Thursday, 27 October 2016

Clinton races ahead of Trump with up to 14-point lead in national poll days before election


Donald Trump and Hillary Clinton trade jokes and insults at charity event ITN


Democrat presidential nominee Hillary Clinton is leading her Republican rival by as many as 14 points in a national poll.

Clinton is topping the majority of recent national polls, with the latest numbers from a head-to-head race by USA Today/Suffolk released on Wednesday (26 October) showing her on 49 points to 39 for Trump.

And in the same poll by Reuters/Ipsos also released on Wednesday, Clinton was on 43 to Trump's 37, with a lead of six points, Real Clear Politics reported.

The polls also show Clinton leading Trump in a four-way race including Independent Gary Johnson and Green Jill Stein, with the Associated Press-GfK poll showing Clinton leading by 14 points on 51, Trump in 37, Johnson with 6 and Stein with 2.

Two other four-way polls have Clinton in the lead, with USA Today/Suffolk showing Clinton leading by nine points on 47, with Trump on 38, Johnson on 4 and Stein on 2, while the Reuters/Ipsos poll has Clinton leading by four points.


Hillary Clinton distributed cake to her staff and the press on board her her campaign plane as part of birthday celebrationsREUTERS/Carlos Barria


The Democrat nominee is also retaining her lead in nine out of 11 swing states, with Trump leading in just Iowa and Ohio – although the latter of these two is considered a key battleground in the election, often used as an indicator for how voting will play out nationally.

Trump is continuing to poll ahead of Clinton in the LA Times/USC Tracking survey, which has Clinton on 44 points and Trump on 45.

However, the methodology of the poll differs from other election surveys and as such has produced consistently different results, although in 2012 this was the poll that most closely predicted the results of the election.
Donald Trump's star on the Hollywood Walk of Fame is seen after it was vandalised in Los AngelesMario Anzuoni/ Reuters

The GOP nominee is seeing a slight uptick in the polls after several weeks of campaign scandals including the release of footage of Trump making lewd comments about women, and a number of women who have come forward to make abuse allegations against him.

WANANCHI KATA YA KITWIRU WAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UJENZI

Na Esta Malibiche

Iringa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Msenza amewataka viongozi wa Serikali za Mitaa kuwa waadilifu na kutojiingiza katika mauzo ya Ardhi ili kuepuka na Migogoro ya Ardhi.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na viongozi wa kata ya Kitwiru iliyopo Manispaa ya Iringa katika ziara yake aliyoifanya jana[leo]huku akiambatana na katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu,Watalaam wa Afya na Mazingira kutoka mkoani na Manispaa ya Iringa.

Masenza alisemakuwa lengo la ziara hiyo ni kutembelea na kukagua ujenzi holela katika Mtaa wa Kibwabwa’ B’,kukagua uchimbaji n a upondaji wa mawe unaofanywa na baadhi ya wananchi katika eneo la shule ya Msingi Mnazi mmojapamoja na Kukagua hali ya usafi wa Mazingira katika mtaa wa Kitwiru na Uyole .

"Ninatoa agizo kwa wale wote wanaoporomosha mawe na kujenga naomba wachukuliwe hatua za kinidhamu.Milimani,Mabondeni na katika vyanzo vya uhifadhi hairuhusiwi kujengwa,ninawaomba Manispaa iweke vibao vitakavyoonyesha maeneo yaliyohifadhiwa ili yasivamiwe na kuuzwa,"alisema Masenza.

Aliwasihi wananchi kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kupata vibari vya ujenzi na mara wanapotaka kununua uwajanja na kujenga nyumba ili kuepukana na Migogoro ya udanganyifu kutoka kwa viongozi wasio waaminifu.

"Wenyeviti wa mitaa tuendelee kutoruhusu wananchi wasitende makosa ya kujenga bila kufuata kanuni na taratibu za ujenzi ikiwa ni pamoja na kufuata michoro iliyopo," alisema Masenza

Awali kaimu Mkurungenzi wa Manispaa ya Iringa Omary Mkangama, akisoma Taarufa ya kuzuia ujenzi holela,Mikakati ya kulasimisha makazi,kuzuwia uvamizi katika maeneo ya milimani na uasafi wa Mazingira kwa mkuu wa mkoa wa Iringa, alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni miongoni mwa Halmashauri zinazokuwa kwa kasi kubwa hivyo kupelekea tatizo la ujenzi holela kukithiri katika maeneo yasiyopimwa na uvamizi katika maeneo ya mlimani.

Mkangama alisema hali hiyo inatokana na ongezeko la idadi ya watu,kutanuka kwa mji na ufinyu wa maeneo yaliyopimwa. Pia maeneo yaliyokithiri kwa ujenzi holela ndani ya Manispaa hiyo ni pamoja na Ipogolo, Mapogolo, Ndiuka, Semtema, Mtwivila, Mwangata, Mlandege, Igumbilo, Kihondombi, Isoka, Mafifi na milima ya Mkimbizi.

"Mikakati mbalimbali tumeiweka ili kuzuwia ujenzi holela na uvamizi wa maeneo yasiyopimwa ikiwa ni pamoja na kutumia makampuni ya wapima binafsi kupima viwanja kwenye maeneo yenye michoro ya mipango miji kwa gharama zilizotolewa na Serikali.

Alisema wanaendelea kutoa vibali vya ujenzi kwa haraka hasa kwenye maeneo yaliyopimwa ili kuepuka wananchi kujenga pasipo kufuata taratibu.Kuendelea kuuza viwanja vilivyopimwa kwa kuzingatia pato la mwananchi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Kitwiru Simba Nyunza akisoma Taarifa ya mikakati ya uboreshaji wa matumizi ya vyoo bora na Usafi wa mazingira kwa ujumla alisema kuwa majengo 2255 ndiyo yenye vyoo bora sawa na asilimia 93 ya majengo yote yaliyotambuliwa.

Nyunza alisema kuwa mikakati ya kata ni kuondoa na kuwezesha idadi ya majengo 168 yenye vyoo vinavyohitajika kuboreshwa viboreshwe mpaka kufikia mwisho wa mwezi Novemba mwa huu 2016.Na kwa wale watakaobainika kushindwa kutekeleza agizo hilo sheria ndogo ya Halmshauri itatumika.

"Baadhi ya wakzi wanashindwa kujenga vyoo bora kwa kuwa maeneo yao yana Ardhi oevu,hivyo wanashindwa kuchimba mashimo kwa kuwa maji chini ya Ardhi yapo jirani sana. Pia Ardhi iliyopo ni ya mchanga sana. Hivyo tunashirikisha wataalamu wa ziada kutoka ofisi ya Afya ya Manispaa kutoa Elimu ya Ujenzi wa vyoo bora katika maeneo oevu,"alisema Nyunza

Akielezea mikakati ya kutdhibiti ujenzi holela alisema ili kudhibiti ujenzi holela, kamati za mitaa ambazo ni kamati za mazingira ambazo ziliagizwa kufuatilia vibali vya ujenzi na kutoa maelezo ya namna ya kuomba vibari vya ujenzi kwa wajenzi wote kila mtaa ujenzi unapotokea.

A-FOUR-OLD CHILD RAPED TO DEATH


IRINGA: Iringa regional police are holding a witch doctor on suspicion of the murder of a four- year –old child (name withheld) Semtema Kihesa area in the municipality of Iringa, Iringa region.

The traditional healer known by the names of Peter Mtuka (44), a resident of Sumbawanga was arrested by police after body was found near his area where he do his job for interrogation.

Acting Iringa Police Commander, Assistant Commissioner of Police (ACP), John Kauga said the incident occurred at around 01:30 hrs after mid night on October 26 this year.

Telling a child's disappearance, acting commander said that on October 25 this year, child was playing with her friends in the neighborhoods at around 08:30hrs and 09:00hrs morning, when she disappeared in mysterious circumstances.

And then at 10:00hrs in the morning the mother of the child Monica Msani went to central police station delivery information about the disappearance of her child. 

Acting police commander said after the parents and neighbors continued to search for the child, they managed to find child in the dilapidated house at around as 7:30 but already dead nearby the traditional healer place where he conduct his healing activities..


Kauga further stated that after the body was found, they (parents and neighbors) reported matter to the police station and later on the body was pickup and took sent to Iringa Referral Hospital for postmortem.

According to the hospital report, indicated that child died from after rape, sodomized and squeezed her neck to death.

Moreover, Acting commander added that apart from getting entangled or choked tests also showed the child was raped and sodomized by unknown person or persons.

Police said they are holding a traditional healer in connection of death of the child because the body was found nearby the medicine-man’s place where he conduct his activities and link to superstition.



MTOTO WA MIAKA MINNE ABAKWA HADI KUFA


JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia mganga wa kienyeji kwa tuhuma ya mauaji ya mtoto wa miaka minne (jina limehifadhiwa) eneo la kihesa Semtema katika Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa.

Mganga huyo anayejulikana kwa majina ya Peter Mtuka (44) mkazi wa Sumbawanga alikamatwa na jeshi la polisi baada ya mwili wa marehmu kukutwa karibu na eneo lake lakufanyia shughuli za uganga kwa ajili ya mahojiano. 

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Iringa, Kamshina Msaisizi wa Polisi (ACP), John Kauga amedhitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 7:30 usiku Oktoba 26 mwaka huu. 

Akielezea kutoweka kwa mtoto huyo, Kaimu kamanda alisema kuwa Oktoba 25 mwaka huu akiwa nyumbani kwao majira saa 2:30 na 3:00 asubuhi alitoweka katika mazingira ya kutatanisha, na ndipo saa 4 asubuhi  wazazi wake walienda kuotoa taarifa polisi kuhusu kupotea kwa mtoto huyo katika kituo cha Polisi cha kati.


Alisema baada ya wazazi hao na majirani waliendelea kumtafuta mtoto huyo, ambapo ilipofika majira ya saa 7:30 usiku wa kuamkia Oktoba 26 walifanikiwa kumpata mtoto huyo katika moja ya pagale lililokuwa jirani na nyumba anayofanyia shughuli za kiuganga mganga huyo kienyeji akiwa amefariki dunia.


Kauga alisema baada ya kuupata mwili huo, walitoa taarifa katika kituo cha Polisi na mwili ulipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa kwa uchunguzi zaidi,na ndipo vipimo vya Daktari vilisema kuwa mtoto huyo alifariki dunia baada ya kukosa hewa baada ya kukabwa na mtu au watu wasijulikana.


Aidha Kaimu kamanda huyo aliongeza kuwa mbali na kukabwa lakini pia vipimo vilionyesha mtoto huyo alibakwa na kulawitiwa na mtu au watu wasiojulikana.


Polisi walisema wanamshikilia mganga wa kienyeji kutokana na mwili wa mtoto kukutwa karibu na analofanyia shughuli za zake za uganga na kuhusianisha na tukio hilo na masuala ya ushirikina.

Naye Monica Msani ambaye ni mama wa mtoto huyo alisema kuwa anauchungu mkubwa sana kwani mtoto wake kwa mara ya mwisho alimuona akiwa anacheza na wenzie nje ya nyumba yao na ndipo alipotoka kwenda kumuangalia ili aende kunywa chai ndipo walipomkuta hayupo na wenzake kutoaelewa alielekea wapi.



RPC KINONDONI ATOA TAHADHARI KWA WAMILIKI WA MAGARI JIJINI DAR ES SALAAM



RPC Suzan Kaganda 


Na Dotto Mwaibale


WAMILIKI wa magari wametakiwa kuchukua tahadhari ya kuzima na kufunga milango magari yao pale wanaposimama kwa dharura kupata mahitaji mbalimbali ili kuyanusuru kuibwa.


Mwito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Suzan Kaganda wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu tukio la kuibwa kwa gari la Kapteni Innocent Dallu maeneo ya Mbezi Juu huku akiwemo mtoto wake Lightness.


"Napenda kutumia fursa hii kuwaomba wamiliki wa vyombo vya moto kuchukua tahadhari ya kuzima magari yao na kufunga milango wanaposimama maeneo yoyote kupata mahitaji yao kwani si rahisi kumbaini mhalifu kwani wapo kila sehemu" alisema Kaganda.


Alisema katika tukio la kuibwa kwa gari la kampteni Dallu alikuwa amesimama maeneo ya Mbezi Juu bila ya kulizima akinunua mahitaji ambapo walitokea vijana wakaondoka na gari hilo aina ya Toyota Harrier baada ya kumtelemsha mmoja wa watoto aliyekuwemo ndani ya gari hilo aitwaye Philip huku wakiondoka na mdogo wake Lightness.


Alisema watuhumiwa hao walimtelekeza mtoto huyo maeneo ya Golden Bridge katika baa moja na kisha kuondoka na gari hilo ambalo lilipatikana baada kukamatwa na polisi Kiwangwa mkoani Pwani ambapo kijana mmoja Ezekiel Daud anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.


Alisema ni vizuri wamiliki wa magari kuzingatia jambo hilo ili kuepusha matukio kama hayo ambayo yanapoteza muda mwingi wa kuyatafuta kwani tukio kama hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kinondoni ambapo wahalifu waliweza kuiba gari aina ya Noah lililosimamishwa bila ya kuzimwa na kuondoka nalo na alijapatikana mpaka leo hii.

MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE



TANZANIA
UK

Bayport yajivunia miaka 10 ya kutoa huduma ya mikopo nafuu ya kifedha Tanzania




Dar es Salaam – Taasisi inayoongoza Tanzania kwa kubobea katika kutoa mikopo nafuu, Bayport Financial Services katika kipindi cha miaka 10 iliyopita imechangia kwa kiwango kikubwa katika kuboresha maisha ya maelfu ya Watanzania kupitia utoaji wa mikopo.


Bayport Tanzania ni miongoni mwa taasisi tanzu kumi za Taasisi ya Bayport Group ambayo hutoa ufumbuzi wa kifedha kwa watu binafsi walioko katika ajira rasmi au waliojiajiri ndani ya soko linaloibukia. Huduma zinazotolewa na taasisi hiyo zinaboresha ujumuishwaji kifedha kwa watu ambao hawana uwezo wa kuzifikia huduma za kawaida za kibenki au walio na kiasi kidogo cha fedha katika benki. 


Baada ya kuanza shughuli zake nchini Zambia mwaka 2001, shughuli za Bayport kwa hivi sasa zinaendeshwa katika nchi saba barani Afrika na nchi mbili ndani ya Amerika Kusini. Nchi hizo ni Zambia, Uganda, Ghana, Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Msumbiji, Colombia, na Mexico.


Hivi sasa Bayport imekuwa ni msingi wa kuaminiwa na mteja ikiwa na takribani wateja 518,000 ambao kila mara wamekuwa wakipata na hata na kufurahia huduma inazozitoa. 


Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga, Bayport imeshatoa zaidi ya shilingi bilioni 48 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015 peke yake. Kwa upande mwingine Bayport inachukuliwa kuwa ni ‘mlipa kodi mkubwa’ nchini Tanzania ikiwa imelipa zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa mwaka wa fedha 2014.


“Matamanio yetu ni kuboresha maisha ya wateja wetu na kuwapa fursa ambazo zitawanufaisha sio wao peke yao bali pia watoto wao na kizazi kijacho,” alisema Mbaga katika mazungumzo yake na wanandishi wa habari hivi karibuni. 


Aliongeza, “Tunawasaidia kwa kuangalia unafuu utakaotokana na mtiririko wa fedha katika kipindi kifupi ambapo matokeo yake husaidia familia katika kuongeza na kuwa na ustawi wa kifedha wa kudumu.”


Bayport Tanzania ilianzishwa mwaka 2006, na kwa haraka imekuwa ni mtoaji wa mikopo kwa wafanyakazi katika sekta za umma na binafsi. Kuwepo kwa ofisi zake 83 za kudumu na matawi 45 ya muda kumeifanya kufika kila mkoa kwa Tanzania Bara.


Kampuni hii ina wafanyakazi wa kudumu 300 na mtandao wa mawakala wa mauzo zaidi ya 1000.


“Kazi ambazo tumekuwa tunazitoa zimechangia kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana hapa nchini,” anasema Mbaga. 


Kwa mujibu wa utafiti wa Ujumuishaji wa Nguvu Kazi (Integrated Labour Force Survey 2014), kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Tanzania kilikuwa ni asilimia 13.7.


Mbali na kutoa mikopo, mambo mengine ambayo Bayport inajishughulisha nayo ni pamoja na bidhaa za bima kama vile Sera ya Ulinzi Kielimu ambayo inashughulikia utegemezi wa ada katika elimu kwa muda wa hadi miaka mitatu katika iwapo kwa bahati mbaya mwenye bima hiyo atafariki. Sera ya Bima ya Maisha ya Bayport inahusisha kulipia salio lililobakia iwapo wateja watapunguzwa kazi, watakuwa wamepata ulemavu, watafariki au kupatwa na maradhi kama vile saratani. 


Hivi karibuni Bayport ilizindua aina ya mikopo kwa ajili ya nyumba ambayo inawawezesha wateja kumiliki kiwanja kilichopimwa. Bidhaa hiyo inawezesha Bayport kuifikisha mikopo yake kwa mkopaji kwa kutumia kiwanja kilichopimwa kama dhamana.


Akizungumza kuhusu sera ya Bayport kuhusu kuwajibika kwa huduma za kijamii, Mbaga alisema kwamba elimu ndio kipaumbele chake. “Kupitia mkakati wa ‘Badilisha Maisha’ tumeshafanya ukarabati wa madarasa katika shule kadhaa, kutoa msaada wa madawati, kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na kutoa msaada wa vitabu. Tangu mwaka 2006, tumetoa misaada ya moja kwa moja kwa wanafunzi 1,500 wa shule za msingi na sekondari.” 


Bayport pia inawasaidia watoto yatima. Mradi wa mfano unajidhihirisha kwa kuisaidia shule ya watoto yatima inayodhaminiwa na Mfuko wa Fursa kwa Wote (EOTF) ambapo Bayport imeboresha shule hyo ya awali kuwa katika viwango vya kisiasa.


Uwekezaji wa shilingi milioni 200 uliofanywa na Bayport umewezesha kuwepo kwa mazingira rafiki ukiwepo mwanga wa asili na sehemu asilia za kupitisha hewa kwa ajili ya watoto 40 wanaohudumiwa akatika kituo cha EOTF na wengine 60 kutoka katika vijiji jirani wakinufaika.


Akiangazia kuhusu safari ya miaka kumi ya mafanikio katika biashara hapa nchini, Mbaga anasema kwamba Kampuni hiyo inajivunia kukua kwake na kukomaa ambako imeweza kufikia katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita. “Tunasherehekea fursa hii na uwezo wa kuleta mabadiliko katika maisha ya wateja wetu, wadau, wafanyakazi na jumuia katika maeneo tunakoendesha shughuli zetu.”


Alidokeza kuwa dira ya kimkakati ya taasisi hiyo na utekelezaji wake uliokwishafanyika umejikuta ukipata msaada kutoka kwa wawekezaji, miongoni mwao ni kampuni ya uwekezaji wa Sweden ya AB Kinnevik. Julai 2010 kampuni hiyo iliwekeza dola milioni 40 katika Bayport Group na hivyo kuwa taasisi pekee yenye hisa nyingi ndani ya Bayport. 


Miezi minne baadaye Bayport ilitoa kwa mara ya kwanza katika masoko ya madeni ya mitaji kimataifa kwa kukusanya jumla ya dola milioni 100.

“Mwaka 2016 uongozi wa Bayport uilifikia dola milioni 250 ikiwa ni uwezo wa salio kubwa kupatikana kutoka Shirika la Uwekezaji Binafsi Ng’ambo (Overseas Private Investment Corporation-OPIC), ambayo ni taasisi ya maendeleo ya fedha ya serikali ya Marekani. Mkopo huo wa muda mrefu utasaidia ujumuishwaji wa kifedha wa taasisi na ajenda yake ya kukua katika shughuli zake zote. Kama taasisi tanzu ya Bayport, Bayport Tanzania inachangia katika historia ya uwekezaji wa taasisi na faida zinazotoka ndani yake.”


Kwa mujibu wa Mbaga mkakati wa kibiashara wa Bayport upo katika mabadiliko ya bidhaa na ubunifu wa kiteknolojia na ‘watu wakiwa ndio nguzo yetu kuu’.


Ndani ya mkakati huo wa taasisi, Bayport Tanzania mwaka 2015 utambulisho wake ulipata chapa mpya ikiwa na ujumbe uliojikita kwa watu, na hivyo kuipa taasisi fursa ya ya kujiweka tena yenyewe katika mtoaji wa ufumbuzi wa kifedha.


“Bidhaa yetu mpya haikuanzishwa katika hali ya upweke. Iliibuka ndani ya falsafa yetu ya kibiashara ambayo inaitwa ‘The Bayport Way”, Mbaga alifafanua na kuongeza, “Falsafa hiyo inahusu mambo yote ya namna tunamchukulia mteja, awe ni mwajiriwa, mteja au mwekezaji, na jinsi ambavyo tunaongeza thamani katika maisha yao.”


Kama taasisi Bayport inaamini kwamba mikopo ni nyenzo yenye nguvu inapotumiwa kistaarabu na katika mazingira yaliyo na ufanisi. “Hakuna kinachotufanya kama pale ambapo tunapowaona wateja wetu wakiitumia mikopo katika matumizi chanya na kuendesha shughuli za kiuchumi ambazo kimsingi zinaboresha maisha yao,” Mbaga alisema.


Ofisa Mtendaji Mkuu huyo aliwashukuru wateja wa Bayport Tanzania, wafadhili, serikali na wadau wengine kwa kuiunga mkono taasisi hiyo bila kuchoka katika kipindi chote cha miaka kumi.

Alisema, “Imekuwa ni safari ya kuvutia iliyojaa mafanikio. Bila wadau wetu hawa hatungaweza kufikia hatua hiii. Nawahakikishia kwamba Bayport Tanzania inaimarika kila mwaka. Wakati tunaelekea katika mwongo mwingine tumejipanga na tumejikita katika kufanikiwa hata katika viwango vya hali ya juu vya ufanisi katika kutoa kutoa bidhaa zisizo na ushindani nchini Tanzania.” 


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...