HATIMAYE wafanyabiashara ambao vibanda vyao katika soko kuu la Manispaa ya Songea vilifungiwa na serikali Februari 11 mwaka huu kwa kushindwa kutimiza masharti yaliowekwa na Manispaa, wamekubaliana na masharti yaliowekwa na Manispaa hiyo ikiwemo kusaini mikataba na kufanya malipo.
Uongozi wa wafanyabiashara wa Mkoa wa Ruvuma,wakizungumza na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Abdul Hassan Mshaweji, ofisini kwake kwa niaba ya Uongozi wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Masoko Songea (UWABIMASO ) ,wamesema wamekubali kumaliza changamoto iliyojitokeza na kuahidi kutoa ushirikiano kati ya Manispaa na wafanyabiashara wa soko kwa masharti yaliowekwa na Manispaa.
Tayari vibanda vingi vimefunguliwa baada ya wafanyabiashara kusaini mikataba na kulipa.