Sunday, 19 July 2015

CCM WILAYA YA IRINGA MJINI YAANZA KUWATAMBULISHA WAGOMBEA UBUNGE KWA WANACHAMA


Katibu wa Wilaya ya Iringa mjini, Elisha Mwampashi (kulia) akiongea na waandishi wa habari jioni leo na kushoto ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Iringa mjini Abeid Kiponza.



Zoezi la awali la utoaji na urejeshaji wa fomu kwa wagombea nafasi za ubunge na madiwani kupitia Chama cha Mapidunzi (CCM) nchi nzima umekamilika jana.

Katika Jimbo la Iringa mjini, mkoani Iringa chama hicho kimeandaa mikutano kwa wagombea ubunge wote ya kuwatambulisha kwa wanachama ikiwa sehemu ya pili ya mchakato ya kumpata mgombea pekee atakaye peperusha bendera ya chama hicho kwa kushindana na vyama vya upinzani katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana usiku, Katibu wa Wilaya ya Iringa mjini, Elisha Mwampashi alisema awamu ya kwanza ya kutoa na kurudisha fomu za ubunge limealianza tarehe 15.07.2015 na kumalizika hadi 19.07.2015.

Aliongeza kuwa awamu ya pili ya mchakato itaanza tarehe 20.07.2015 hadi 31.07.2015 lengo ni kuwatambulisha watia nia kwa wanachama katika matawi ambapo utaratibu ni kwamba watapanda gari moja wagombea wote 13 na kila mmoja atapewa nafasi ya kujieleza wakati wa mikutano katika kata zote 18 za Jimbo la Iringa mjini.

Alisema kuwa jumla ya wagombea ubunge 13 Iringa mjini waliochua na kurudisha fomu na wataanza safari hiyo ya kuwatambulisha kwa wanachama katika matawi 81 ya CCM.

Wana CCM hao wanaoomba nafasi ya ubunge ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu, Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Frederick Mwakalebala na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mahamudu Madenge.

Katika orodha hiyo yupo pia Dk Yahaya Msigwa, Nuru Hepautwa, Addo November Mwasongwe, Adestino Mwilinge, Frank Kibiki, Aidani Kiponda, Peter Mwanilwa, Fales Kibasa, Michael Mlowe na Balozi mstaafu Dk. Augustine Mahiga.

Kwa mwaka wa tano sasa, jimbo hilo linaongozwa na Mch. Peter Msigwa (Chadema) aliyeshinda kwa tofauti ya kura 828 katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 baada ya kujipatia kura 17,744 dhidi ya kura 16,916 alizopata mgombea wa CCM, Monica Mbega.

MCHUNGAJI MSIGWA APATA MAPOKEZI MAKUBWA IRINGA..!

Sehemu ya umati wa wakazi wa Iringa mjini wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa leo. (Picha na Friday Simbaya)


Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu wakihutubia wa wakazi wa Iringa mjini katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa katika Jimbo la Iringa mjini leo. (Picha na Friday Simbaya)

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...