Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege akizungumza na waandisshi wa habari kuhusu SIku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Kushoto ni Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile.(Picha na Modewjiblog)
Siku za Uhuru wa Vyombo vya Habari ambayo hufanyika Mei 3 ya kila mwaka inataraji kufanyika jijini Mwanza kwa mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman na kuhudhuliwa na viongozi wengine nchini na wengine kutoka nje ya nchini ambapo kwa mwaka huu kaulimbiu ni KUPATA TAARIFA NI HAKI YAKO YA MSINGI.
Akizungumzia sherehe hizo katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege amesema sherehe za mwaka huu zinataraji kuwa na wageni zaidi ya 250 akiwepo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues.
Aidha Berege amesema kuwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mwaka huu itafanyika kwa siku mbili, Mei, 2 kutakuwa na kongamano ambalo litatumika kujadili hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini na Mei, 3 ndiyo itakuwa siku husika ya maadhimisho.
“Kikawaida huwa kuna mambo tunafanya katika siku hiyo, tutawakumbuka waandishi wa habari waliopoteza maisha kazini, tutawakumbuka waandishi wa habari maveterani na waandishi wa habari waliopatwa na matatizo wakiwa kazini ... kwa mwaka huu tutakuwa na mambo ya kipekee tofauti na miaka iliyopita,” amesema Berege.
Pia ameongeza kuwa watapitia sheria zinazohusu uhuru wa vyombo vya habari kama Cyber Crime Act 2015 na Sheria ya Takwimu 2015 pia kuipitia miswada ya huduma ya vyombo vya habari na uhuru wa kupata taarifa.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la JAMHURI na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile akizungumzia hali ya uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata taarifa ilivyo nchini. Kulia ni Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga, Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege na Ofisa Miradi katika Kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizelege.
Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga akizungumza jinsi TMF inawasaidia waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile. Kulia ni Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege na Ofisa Miradi katika Kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizelege.
Ofisa Miradi katika Kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizelege akizungumzia ushiriki wa UNESCO katika kuandaa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo kwa mwaka huu zinafanyika Mwanza. Kushoto ni Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege na Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma-Ledama akieleza kazi za Umoja wa Mataifa ili kuvisaidia vyombo vya habari kupata uhuru wa kufanya kazi bila kuingiliwa.
Baadhi ya waandishi wa habari na watumishi waliohudhuria mkutano huo.