Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam, juu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka.
WAKATI tukielekea katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa katika uhifadhi wa mazingira ambapo asilimia 61 ya nchi inakabiliwa na jangwa.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho hayo ambayo huadhimishwa Juni 5 kila mwaka.
“Tukielekea kwenye maadhimisho ya siku ya Manzingira Duniani, hali ya uhifadhi wa mazingira nchini inachangamato kubwa, asilimia 61 ya nchi yetu inakabiliwa na jangwa,” amesema Makmaba.
Amesema sababu ya hali hiyo nikutokana na kilimo, ufugaji na uvuvu usioendelevu ambao umepelekea upotevu wa viumbe hai, kuaharibiwa kwa vyanzo vya maji, kupunguwa kwa tija za shughuli za uzalishaji mali na uharibifu wa mazingira.
Ameeleza kuwa hali hiyo imepelekea hata kutokea kwa magonjwa amabyo ahayakuwepo ambapo alitoa mfano ni kuwepo kwa ugonjwa wa malaria katika maeneo ya milimani tofauti na awali.
Akizungumzia maadhimisho hayo, waziri Makamba amesema lengo ni kuelimisha jamii, masuala mbalimbali yahusuyo mazingira, kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za maadhimisho hayo, kuhamasisha jamii kuwa mstari wa mbele kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda mazingira ya maeneo yao.
Pia amesema ni kutoa fursa kwa jamii mbalimbali kufahamu wajibu wao wa kuzuia madhara kwenye mazingira yanayotokana na shughuli za kijamii wanazofanya na kuhamasisha jamii kuyafanya mazingira yao kuwa salama na masafi ili kila mtu afurahie hali hiyo katika maisha ya sasa na ya vizazi vijavyo ambapo kimataifa yanafanyika ichini India katika mji wa New Delhi huku kitaifa yakifanyika jijini Dar es Salaam.
Makamba amesema lengo la maadhimisho haya kitaifa kufanyika jijini Dar es Salaam ni kuwapa fursa wananchi wa jiji hilo ya kuelemishwa na kuhamasishwa kupambana na changamoto za uharibifu wa mazingira unaolikumba jiji hilo kama vile, mafuriko, uchafuzi wa mazingira utokanao na plastiki, kubomoka kwa kuta za fukwe za bahari ya hindi pamoja na utumiaji wa kiasi kikubwa cha nishati ya mkaa.
Amesema kutokana na changamoto mbalimbali zinazokabili uhifadhi wa mazingira nchini, kuelekea siku ya maadhimisho hayo kutatanguliwa na wiki ya mazingira itakayo zinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Mei 31 hadi Juni 5, 2018 katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kutakuwepo na maonesho ya nishati mbadala ya mkaa na Teknolojia.
Ameongeza kuwa wajasiriamali na wataalamu wa teknolojia ya nishati mbadala wa mkaa watatoa mafunzo kwa jamii na kuwahamasisha kutumia nishati mbadala ya mkaa na maadhimisho hayo yatafungwa na Rais John Magufuli siku ya kilele Juni 5, 2018.