Diwani wa VitiMaalum Tarafa ya Kasanga kutoka Mninga katika Kijiji cha Mkalala, Asumpta Adriano Mtende akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi hivi karibuni. (Picha na Friday Simbaya)
`
|
Na Friday Simbaya, Mufindi
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa imeanza kuboresha huduma za afya vijijini kwa kukatarabati na kujenga miundombinu muhimu katika vituo vyake mbalimbali vya afya ili kusogeza huduma hizo karibu na wananachi.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Festo Elia Mgina hivi karibuni watika wa Kikao cha Baraza la Madiwani cha mwaka, ambapo pamoja na mambo mengine kikao hicho kilipitia taarifa ya utekeleazji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018.
Mkutano huo wa Baraza la Madiwani ulikuwa na agenda ya uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa halmashauri ambapo Diwani wa Kata ya Sadani, Ashery Mtono alichaguliwa kuwa makamu mweneyekiti mpya wa halmashauri hiyo pamoja na uundwaji upya wa kamati za kudumu za halmashauri.
Alisema kuwa halmashauri hiyo imeanza kuboresha utoaji wa huduma za afya vijijini kwa kuboresha vituo vya afya ili kusogeza huduma hizo karibu na wananchi kwa kuzingatia kuwa halmashauri hiyo haina hospitali ya wilaya.
Mgina alisema kuwa halmashauri hiyo haina hospitali ya wilaya baada ya Wilaya ya Mufindi kuganyika na kuzaliwa kwa Halmashauri ya Mji Mafinga na Hospitali ya Mafinga ya Wilaya kuwa chini ya halmashauri hiyo mpya.
Alisema kuwa awali, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ilikuwa inatumia Hospitali ya Mafinga kama hospitali yake ya wilaya lakini kutokanana mgawanyiko huo kwa sasa ipo chini Halmashauri ya Mji Mafinga.
Alifafanua kuwa ili kusongeza huduma za afya karibu na wanannchi na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Mafinga, halmashauri hiyo imeanza kukarabati na kujenga miundombinu muhimu katika vituo mbalimbali vya afya.
Mgina alisema kuwa katika Kituo cha Afya cha Malangali wamejenga jengo la akina mama la kujifungulia, maabara pamoja na nyumba ya mtumishi.
Aidha, katika kituo kingine cha Afya cha Ifwagi pia wamekarabati na kujenga miundombinu muhimu hususan jengo la upasuaji, jengo la akina mama kujifungulia, maabara na nyumba ya mtumishi kwa kushirikiana na serikali kuu pamoja na wadau wa maendeleo mbalimbali.
Aliongeza kuwa kupitia mpango wa ‘force account’, serikali kuu imetoa shilingi milioni 400 (400,000,000/-) kwa kila kituo cha afya yaani Malangali na Ifwagi kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu muhimu.
Katika upande wa mapato, mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi alisema kuwa halmashauri imekusanya zaidi ya asilimia 90 ya mapato yake ya ndani katika kipindi cha mwaka 20172018, ambao ni mwaka wa fedha ulioisha ijumaa wiki iliyopita.
Alisema kuwa halmashauri hiyo ilijewekea malengo ya kukusanya mapato ya ndani ya shilingi bilioni 3.8 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na kufanyikwa kukusnaya zaidi ya asilimia 90.
Mgina alifafanua kuwa asilimia kubwa ya mapato yake ya ndani yanategemea kutoka mazao ya misitu zikiwemo mbao na mirunda kwa zaidi ya asilimia 75 yanatokanayo na mazao mbalimbali ya misiti.
Alisema kuwa kumekuwepo na changamoto katika kukusanya mapato kutokana zikiwemo utoroshaji wa mbao kwa lengo kukwepa kulipa usharu kwa baadhi ya wafanyabiashara pamoja na kuwepo kwa miundombinu ya barabara sio rafiki.
Alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto ya utoroshaji wa mazao ya misitu halmashauri hiyo imefungua mageti mengi katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kudhibiti utoroshaji pamoja na kuimarisha doria za usiku na mchana kwa kushirikiana na wataalamu ya halmashauri hiyo.
Wakati huohuo, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, mkoani iringa imetumia zaidi ya shilingi milioni 39 katika utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira chini ya program ya maji vijijini (RWSSP) kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kupitia mapato yake ya ndani.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Ijumaa wiki iliyopita, John Bosco Quman kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wakati Kikao cha Baraza la Madiwani cha Mwaka alisema kuwa jumla ya visima vibovu vya maji 21 vilikarabatiwa kupitia program maji vijijini.
Alisema kuwa kuwa halmashauri hiyo imekarabati visima vya maji katika vijiji vya Ihanzutwa, Kihanga, Nzivi na Ibatu kupitia mpango wa payment by result (PbR) na kufafanua kuwa katika kijiji cha Kihanga visima nane (8) vilikarabitwa, Ihanzutwa visima vinne (4), Nzivi visima vitano (5) na Ibatu visima vinne (4) vilitengenezwa na vinatoa huduma.
Quman alisema alifafanua kuwa ukarabati wa visima vya maji 21 katika vijiji hivyo uligharimu jumla ya shilingi 13,650,000/- kupitia program ya maji vijijini (RWSSP) chini ya mpango wa payment by result.
Alisema kuwa miradi mimgine iliyotekelezwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 chini ya RWSSP ni pamoja na ukarabati wa mtego wa maji wa mradi wa Kijiji cha Ikimilinzowo uliogharami zaidi ya shilingi milioni 12, utekelezaji wa shughuli za kampeni ya usafi wa mazingira shilingi milioni 7.3 na usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maji shilinhi milioni sita (6) mtawaliwa (respectively).