Sunday, 30 August 2015

LOWASSA KUTIMUA VUMBI IRINGA KAMPENI YA URAIS LEO

MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa anatarajia kutimua vumbi katika jimbo la Iringa Mjini leo. 

Lowassa anayewania nafasi hiyo kupitia vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), atawasili mkoani Iringa siku moja tu baada ya umoja huo kufanya uzinduzi wa kampeni zake jijijini Dar es Salaam jana.


UKAWA wamezindua rasmi kampeni zao Agosti 29, katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam baada ya kuruhusiwa kuutumia uwanja huo ambao awali ulielezwa kutaka kutumiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa shughuli nyingine.

KESI YA TALAKA YA MMILIKI WA ST. MATHEW YAAHIRISHWA TENA



Na Mwandishi wetu

MAHAKAMA ya Mwanzo Kizuiani Mbagala, Dar es Salaam, imepanga Septemba Mosi mwaka huu kutoa hukumu katika kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali zenye thamani ya Sh Milioni 800 inayomkabili Mmiliki wa Shule ya Sekondari ya St. Mathew na St. Marks, Thadei Mtembei.

Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa juzi lakini iliahirishwa kutokana na upande wa mlalamikaji kutofika mahakamani.

CHADEMA YAZINDUA KAMPENI JIMBO LA KALENGA






Na Mathias Canal, Iringa 
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa katiba ya Wananchi {UKAWA} kimezindua kampeni zake katika Jimbo la Kalenga lililopo mkoani Iringa kwa muktadha wa kuanza vyema mikikimikiki ya kumnadi mgombea wake ambaye mara kadhaa amesikika akisema jimbo hilo limekosa muwakilishi wa wananchi bungeni. 

Chadema/ukawa inataraji kuanza kampeni zake za kumnadi mgombea wa Urais, wagombea ubunge, na udiwani mara baada ya uzinduzi wa kampeni zinazotaraji kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo zilizofanyika katika eneo la Ifunda, mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema/Ukawa, Mdede Mussa Leonard amesema kuwa ameamua kugombea jimbo hilo kwa kuwa ni mkazi wa Kalenga hivyo hakusoma kwenye kitabu changamoto za jimbo na wala hana haja ya kusimuliwa.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...