016 (The Media Services Bill, 2016).

Uwasilishaji huu ni kwa mujibu wa Kanuni ya 86 (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016. Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia Kanuni ya 84 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, uliipa Kamati jukumu la kushughulikia Muswada huu wa Sheria. Aidha, kabla ya kuanza shughuli hiyo muhimu, Kamati ilipata fursa ya kupokea Maelezo ya Serikali kuhusu Muswada tajwa kutoka kwa Mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) ambaye alieleza kuhusu madhumuni, sababu na mpangilio wa Muswada huu.

2.0 DHANA YA TAALUMA NA HUDUMA ZA HABARI

Mheshimiwa Spika, Kabla ya kuendelea napenda kutoa maelezo machache kuhusu Dhana na Chimbuko la Taaluma ya Habari na Huduma za Habari. Mheshimiwa Spika, Taaluma ya Habari ni moja kati ya Taaluma muhimu sana katika jamii yoyote kwani hutumika kuuhabarisha umma kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea yakiwemo ya kisiasa, kiafya, kielimu na hata kiuchumi. Habari ina nafasi kubwa katika jamii kwani inawezesha watu katika jamii husika kupata taarifa, habari na maarifa; kuzitumia kudadisi na kuhoji; kufikiri zaidi na kupembua na kuweza kuwa na maoni na kufanya maamuzi sahihi juu ya kile ambacho kinawagusa au kuwahusu. Mheshimiwa Spika, Taifa lenye watu wenye kupata habari sahihi kwa wakati sahihi linakua vizuri katika nyanja mbalimbali kama za kiuchumi, kisiasa na hata kiutamaduni. Kuna msemo usemao “Information is Power” kwa tafsiri isiyo rasmi ni “Taarifa ni uwezo au nguvu. Habari kwa upande mwingine inaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii endapo haikutolewa kwa kufuata misingi yake kwa maana ya habari gani itolewe kwa umma, namna ya utoaji na hata wakati gani wa kutoa habari hiyo.Mwandishi mmoja wa Kimarekani katika Tasnia ya

Habari aitwaye Eric Qulman aliwahi kusema “We don’t have a choice on whether we do Social Media, the question is how well we do it”. Hivyo basi ni muhimu kuwepo na utaratibu wa utoaji wa habari unaozingatia weledi na maadili. Mheshimiwa Spika, Vyombo vya habari vina wajibu wa kusimamia ukusanyaji, utayarishaji na utoaji habari kwa umma, Utoaji wa habari huu ni muhimu uzingatie weledi na maadili ya uandishi wa habari ili kuupa umma habari sahihi na za kweli na kuwawezesha kufanya angalau maamuzi sahihi katika wakati sahihi.

Mheshimiwa Spika, Dhana ya Huduma za Habari ni dhana iliyokuwepo miaka mingi iliyopita ndani na nje ya Bara la Afrika. Msingi mkubwa wa Dhana hii ni dhamira ya kuzingatia umuhimu wa usimamizi wa Tasnia ya Habari ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo na utoaji wa habari unaozingatia maadili na usiyo na athari kwa mtu yeyote katika jamii husika.

Mheshimiwa Spika, vyombo vya habari vipo vya aina nyingi kamavile magazeti, redio, televisheni, mitandao ya kijamii n.k. Katika utafiti wa Kamati, imebainika kwamba katika Bara la Afrika sehemu ya kwanza ya uchapaji (Printing Press) ilianza kazi mnamo Mwaka 1794 katika Mji wa Freetown uliopo Sierra Leone. Aidha, mnamo Mwaka 1800, gazeti la kwanza lilianza kuchapishwa nchini Sierra Leone na lilikuwa likiitwa “The Sierra Leone Advertiser”. Tangu hapo, nchi mbalimbali zikaanza kujikita zaidi katika kutoa huduma ya habari kupitia vyombo mbalimbali. Katika kuhakikisha kuna kuwa na usimamizi thabiti katika Tasnia ya habari, nchi hizo zikaanza kutunga sheria hii ya Huduma za Habari baada ya kuonekana kuwa hakuna usimamizi wa kisheria wa tasnia ya habari hali ambayo ilionekana kudhoofisha Tasnia hii.

Mheshimiwa Spika, Takwimu zinaonesha kuwa hapa nchini mnamo mwaka 1992, kulikuwa na magazeti 5 tu. Hata hivyo, kufikia mwaka 2013 kulikuwa na zaidi ya magazeti 700 ambayo yamesajiliwa, Stesheni za Radio zilizosajiliwa 128 na 53 ambazo zinafanya kazi. Aidha, Vituo vya Televisheni vilivyosajiliwa 54 na ambavyo vinafanya kazi (kurusha matangazo) 28 (Tibanyendera, 2014).

Mheshimiwa Spika, Vyombo hivi vya habari nchini ni vingi ambavyo bila ya kuwepo na sheria ya kuvisimamia kuna uwezekano kabisa wa baadhi ya vyombo hivyo kukiuka misingi na hata taaluma. Katika kufuatilia tumebaini kuwa nchi nyingi duniani zimetunga Sheria za kufanana na Sheria hii inayotarajiwa kutungwa ya Huduma za Habari, 2016. Nchi hizo ni pamoja na:- Sierra Leone (Seditious Libel Law of 1965), Russia (Law on Mass Media,1991), Slovenia (The Mass Media Act, 2001), Australia (Communications and Media Authority Act 2005), Kenya (The Media Act, 2007), Estonia (Media Services Act, 2011), Hungary (Media Services and Mass Communication Act, 2010)

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo hayo ni dhahiri kuwa kuna haja kabisa kwa nchi yetu kuwa na Sheria hii ambayo itakidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa katika kusimamia Tasnia hii muhimu nchini.

3.0 CHIMBUKO LA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI

Mheshimiwa Spika, Siyo mara ya kwanza kuwepo kwa pendekezo la Serikali la Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari hapa Bungeni.

Kwa mfano: Muswada wa kwanza wa Huduma za Habari uliwasilishwa Bungeni mnamo mwezi Machi Mwaka 1993 na aliyekuwa Waziri wa Habari na Utangazaji Mhe. William Shija (Marehemu). Muswada huu uliitwa Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Taaluma ya Habari (The Media Profession Regulation Bill, 1993) ukilenga kuweka mfumo wa Kisheria ambao ungewezesha kulinda Haki ya Msingi ya kupata Habari nchini. Hata hivyo, mwezi Septemba, 1993 Muswada huu uliondolewa Bungeni baada ya kukosolewa na Wabunge pamoja na Wadau mbalimbali nchini kwa kuwa ulionekana kuwa unaminya uhuru wa vyombo vya habari. Muswada huu ulipendekeza kuweka mchakato wa usajili wa wanahabari nchini pamoja na kuanzisha Baraza la Wanahabari ambalo lilikuwa na Mamlaka ya kuwaondoa wanahabari walioandikishwa kwenye orodha kwa mujibu wa vigezo ambavyo vingeainishwa kwenye kanuni ambazo zingepitishwa na Waziri baada ya kupata maoni ya Wadau pia. Aidha, Mchakato wa kuwasajili Wanahabari ulitaka Wanahabari wawe na Elimu ya ngazi ya cheti, astashahada, shahada au sifa zozote katika taaluma stahiki, pamoja na hayo Muswada uliweka sharti kwamba mtu asingeweza kusajiliwa kuwa Mwanahabai hadi pale Baraza litakapokuwa limejiridhisha kuwa taaluma na maadili ya mwombaji yanafaa kwa ajili ya kusajiliwa kuwa Mwanahabari.

Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 20 Februari, 2015, Muswada wa Sheria wa Huduma za Habari ulitangazwa kwenye Gazeti la Serikali, Toleo Na.8, Juzuu ya 96. Muswada huo ulisomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa 18 wa Bunge la Kumi. Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ile ya Muswada kuletwa kwa hati ya dharura, Muswada haukufika katika hatua ya pili. Hivyo basi, katika Bunge hili la Kumi na Moja (11) Muswada wa Huduma za Habari wa Mwaka 2016 (The Media Services Bill, 2016) umeletwa tena Bungeni na ulisomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Nne (4), tarehe 16 Septemba, 2016 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb), baada ya kuchapishwa katika Gazeti la Serikali, Toleo Na. 36, Juzuu ya 97 la tarehe 26 Agosti, 2016.

Mheshimiwa Spika, Kama ilivyoelezwa hapo awali, Muswada huu ulishawahi kuletwa Bungeni na kuondolewa, Kamati imebaini kuwa, kuondolewa huko kuliipa Serikali wasaa wa kufanya marekebisho mbalimbali kwa lengo la kuuboresha.

4.0 DHUMUNI LA MUSWADA

Mheshimiwa Spika, Tasnia ya habari ni moja ya Tasnia muhimu nchini ambayo imekuwa ikikua kwa kasi. Kama ilivyoelezwa awali kuhusu umuhimu wa habari, Muswada huu unapendekeza kutungwa kwa Sheria ya Huduma za Habari kwa madhumuni ya kuweka utaratibu wa kisheria katika tasnia ya habari, kuunda Bodi ya Ithibati ya wanahabari, kuunda Baraza Huru la Habari, kushughulikia masuala ya kashfa na makosa yanayohusiana na utangazaji.

5.0 UCHAMBUZI WA MUSWADA

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 84 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, mnamo tarehe 19 Oktoba, 2016, Kamati ilifanya Mkutano na Wadau kwa lengo la kupokea Maoni yao (Public hearing) ili kuisadia katika Uchambuzi wa Muswada huu.

Mheshimiwa Spika, Wadau mbalimbali walifika katika Mkutano huo lakini walishindwa kuwasilisha maoni yao kwa maelezo kuwa walikuwa hawajashirikishwa kwenye mchakato lakini pia wamepata taarifa ndani ya muda mfupi. Ni kwa msingi huo wadau waliomba waongezewe muda. Miongoni mwa wadau waliofika mbele ya Kamati ni Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jukwaa la Wahariri (Tanzania Editors Forum), Shirika la Kitaifa la Msada wa Kisheria (NOLA), Kituo cha Sheria cha Haki za Binadamu (LHRC), Chama cha Wanasheria Tanzania(TLS) na Umoja wa Vyama vya Michezo (UTPC).

Mheshimiwa Spika, Kamati ilitafakari ombi la Wadau hao na kuamua kuongeza muda wa siku 10 hadi kufikia siku ya Jumamosi, tarehe 29 Oktoba, 2016. Hata hivyo, kwa mara nyingine Wadau hao hawakuweza kufika kwenye Mkutano huo licha ya kukiri kupokea barua za mwaliko. Baadhi yao wadau hao ni: Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania

(UTPC) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF). Aidha, wadau hao waliandika barua kwako Mheshimiwa Spika kuomba waongezewe muda hadi mwezi Februari 2017. Hata hivyo, wapo baadhi ya Wadau ambao waliwasilisha maoni yao kwa njia ya maandishi, wadau hao ni pamoja na:- Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), Taasisi ya Twaweza pamoja na mtu mmoja mmoja.

Mheshimiwa Spika, napenda kulieleza Bunge lako Tukufu kuwa,Muswada huu ni moja kati ya Miswada ambayo imejadiliwa sana na wadau wa habari kupitia vyombo mbali mbali kama Redio, Televisheni na Magazeti. Mijadala hiyo imewezesha wadau wengi kufahamu umuhimu wa Muswada huu katika Tasnia ya Habari nchini.

Mheshimiwa Spika, Nawashukuru sana Wadau wote walioweza kutuma maoni yao kwa Maandishi na hata waliokuwa wanajadili kupitia vyombo vya habari kwani yamesaidia kuboresha Muswada huu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kupokea Maoni ya wadau, katika kikao cha tarehe 30 Oktoba 2016, Kamati ilifanya mashauriano na Serikali kwa lengo la kuzingatia maoni ya Kamati na wadau.

Mheshimiwa Spika, napenda kulieleza Bunge lako Tukufu kuwa, baada ya Kamati kukaa na kuchambua Muswada, pamoja na kusikiliza maoni ya wadau wa habari yaliyotolewa kwa njia ya maandishi na yale yaliyotolewa kwenye vipindi mbalimbali vya televisheni na redio,Kamati imependekeza mabadiliko ya Muswada kwenye maeneo yafuatayo: Fursa ya kukata rufaa Mahakamani pale mtu anapokuwa hajaridhika na Maamuzi ya Mkurugenzi wa Habari Maelezo na Waziri, Uwakilishi wanahabari kwenye Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari; Utaratibu wa usikilizaji wa malalamiko kabla ya hatua ya rufaa; Utaratibu wa kusikiliza kwa haraka kesi zitakazofunguliwa za makosa ya kashfa; Utaratibu wa kufanya upekuzi na ukamataji wa mashine na

mitambo zinazotumika kuchapisha huduma mbalimbali, na utaratibuwa kushughulikia makosa ya uchochezi.

Mheshimiwa Spika, maeneo yote hayo muhimu ambayo Kamati ilishauri yafanyiwe marekebisho Serikali imeyafanyia kazi kama inavyooneshwa katika jedwali la marekebisho la Serikali (Schedule of

Ammendments).

6.0 MAONI, MAPENDEKEZO NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa Maoni, Ushauri na Mapendekezo ya Kamati kama ifuatavyo kwa lengo la kuboresha Muswada huu:-

6.1 MAONI KUHUSU VIFUNGU

Mheshimiwa Spika, Kamati ina maoni yafuatayo:-

a) Kamati imebaini makosa ya uchapaji na sarufi (spelling and grammatical errorrs)

b) Ushauri: Marekebisho yafanyike kwenye maeneo yote yenye makosa hayo ili kuleta muundo na maana sahihi ya maneno hayo. Kwa mfano Kifungu cha 6 neno Ownsereship lisomeke

Ownership; Kifungu cha 7 (2) (a) (ii) neno inforcement linaloonekana kati ya maneno law na agent lisomeke enforcement na Kifungu cha 25 (2) neno excecution lisomeke execution.

c) Kifungu cha 3, tafsiri ya neno “content.”

d) Pendekezo: Kiandikwe upya ikijumuishwa maana ya kuchapishwa katika mithili ya kielekroniki ikijumuisha picha, michoro, katuni na nyingine ambazo ni mnato au zinazotembea (characters moving or still) ili kuweza kuleta maana fasaha inayokusudiwa katika sheria inayotungwa.

c) Kifungu cha 4 kinachohusu Director of Information Services Pendekezo: Kufuta jina “Director of of Information Services”kila linaposomeka katika Muswada huu na badala yake iandikwe na kusomeka“Director of Information Services Department” ili itambulike kwamba ni Idara siyo mtu binafsi anayejitegemea.

d) Kifungu cha 5 kinachohusu “Functions of the Director of Information Services “ Pendekezo: Kifungu kidogo (k) kiboreshwe kwa kuongeza mwanzoni mwa kipengele maneno yafuatayo“in collaboration with the relevant Government agencies na kuondoa neno “platforms”na hii ni kutokana na ukweli kuwa kuna Taasisi nyingine ambazo zinahusika na kusimamia Tovuti ya Taifa hivyo ni muhimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo akashirikiana nao.

e) Kifungu cha 7 kinachohusu “Obligation of Media Houses”,

Pendekezo:

• Kifungu kidogo cha (1a) na (1b) kuongeza kifungu kidogo (vi) “maintain accountability and transparency in funding” na kufanya vipengele vidogo kuongezeka kufikia sita (6) ili kipengele hicho kiweze kusimamia uwazi na uwajibikaji kwa vyombo vya habari.

• Kifungu kidogo cha (2) kuongeza kifungu (c) kitakachosomeka “does not constitute to hate speech as stipulated under the Penal Code” ili kuweka masharti katika Sheria hii ya kutambua makosa yanayotokana na kutoa matamshi ya uchochezi ambayo yanaweza kuhatarisha amani.

• Kifungu kidogo (2) (h) kiboreshwe kwa kukiandika upya ili kupata maana sahihi iliyokusudiwa

e) Kifungu cha 8 kinachohusu “Print Media Licensing”.

Pendekezo: Kifungu kidogo cha 2 kifutwe kwa kuwa maudhui ya kifungu hicho yameelezwa vizuri kwenye Kifungu cha 60 ambacho ndiyo kifungu sahihi cha Waziri kutunga Kanuni.

g) Kifungu cha 9 kinachohusu “Power to reject applications and cancellation of license”.

Pendekezo: Kuwepo na fursa ya kukata rufaa pale ambapo mlalamikaji atakuwa hajaridhika na maamuzi ya Mkurugenzi wa Habari Maelezo ya kukataa maombi ya leseni au kuifuta leseni

hiyo ya Mwombaji. Kifungu kisomeke “Any person aggrieved by the decision of the Director of Information Services Department under section 9 may, within thirty days from the date of such 
decision, appeal to the Minister.” Na endapo hataridhika kwa Waziri mwenye dhamana basi kuwepo na kifungu kitakachomruhusu kukata rufaa Mahakama kuu kwa kufanya hivi itakuwa imempa mlalamikaji haki yake Kikatiba ya kusikilizwa (Kifungu 10 kipya “Appeals against decision of the Director”) h) Kifungu cha 10 kinachohusu “Journalist Accreditation Board” kifungu kidogo cha 2.

Pendekezo: Kiongezwe kifungu kidogo (d) kitakachosomeka “doing all or such others acts and things which a body corporate may lawfully perform, do or suffer to be done”.

i) Kifungu cha 11, kinachohusu “Composition of the Board”.

Pendekezo:

• Kifungu kidogo 1 (f) kiboreshwe ili wajumbe hao wa Bodi ambao ni waandishi wa habari wenye uzoefu mmoja atoke kwenye Private Media House na mwingine atoke kwenye Public Media House.

• Kiongezwe kifungu kidogo cha 4 ambacho kitasomeka “The Minister may, by order published in the Gazzette amend the Schedule to this Act” ili kutoa nafasi kwa Waziri kufanya marekebisho kwenye jedwali.

j) Kifungu cha 12 kinachohusu “Functions of the Board”.

Pendekezo:

• Kifungu kidogo (e) kufuta neno“training” ambalo lipo kati ya maneno relevant na Institutions kwa kuwa vyuo hivyo vipo chini ya mamlaka nyingine kama Shirikisho la Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Vyuo Vikuu Tanzania (NACTE). Hivyo, Baraza hilo litafanya ushauri rejea na

mamlaka hizo.

• Kuongeza kipengele (i) to administer the accounts, assets and liabilities of the Board and (j) to carry such other functions as the Minister may direct. Vifungu hivi vitasaidia kuongeza jukumu la Bodi katika usimamizi wa fedha pamoja na rasilimali zake zote.

k) Kifungu cha 13 kinachohusu Powers of the Board.

Pendekezo: Kiongezwe kifungu kipya (a) “establish such number of committees as may be necessary for the better carrying out their functions” ili kuipa Bodi mamlaka ya kuunda Kamati kwa ajili

ya kuendesha shughuli zake au majukumu yake mbalimbali.

l) Kifungu cha 18 kinachohusu “Accreditation of Journalists”, Pendekezo: Kifungu kidogo cha (3) kiboreshwe ili Waandishi wa Habari ambao siyo raia wa Tanzania kuongezewa muda kutoka siku 60 (miezi 2) hadi 90 (miezi 3). m) Kifungu cha 22 kinachohusu “Sources of the Fund”, Pendekezo: Kifungu kidogo (a) kifutwe kwa kuwa ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa mifuko kama hii kuwa na vyanzo vyake vya mapato na siyo kupata fedha zinazoidhinishwa na Bunge, mfano mzuri ni Sheria ya Wataaluma wa Kemia ya Mwaka 2016, ambapo mfuko wa Baraza la wanataaluma hao ni wa

kujitegemea na siyo kutoka katika bajeti ya kupitishwa na Bunge.

n) Kifungu cha 25 kinachohusu “Functions of the Council” Pendekezo: Kifungu kidogo (a) (i) kirekebishwe kwa kuongeza neno“set” na kufuta maneno prepare and adopt kwa kuwa kazi

hiyo inafanywa na Bodi.

o) Kifungu cha 26 kinachohusu “Committees of the Council”.

Pendekezo: Kifungu kidogo (3) kifutwe kwa sababu ya kuwepo kwa kifungu kipya cha 27 (1) & (2) ambacho kitakidhi matakwa hayo.

p) Kifungu cha 26 kinachohusu “Committees of the Council. Pendekezo: Katika kifungu kidogo (1), yaongezwe maneno “a Secretariat and… after the word establish ili Sekretarieti hii ianzishwe kisheria.

q) Kifungu cha 27 kinachohusu “Appeals”.

Pendekezo: Maboresho yafuatayo yazingatiwe:

• Kifungu kidogo (1) kisomeke “A person aggrieved by content of a print media, may, within three months, from the date of publication of the content, make a written complaint to the Complaint Committee” ili kumpa nafasi ya kuweza kuwasilisha malalamiko yake.

• Kifungu kidogo (2) kiseme “The Complaints Committee shall hear and determine the matter in accordance with the rules set out by the council.”

r) Kifungu cha 29 kinachohusu “Appointment of Secretary to the Council”.

Pendekezo: Katika kifungu kidogo cha 2 muda wa kukaa madarakani kwa Katibu wa Baraza uwe ni miaka 5 badala ya miaka 3.

s) Kifungu cha 38 kinachohusu Redress for defamation Pendekezo:

• Kifungu cha 3 kirekebishwe kwa lengo la kuitaka mahakama kusikiliza kesi za kashfa zinazowasilishwa chini ya sheria ndani ya muda mfupi iwezekanavyo.

• Kuongeza kifungu kipya kidogo cha 4 kitakachompa Jaji Mkuu mamlaka ya kuandaa kanuni ambazo zitaweka utaratibu wa kusikiliza kwa haraka kesi zinazotokana na makosa ya kashfa

t) Kifungu cha 47 kinachohusu “Offences relating to Media Services”

Pendekezo: Kifungu kidogo (2) (d) kifutwe kwa kuwa kosa hili tayari limezingatiwa katika kifungu cha 50 (1) (c).

u) Kifungu cha 50 kinachohusu “Seditious Offences”

Pendekezo:

• Kifungu kidogo cha (1) (c) kirekebishwe ili kiweze kumlinda mtu ambaye kazi yake ni kuchapisha ambaye siyo mmiliki wa chapisho hilo na badala yake kimwajibishe mmiliki wa chapisho na wakati huohuo ana mitambo ya kuchapisha.

• Kifungu kidogo (4), (9), (10) na (11) vifutwe kwa sababu havina msingi.

v) Kifungu cha 52(1) kinachohusu “Offences by corporations or societies”

Pendekezo: Kiandikwe upya ili kuweka ukomo wa adhabu badala ya kukiacha kuwa na adhabu isiyo na mwisho. Aidha Kamati inashauri kuongeza neno not baada ya neno but ili kuweka ukomo huo na kusomeka….not exceeding twenty five million shillings.

w) Kifungu cha 53 kinachohusu “Liability of the Employer or Principal”,

Pendekezo: Kiboreshwe ili kuondoa utata wa maana iliyokusudiwa x) Kifungu cha 56 kinachohusu “Powers of Seizure”

Pendekezo: Kiboreshwe ili kuhakikisha utaratibu wa kufanya upekuzi na ukamataji unaotumika katika sheria mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia masharti yaliyoainishwa kwenye Sheria ya

Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura ya 20 yaweze kutumika katika Sheria hii, pia kuweka utaratibu mahsusi utakaotumika katika ukamataji wa mitambo au mashine zinazotumika kuchapisha huduma mbalimbali y) Kifungu cha 60 kinachohusu “Regulations”,

Pendekezo: kifungu kidogo cha (2) (f) kiboreshwe ili kuweka sharti la vigezo vya ithibati kuzingatiwa katika utungaji wa Kanuni

6.2 MAONI YA JUMLA

6.2.1 Kuzingatia Weledi

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Azimio la Haki za Binadamu, kifungu cha 19 la Mwaka 1948 (Universal Declaration of Human Rights, Article 19) limesisitiza umuhimu wa haki ya kutoa maoni na kupata habari ambayo nukuu yake ni kama ifuatavyo:-“Everyone has the right to freedom of opinion and expression, this right includes freedom to hold opinions without interference and to seek, receive and impart information and ideas through any media and regardless of frontiers”. Hakuna Haki isiyo na Wajibu, pamoja na Azimio Kamati inatoa Rai kwa Vyombo vya habari kutoa habari kwa kuzingatia misingi bora ya Taaluma ya Habari.



6.2.2 Uandishi wa Habari

Mheshimiwa Spika, kumezuka tabia ya baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari ambazo mara nyingi zimekuwa zikidhalilisha watu mbalimbali katika jamii. Mwanaharakati wa kutetea haki za Binadamu Malcolm X aliwahi kusema “The media is the most powerful entity on earth, they have the power to make the innocent guilty and the guilty innocent, and that is power because they

control the minds of the masses”. Kamati inatoa angalizo kwa wana tasnia ya habari kuwa ni vyema sasa tabia hii ikaisha kwani kwa mujibu wa Kifungu cha 47 chombo hiko kitakuwa kimetenda kosa na kitachukuliwa hatua.

16

6.2.3 Mavazi (Dress Code)

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Serikali kwa kuja na Muswada huu kwani utaifanya taaluma hii iwe ya kuheshimika kama zilivyo taaluma nyingine. Pamoja na uvaaji wa vitambulisho ni vyema kwenye Kanuni ikaelezwa kuhusu Mavazi (Dress code) ya wanataaluma hii kwani mwana tasnia ya habari ni kioo cha jamii kwa namna moja au nyingine. Kuna mifano mizuri ya kuigwa kutoka

kwa Wanataaluma nyingine nyingi wakiwemo Wanasheria, Madaktari na Wauguzi nikiwataja kwa

uchache.

6.2.4 Usajili wa Waandishi wa Habari (Accreditation) Mheshimiwa Spika, Katika Mkutano wa Nne Bunge lako Tukufu lilitunga Sheria ya Wanataaluma ya Kemia ya Mwaka 2016 (The Chemist Professionals Act, 2016) ambapo kuliundwa Baraza la Wanataaluma wa Kemia kwa lengo la kusimamia wanataaluma wa Kemia kwa kuwasajili kutokana na wimbi la vitendo vilivyokuwa

vinafanywa na watu ambao sio waaminifu. Uthibitishaji (Accreditation) wa Waandishi wa Habari haina tofauti na Wanataaluma wa Kemia kwani lengo ni kuwatambua.

Hivyo basi kupitia sheria hii inayotarajiwa kutungwa liundwe Baraza la Wanahabari ili lipate kusimamia misingi ya tasnia hiyo.

7.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha Maoni, Ushauri na Mapendekezo ya Kamati kuhusu Muswada huu wa Huduma za Habari, 2016.

17

Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia James Wambura (Mb), Naibu Waziri, Ndg. Prof. Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu, Ndg. Nuru Milao, Naibu Katibu Mkuu na watendaji wote wa Wizara kwa ushirikiano wanaoipa Kamati katika utendaji kazi wake wa kila siku pamoja na kuwasilisha vyema Muswada mbele ya Kamati na kutoa ufafanuzi mzuri. Namshukuru pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Watendaji wake Ndg. Shaban Kabunga na Optat Mrina kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kutoa mwongozo wa kisheria wakati wote wa uchambuzi wa Muswada.

Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kuwashukuru tena Wadau wote waliotuma maoni yao kwa njia ya maandishi kwani maoni hayo yamesaidia kupata sheria hii muhimu kwa Maslahi mapana ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee nawashukuru sana Wajumbe wa Kamati kwa weledi na umahiri waliouonesha wakati wa uchambuzi wa Muswada huu.Wajumbe wamefanya kazi nzuri na

kubwa na kujitoa hata siku za mapumziko kuhakikisha Muswada huu unakuwa hivi kwa maslahi ya Taifa zima. Napenda kuwatambua Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa majina kama ifuatavyo:-

1. Mhe. Peter J. Serukamba, Mb Mwenyekiti

2. Mhe. Mussa A. Zungu, Mb M/Mwenyekiti

3. Mhe. Hussein Mohamed Bashe, Mb Mjumbe

4. Mhe. Peter Ambrose Lijualikali Mjumbe

5. Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi, Mb Mjumbe

6. Mhe. Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile Mjumbe

7. Mhe. Kasuku Samson Bilago, Mb Mjumbe

8. Mhe. Dkt. Elly Marko Macha, Mb Mjumbe

9. Mhe. Lucia Ursula Michael Mlowe, Mb Mjumbe

18

10. Mhe. Dkt. Jasmine Tiisekwa, Mb Mjumbe

11. Mhe. Ahmed Ally Salum, Mb Mjumbe

12. Mhe. Susan Anselm Lyimo, Mb Mjumbe

13. Mhe. Juma Selemani Nkamia, Mb Mjumbe

14. Selemani Said Bungara, Mb Mjumbe

15. Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, Mb Mjumbe

16. Mhe. Boniphace Mwita Getere, Mb Mjumbe

17. Mhe. Bernadetha K. Mushashu, Mb Mjumbe

18. Mhe. Jaku Hashim Ayoub, Mb Mjumbe

19. Mhe. Grace Victor Tendega Mjumbe

20. Mhe. Sikudhani Yassin Chikambo Mjumbe

21. Mhe. Hussein Nassor Amar Mjumbe

22. Mhe. Savelina Sylvanus Mwijage Mjumbe

Mheshimiwa Spika, mwisho lakini sio kwa umuhimu napenda kumshukuru Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, Mkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bunge Ndg. Athuman B. Hussein, Mkurugenzi

Msaidizi wa Kamati Ndg. Dickson M. Bisile pamoja na Makatibu wa Kamati Ndg. Pamela Pallangyo na Ndg. Agnes Nkwera; na Msaidizi wao Ndg. Gaitana Chima kwa kuratibu vyema shughuli za Kamati na

kuhakikisha Taarifa hii inakamilika kwa wakati. Aidha, namshukuru Kaimu Mshauri Mkuu wa Mambo ya Sheria wa Bunge Ndg. Pius T. Mboya pamoja na wasaidizi wake Ndg. Stephano Mbutu na Ndg.

Mariam Mbaruku kwa Uchambuzi wa kisheria walioufanya kuisadia Kamati.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na naomba kuwasilisha. Peter Joseph Serukamba, Mb



MWENYEKITI KAMATI YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII

4 Novemba, 2016

Why Donald Trump draws crowds, Hillary Clinton doesn't


Some analysts believe many are simply reluctant to admit they're on Hillary Clinton's side.


Clinton is seeking the company of stars like Pharrell Williams and Bernie Sanders to draw crowds [Brian Snyder/Reuters]
by



It makes fans of Hillary Clinton very anxious every time I state this simple fact: attendance at the Democratic candidate's rallies is mediocre at best.

The pictures have told the story over the past six months. Republican Donald Trump is filling convention centres, airport hangars and parks. Clinton, on the other hand, is filling community centres and small colleges, but just barely.

The people campaigning for her - the rock stars of the Democratic Party like First Lady Michelle Obama, President Barack Obama and Vermont Senator Bernie Sanders - have bigger and more energetic crowds.

Moreover, as Clinton goes into the final weekend of campaigning, she is drawing on mega-celebrities to attract people to her cause by holding separate events with musicians Pharrell Williams, Jay Z and Katy Perry.

There was a momentary spike this past week in Tempe, Arizona where, aside from July's Democratic National Convention, she had one of her biggest rallies yet.

More than 10,000 people attended an event where she went solo. But you could chalk that up to the fact a Democratic presidential nominee in Arizona is rare. Unlike Florida, North Carolina, Pennsylvania, Wisconsin, New Hampshire and other battleground states, Arizonans aren't bombarded with campaign stops.

Clinton rallied in Winterville, North Carolina, on Thursday [Chris Sheridan/Al Jazeera]


Conservative media and Trump himself have pointed to the smaller size of the rallies and bring it up all the time.

"I have to say, we have rallies like this and we have seven, eight, nine, ten thousand routinely," he boasted back in September at a stop in North Carolina. "Hillary goes out for rallies and yesterday I think she had 200 people, maybe 300."

But some analysts believe that, contrary to Trump's persistent assertion that there's a "silent majority" in the US who want him to win, the opposite may be true and that could explain at least some of the low numbers at Clinton rallies.
Proud Trump supporters

There is no doubt Trump supporters are proud to say they're voting for him. That's been evident since the beginning of his campaign.

But Lara Brown, an associate professor of political management at George Washington University, argues size doesn't necessarily matter.

"Trump is a novelty and for some, to say that they went is like saying they went to a sporting event," she argues. "Trump has also regularly been going to places where he is most beloved, not where the ground game is most competitive."

Other analysts believe many are simply reluctant to admit they're on Clinton's side.

The controversies surrounding her - the use of a private email server while secretary of state, allegations she gave special access to world leaders while in government in exchange for donations to her family's foundation and, more recently, a FBI investigation into her staff emails - have made it harder for people to show their love.


"I've had a number of students tell me that they're reluctant to be too public or too publicly enthusiastic over their support for Clinton," says Chris Galdieri, assistant professor at St Anselm College in New Hampshire. But he believes the support is there.

"My wife recently took our daughter to see Clinton at an event here in New Hampshire," he says. "And met women from New Hampshire and other states who had brought their daughters with them specifically to see Clinton, because there's a good likelihood she will be the first woman president."

The Clinton campaign insists they've baked in the small numbers into their strategy. At a stop in Winterville, North Carolina, I asked one of Clinton's top aides whether she's concerned about the mediocre attendance.

"We've gone into less populous parts of the state for a reason," said Jennifer Palmieri, Clinton's communications director. "There are voters in this area [North Carolina] that we want to turn out so if you go to a place where there aren't as many people who live there, you aren't likely to get the crowds."

On a Friday conference call with reporters, Robby Mook, Clinton's campaign manager, said they've had success in early voting getting people who haven't cast a ballot much in the past - so-called "low propensity voters" - to come out to the polls.

But on the same call campaign officials barely addressed questions about reports that African-American early voting is down from 2012. That's a key group of people for Clinton.

At the end of the day, the voting booth is where the attendance really counts.

"Enthusiasm is great, but it doesn't predict the result," says Brown.


Source: Al Jazeera News

MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WASOMWA MARA YA PILI






Na Eleuteri Mangi- MAELEZO


Muwada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 umesomwa mara ya pili Bungeni mjini Dodoma ukiwa na lengo la kuifanya tasnia ya habari nchini kuwa taaluma kamili.


Wiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema hay oleo Bungeni Dodoma alipokuwa akiwasilisha Muswada huo, huku akisisitiza kuwa una sehemu kuu nane ambazo zinaufanya kuleta mageuzi katika tasnia ya habari nchini na kuifanya kuwa taaluma kamili itayowaletea heshima wanahabari na tasnia hiyo kwa ujumla. 


“Hatuwezi kwa na vyombo vya habari makini kama hatutakuwa na wanahabari wenye taaluma ya habari nchini” alisema Nape.


Katika kuonesha ushirikishwaji wa wadau katika kutoa maoni yaliyolenga kuboresha Muswada huo, Waziri Nape amesema kuwa kumekuwa na ushirikishwaji mkubwa wenye wigo mpana kutoka kwa mwananchi mmoja mmoja, wanataaluma wa habari, wanasheria kupitia Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa Wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT) na Taasisi ya Wanahabari Kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania (MISA-TAN).


Wadau wengine walitoa maoni yao ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Sikika, Wabunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na michango ya Wabunge kupitia Kamati nyingine ambao umesaidia katika kuboresha Muswada huo wenye dhamira ya kuleta ufanisi katika sekta ya habari. 


Miongoni mwa maeneo ambayo wadau hao wameyafanyia maboresho ili Muswada uwe na tija ni pamoja na kuainisha haki na wajibu wa wananhabari ikiwemo uhuru wa kukusanya, kuhariri na kuchapisha au kutangaza habari pamoja na kuainisha haki ya chombo cha habari kukata rufaa kwa kuzingatia mfumo wa wazi na wa kidemokrasia kupitia vyombo vya kutoa haki ikiwemo mahakama huku Jaji Mkuu akiweka utaratibu wa kusikilizwa haraka kwa kesi za masuala ya kihabari.


Maboresho mengine yaliyofanya ni uwakilishi wa wanahabari katika Bodi ya Ithibati kwa kuzingatia uwiano wa wajumbe kutoka sekta ya habari ya umma na ya binafsi, kuviondolea adhabu vyombo vya habari au wamiliki baadhi ya makosa ya mwandishi ambapo atawajibishwa na Bodi ya Ithibati akiwa yeye ni mwanataaluma kamili kukutenda makosa ya kimaadili na vyombo vya dola kukamata mitambo na vifaa vya wanahabari maboresho yanaonesha kazi hiyo sasa itafanywa na Jeshi la Polisi kwa sheria ya Mwenendo wa Mkosa ya Jinai badala ya kazi hiyo kufanywa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari. 


Zaidi ya maboresho hayo, Waziri Nape ameongeza kuwa maboresho mengine ni kuhusu mitambo kutohusika moja kwa moja kwa kosa la gazeti ambalo limechapisha habari yenye makosa ya kisheria dhidi ya watu au taasisi mbalimbali.


Waziri Nape amefafanua kuwa chimbuko, muktadha na mchakato wa kuandaa Muswada huo unatokana na baadhi ya vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 1984 ambapo haki ya kikatiba ya kutafuta, kupokea na kutoa habari imeainishwa kwenye Ibara ya 18 (b) pamoja na mikataba mbalimbali ya kimataifa ya inayoainisha haki na wajibu wa sekta ya habari. 


Mkatabahiyo ya Kimataifa ni ule wa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966 ambao Tanzania iliuridhia Juni 11, 1984 pamoja na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu 1981 ambao nao uliridhiwa Februari 18, 1984.


Akinukuu maneno mbalimbali ya watu maarufu duniani juu ya masuala ya habari akiwemo Rais wa Marekani Thomas Jefferson Januari 16, 1789, Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Muasisi wa Taifa la India Mahatma Ghandhi, Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill (1806-1873) pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Waziri Nape akinukuu maneno ya mmoja wa viongozi hao Mahatma Ghandhi aliamini kuwa uhuru wa kweli wa kujieleza ni ule unaoweka mbele heshima ya watu wengine na kuwalinda dhidi ya dhara, kebehi, kejeli na madhara mengine huku Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill akibainisha dhima ya uhuru wa vyombo vya habari na umuhimu wa kuwa huriu unapaswa kuzingatia ukomo wa haki ya kupata habari kuwa unakoma pale haki za watu wengine zinapoanzia.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba amesema kuwa kamati yake imeufanyia kazi Muswada huo kupitia maoni ya wadau na watu mbalimbali nchini ambayo ndio yamakuwa msingi wa kuuboresha muswada huo.


Serukamba aliongeza kuwa kati ya miswada ambayo wananchi wengi wameisoma na kusikilizwa ni Muswada habari ambao umejadiliwa kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari; kwenye magazeti, kwenye radio na Televisheni kupitia vipindi maalum vya kujadili Muswada huu na maoni yao mengi yameingizwa kwenye Muswada huu” alisema Serukamba.

FILAMU NA TAMTHILIA ZA KITANZANIA ZAZINDULIWA, ZITARUSHWA NA DSTV




Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ali Mpungwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Filamu na Tamthilia za Kitanzania zitakazorushwa na DSTV kupitia Chaneli yao kuanzia Maisha Magic Bongo Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana. 




Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati wa uzinduzi huo.



Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo akizungumza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi.



Mtendaji Mkuu wa Multchoice, Chande Maharage, akizungumza kwenye uzinduzi huo.



Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi akizungumza kwenye uzinduzi huo.



Mkurugenzi Mkuu MNET, Yalisa Phawe akitoa hutuba fupi katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi.



Wadau wa filamu wakiwa kwenye uzinduzi huo.



Viongozi mbalimbali walioshiriki uzinduzi huo.



Wasanii wa filamu na wadau mbalimbali wakiwa kwenye 


uzinduzi huo.



Taswira katika uzinduzi huo.



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) na viongozi wengine wakizindua Filamu na Tamthilia za Kitanzania.






Na Dotto Mwaibale



TANZANIA imeingia katika mapinduzi makubwa ya tasnia ya filamu baada ya Maisha Magic Bongo kwa kushirikiana na Multchoice Tanzania pamoja na maprodyusa kuzindua rasmi chaneli yao (160) Maisha Magic Bongo itakayo kuwa ilirusha filamu na tamthilia za kitanzania.


Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu na Tamthilia za kitanzania kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo alisema mpango wa kurusha filamu za kitanzania kupitia mtandao wa DSTV utasaidia sana kutangaza filamu zetu na kuleta ushindani katika ulimwengu wa kimataifa.


"Serikali tunaona hili ni jambo muhimu sana litakalowafanya wadau wa kazi za kitanzania kutabasamu tena kwani sote tunafahamu umaarufu wa chaneli zilizopo DSTV na jinsi zinavyoweza kuwafikia watu wengi duniani" alisema Fissoo.


Aliongeza kuwa uzinduzi huo uliohusisha filamu sita, tamthilia mbili na kazi nyingine mbili DSTV wametoa mtaji wa dola za kimarekani 450,000.






Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi alisema uzinduzi huo umelenga kusherehekea kazi nzito za maprodyusa wa filamu hapa nchini na utambulisho rasmi wa chaneli yetu yenye maudhui ya kitanzania.


Alisema chaneli hiyo imelenga kuburudisha na kuelimisha watamazaji wa kitanzania kupitia filamu, tamthilia na maigizo mbalimbali ya kiswahili.


Aliongeza kuwa chaneli hiyo itapatikana kwenye kifurushi cha huduma za DSTV (160).


Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ali Mpungwe alisema DSTV Tanzania imetoa ajira 80 hivyo kusaidia katika maendeleo ya nchi.


Mtendaji Mkuu wa Multchoice, Chande Maharage alisema mpango huo utasaidia kukuza lugha ya kiswahili kama alivyokuwa akifanya mtunzi wa mashairi hayati marehemu Shabani Robert katika kukuza lugha hiyo.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...