Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati) akiwasili katika ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia) pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez kwa ajili ya kuzindua rasmi ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Nyuma yao ni Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF), Dk. Tausi Kida.
Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa umesema kwamba utaendelea kuisaidia serikali ya Tanzania katika kutanzua changamoto za maendeleo zinazoikumba nchi hii.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja huo (UNDP), Alvaro Rodgriguez wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2014 mwishoni mwa wiki.
Ripoti hiyo imeandaliwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na jamii- ya ESRF kwa ufadhili wa UNDP na inagusia changamoto za Maendeleo .