Mwenyekiti wa Umoja wafanyabiashara Manispaa ya Songea (UWABIMASO) Karim Ismail Matumca akifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano wa wadau wa habari ulioendeshwa na Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma (RPC) kwa ufadhili ya Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC),uliyofanyika Ukumbi wa Majengo SACCOS Mitumbani Songea mijini.
Saturday, 14 September 2013
MKUTANO WA WADAU WA HABARI SONGEA
(L-R) Mohamed Mchele mdau, M/kiti - UWABIMASO Karim Ismail na Shekhe Abdullah Hamidu (Kitete) ambaye in shekhe wa Wilaya ya Songea mjini wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano wa
wadau wa habari ulioendeshwa na Chama cha waandishi wa habari mkoa wa
Ruvuma (RPC) kwa ufadhili ya Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari
nchini (UTPC),uliyofanyika Ukumbi wa Majengo SACCOS Mitumbani Songea
mijini.
JKT MLALE YAIBAMIZA MAJIMAJI FC MAGOLI 2-0
Mwenyekiti wa Timu ya Majimaji Hamphrey Milanzi (kushoto)
na Kocha ya timu hiyo Peter Mhina wakifuatilia mchezo kwa umakini
kati ya timu yao na JKT Mlale uliofanyika katika Uwanja wa Majimaji
mjini Songea, mkoani Ruvuma leo, ambapo JKT Mlale ilishinda magoli 2-0.
(Picha
na Friday Simbaya)
JKT MLALE imeiadhibu timu ya Majimaji ya Songea mjini bila huruma kwa kuibamiza magoli 2-0 katika michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu msimu huu, iliyoanza kutimua vumbi Septemba 14, mwaka huu.
Mechi ya ufunguzi ya timu hizo mbili zilifanyika katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma, huku wenyeji Majimaji FC wamechapwa magoli 2-0 na timu ya JKT Mlale.
Aidha, JKT Mlale ilipata goli la kwanza kupitia mshambuliaji wake Edward Songo mnamo dakika 19 katika kipindi cha kwanza na goli la pili lilifungwa na Ally Bilali dakika ya 21.
Kila timu itakayoongoza kundi lake katika ligi itakayochezwa kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini) ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2014/2015.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mechi za ufunguzi kwa kundi A zitakuwa kati ya Tessema dhidi ya Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam) wakati Septemba 15, mwaka huu ni Transit Camp itakayocheza na Polisi Dar (Uwanja wa Mabatini, Pwani).
Mechi nyingine siku hiyo ni Ndanda itakayoivaa Friends Rangers (Uwanja wa Nangwanda, Mtwara) wakati Villa Squad itaikabili African Lyon itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B ni Burkina Faso itacheza na Polisi Moro (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Mkamba Rangers itaivaa Lipuli (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro), Majimaji itakuwa mwenyeji wa Mlale JKT (Uwanja wa Majimaji) wakati Septemba 15, Kimondo SC itacheza na Kurugenzi (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).
Mechi za ufunguzi kundi C ni Polisi Mara dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja wa Karume, Musoma), Kanembwa JKT itacheza na Polisi Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma), Stand United itaivaa Mwadui (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), na Pamba dhidi ya wenzao Toto Africans (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).
Taarifa ya TFF ilisema kuwa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 26, mwaka huu wakati wa pili utamalizika Machi 22, mwakani.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...