Sunday, 26 March 2017

MAGAZETI YA LEO JUMATATU


































MANISPAA YA IRINGA YATOA MKOPO WA 70M/- KWA WANAWAKE NA VIJANA










HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa imetoa mkopo kwa vikundi 35 vya wanawake na vijana ikiwa ni utekeleza wa agizo la serikali la kutenga asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi hivyo jana.

Akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 70,000,000/- kwa vikundi hivyo katika awamu ya pili ya kipindi cha mwaka 2016/2017, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Alex Kimbe amewataka kinamama na vijana kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizokusudiwa ili ziweze kuleta manufaa na kuwatoa katika lindi la umasikini.

Alisema kuwa jumla ya vikundi 35 toka katika kata zote 18 za Manispaa ya Iringa vimepokea mikopo, ambapo vikundi 16 vya vijana vimepokea jumla ya shilingi milioni 32,000,000/- na shilingi milioni 38,000,000/- zimetolewa kwa vikundi 19 vya wanawake.

Kimbe alisema mkopo huo umetolewa kwa awamu ya pili, ambapo kwa awamu ya kwanza kipindi cha mwaka 2016/2017 Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ilitoa kiasi cha shilingi milioni 70,147,000/- kutoka mapato ya ndani kwa vikundi 35 vya wanawake na vijana.

Aidha, jumla ya 647,000/- zilitumika kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi wa vikundi vilivyokopeshwa, ambapo vikundi 18 vya vijana na vikundi 17 vya wanawake vilinufaika.

Naye Kaimu Ofisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Iringa, Eliah Kasanga alisema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na watendaji wa kata wameendelea kufanya ufautiaji kwa vikundi vilivyokopeshwa, na mpaka Januari, 2017 jumla ya 39,788,000/- zimerejeshwa na ufualiaji unaendelea.

Alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imekuwa ikitekeleza agizo la serikali la kutenga asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana.

Kasanga aliongeza kuwa agizo hilo lilianza kutekelezwa kuanzia mwaka 2012 kwa kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake tu na kufikia mwaka 2013 mikopo hiyo ilianza kutolewa kwa vikundi vya vijana pia.

Alisema kuanzia mwaka 2012/2013 mpaka 2016/2017 kiasi cha shilingi 175,100,000/- zimenufaisha walengwa 1,243 wa vikundi vya wanawake na vijana.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mikopo ya Vijana Manispaa ya Iringa, Maria Sangana alisema mfuko huo umekuwa ukikabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na vikundi kutorejesha fedha walizokopeshwa kwa wakati.

Alisema kuwa hali hii imekuwa ikichelewesha utoaji wa mikopo kwa vikundi vingine na kuongeza kuwa baadhi ya vikundi kutotumia fedha kwa shughuli walizopanga wakati wa kuomba mkopo.

Pia, Sangana alisema kuwa baadhi ya vikundi vinakabiliwa na mikopo mengine mingi toka taasisi zingine za fedha na kuongeza kuwa kuna upotoshaji unaendelea mitaani kuwa fedha inayotolewa na serikali ni msaada.


Aidha, katika kukabiliana na changamoto hizo ofisi ya maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeeandaa mfumo wa ufuatilaji wa marejesho ya fedha za mfuko huo, pamoja na kuendelea kutoa elimu ya stadi za kazi na ujasiliamali kwa kivundi vya ujasiliamali.

ZAIDI YA 80 IRINGA WAPATA MAFUNZO YA UKARIMU NA UTALII


Mwenyekiti wa vikundi vya asili vya ngoma kutoka Ikwavila New Force katika Kijiji cha Mahuninga, tarafa ya Idodi wilayani Iringa, mkoani Iringa, Recktika Palinoo (wa mbele kulia) pamoja na katibu wake Leonatus Kikoti wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya ukarimu na utalii yaliyofanyika mkoani Iringa jana.  (Picha na Friday Simbaya)


MKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka watoa huduma katika sekta ya ukarimu na utalii kanda ya kusini kuboresha huduma zao ili kukidhi haja soko la utalii katika ukanda huu.

Alisema kuwa ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi za taifa za kusini watoa huduma kwa kushirikiana na sekta binafsi hawanabudi kuinua viwango vya utowaji wa huduma.

Masenza alisema hayo wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watoa huduma katika sekta ya ukarimu na utalii yaliyofanyika mkoani Iringa jana.

Alisema kuwa serikali ipo katika machakato wa kuboresha miundombinu za barabara na viwanja vya ndege ili kurahisha watalii kufika katika hifadhi pamoja na vivutio vilivyopo katka ukanda wa kusini.

Alisema kuwa takwimu za mwaka 2015 zinaonesha kuwa watalii wengi zaidi walitembelea mbuga za kanda za kaskazini kuliko kanda ya kusini, kwa hiyo mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuboresha utoaji wa huduma katika kanda ya kusini.

Zaidi wa washiriki wa 80 wamepata mafunzo ya ukarimu na utalii yaliaanza tarehe 22 hadi 24 Machi mwaka huu, yaliyotolewa na Chuo cha kitaifa cha utalii kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na SPANEST kwa ufadhili shirika la umoja wa mataifa la maendeleo (UNDP).

Alisema mafunzo hayo wamewaongezia ujuzi pamoja na kujiamini wakati wa kutoa huduma kwa watalii wanaotembelea ya kanda ya kusini.

Aidha, Masenza alisema Wizara ya Maliasili na Utalii ipo katika mchakato wa kutunga kanuni zitakazowazuia wafanyakazi wa hoteli wasio na vyeti vinavyotambulika na serikali kutoa huduma katika sekta ya utalii.

Alisema kuwa kanuni hiyo ambayo msingi wake unalenga kuendeleza na kuboresha huduma katika ya sekta hiyo, utahusisha pia kuvibana vyuo vya hoteli na utalii ili vitoe mafunzo yanayokidhi viwango.

“Baada ya kutungwa na kuanza kutumika kwa kanuni hizo, waajiri katika sekta hiyo watalazimika kuwaajiri wafanyakazi wenye sifa ambao wamesajiliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii,” alisema Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, alisema Masenza.

Aliyasema hayo jana kwenye mafunzo ya siku tatu ya ukarimu na utalii yanayoshirikisha watoa huduma zaidi ya 80 wanaofanya biashara inayohudumia watalii mkoani Iringa.

Mafunzo hayo yanayotolewa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Mradi wa Kuboresha Mtandao wa Maeneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST), yanafanyika kwa siku tatu mjini Iringa.

Masenza alisema mafunzo hayo ya muda mfupi yameanza kutolewa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini baada ya serikali kubaini baadhi ya vyuo vinavyotoa mafunzo hayo kuyatoa chini ya viwango.

Mratibu wa SPANEST, Godwell Ole Meing’ataki alisema changamoto hizo zimesababisha huduma duni katika maeneo ya mapokezi, chakula, vinywaji na malazi, na hivyo kuleta malalamiko makubwa sana kwa wageni.





Kwa kupitia mafunzo hayo mafupi Meing’ataki alisema; “ni mtarajio yetu maarifa watakayopata washiriki hawa yatawawezesha kutambua wajibu wao ili wageni wanaopata wapate huduma wanazotarajia.”

“Sekta ya utalii ina changamoto nyingi, lakini eneo hili la huduma ni muhimu kwasababu linaweza kusaidia kumrudisha mgeni tena na tena na kumfanya awe balozi kwa watu wengine,” alisema.

Kwa wawekezaji katika sekta hiyo, haitoshi tu kuwa na hoteli kubwa kama itakuwa haina huduma bora kwa wageni wake.

Awali, akifungua mafunzo hayo tarehe 22 Machi, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Fikira Kissimba alisema licha ya ukanda wa nyanda za juu kusini kuwa na vivutio vingi vya utalii, idadi ya watalii wanaovitembelea ni ndogo na moja ya sababu yake ni uduni wa huduma katika sekta hiyo ya utalii.


Akishukuru wizara ya maliasili na utalii na SPANEST kwa kutoa mafunzo hayo, Kissimba alisema yatakuwa chachu katika kukuza na kuendeleza utalii kusini mwa Tanzania kwa kutoa huduma bora kwa watalii.

Aliwataka wahudumu katika sekta hiyo waache tabia ya uvivu, kufanyakazi kwa mazoea na wawe wepesi kujifunza ili kuboresha huduma zao.



MANISPAA YA IRINGA YAAGIZWA KUSIMAMIA MIRADI KWA ZINGATIA VIWANGO VYA UBORA




Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)imeiagiza Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa kuboresha barabara zake za pembezoni mwa mji ili zitoe huduma kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa majumwisho wa ziara ya siku moja ya kamati kwenye Manispaa ya Iringa jana makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Abdallah Chikota alitoa maelekezo kuboresha miundombinu ya barabara pembezoni mwa mji.

Alisema kuwa Manispaa ya Iringa imeelekeza nguvu kubwa katikati ya mji na kusahau barabara za pembezo ambazo zitasaidai kutoa huduma kwa wananchi.

Chikota alisema kuwa wananchi walioko pembezoni mwa mji ni sawa na wananchi wa katikati ya mji.

Kuna tofauti kubwa kati ya wananchi waishio pembezoni na katikakti. Barabara za pembezoni mwa mji hazina kiwamgo vya ubora…,” alisema Chikota.

Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge za Hesabu za Serikali za Mitaa ilitembelea barabara za Mkimbizi- kihesa Sokoni-Tumaini Univesrsity and Ngome na kukuta havian vivuko kwa kurahisha wananchi kufika kwa krahisa katika makazi yao.

Alisema kuwa barabara hizo pamoja na kukamilika ujenzi wake zilikuwa hazina baadhi ya alama za barabarani na vivuko vya watembelea kwa miguu. 

Hatua hiyo imetokana na ujenzi wa barabara wa hizo kutokuwa na baadhi ya miundombinu vikiwemo vivuko vya kufanya barabara hiyo kutokuwa rafiki kwa mwananchi.

Mradi wa ujenzi wa barabara unajumuisha vipande vitatu vya barabara za Mkimbizi TBA (1.10km), Kihesa Sokoni-University of Iringa (zamani Tumaini University (0.70km) na Ngome–Mwang’ingo (0.45km) uliyobuniwa ili kuinua kiwango cha barabara hizi kutoka changarawe hadi kiwango cha lami.

Halmashauri ya Manispaa ilifanya matengenezo ya barabara hizi kwa kiwango cha lami kwa kutumia fedha za mfuko wa barabara (Road Fund) kwa bajeti ya mwaka 2013/2014 ambazo zilivuka mwaka.

Akitoa taarifa kwa kamati Mhandishi wa Ujenzi wa Manispaa ya Iringa, Mashaka Luhamba alisema kuwa mradi huo ulianza kutekeleza tarehe 1/11/2013 na uilikamilika tarehe 18/09/2014.

Alisema kuwa kazi hiyo ilitekelezwa na Mkandarasi G’S Contractors kwa mkataba wa gharama ya 1,088,505,000/-.

Luhamba alisema kuwa kazi hiyo ililenga na pia kupunguza kero kwa wananchi wa eneo la mkimbizi ambalo halina barabara ya uhakika na lina wakazi wengi.

Naye, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alisema amepokea maagizo hayo kutoka kamati ya kudumu ya bunge za hesabu za serikali za mitaa (LAAC)na kuahidi kuyafanya kazi mapendekezo hayo.

Wamoja alisema kuwa kupitia sekritarieti ya mkoa atahakikisha wanasimia utekelekezaji wa maagizo kwa manispaa ya iringa yanafanyika.

Kamati ya kudumu ya bunge za hesabu za serikali za mitaa (LAAC) ilitembelea miradi mbalimbali hapa manispaa ya iringa ikiwemoile ya maji, barabara na machinjio ya kisasa ambao hata hiyo mradi huo umechukua muda mrefu kukamilika (miaka kumi).

Pia kaamti hiyo imeagiza watendaji wa Manispaa ya Iringa kusimamia miradi hiyo inayotumia gharama za walipa kodi kwa kuzingatia viwango wa ubora.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...