Tuesday, 22 November 2016

CCM ZANZIBAR YAONYANA KUHUSU UMBEA KWENYE MITANDAO YA JAMII




Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wametakiwa kuacha tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kujadili masuala yanayohusu Chama badala yake watumie vikao halali vinavyotambuliwa na Katiba ya Chama hicho.


Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakati akifunga Mkutano wa Viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja Kichama uliofanyika katika Shule ya Msingi Makunduchi Mkoani humo.


Alifafanua kwamba tabia hiyo ya kujadili, kukosoa na kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa ngazi mbali mbali wa Chama na Jumuiya zake kupitia Mitandao ya kijamii ni utaratibu unaokwenda kinyume na miongozo ya chama hicho.



Alisema Katiba ya CCM inaelekeza Kwamba mambo yote yanayogusa maslahi mapana ya Chama yajadiliwe Katika Vikao halali vinavyotambuliwa na kanuni za Chama, kwani jukwaa hilo ndiyo sehemu rasmi ya kukosoana na kupeana maelekezo.


Vuai alisikitishwa na tabia hiyo na kueleza kuwa njia pekee ya kumaliza Changamoto hiyo ni Wanachama na Viongozi kujenga utamaduni wa Kusoma na kuelewa Kanuni, Katiba na miongozo mbali mbali ya CCM ili kufahamu wajibu, majukumu, haki na maadili yanayoongoza Chama.


Alisema tabia hiyo imekuwa ikifanyika katika Magroup ya Mitandao ya kijamii zikiwemo Facebook, WhatsApp na mitandao mingine, jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa kanuni za Chama.


“ Wanachama, Viongozi na Watendaji naomba muelewe kwamba hiki Chama kinaendeshwa kwa utaratibu maalum ulioelezwa Kikatiba , Kikanuni na miongozo mbali mbali, kwa nia ya kulinda hadhi na heshima ya Chama chetu, na hakuna jambo lolote linaloshindikana kupatiwa ufumbuzi kupitia utaratibu huo.


"Sasa panapojitokeza baadhi ya Watu miongozi mwetu wakaanza kujadili na kuwakosoa wenzao nje ya mfumo huo basi hao tunawahesabu kuwa wana nia ya kuanzisha Majungu, Fitna na mpasuko katika taasisi yetu.”, alieleza Vuai na Kuongeza kuwa CCM ni Chama imara na kinachoheshimu Demokrasia katika kujadili mambo yake na kuyatolea maamuzi stahiki katika Vikao rasmi na sio vichochoroni au vibarazani.


Aliongeza kuwa sio kwamba kuna viongozi na wanachama wanaogopa ama hawataki kukosolewa lakini lazima heshima na nidhamu iwepo katika kutekeleza matakwa ya Demokrasia ndani ya Chama hicho kwa kuheshimu utaratibu uliowekwa Kikatiba.


Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya mwaka 2015/ 2020 katika Mkoa huo aliwapongeza Viongozi wa Majimbo wakiwemo wabunge, wawakilishi na Madiwani huku akiwasisitiza Viongozi wa Chama kuhakikisha wanakagua kikamilifu miradi inayotekelezwa na viongozi hao ili kujiridhisha kama inawanufaisha wananchi wote.


Aliwataka viongozi wa Chama na Jumuiya zake kuwa wa kwanza kutambua kero na changamoto za wananchi wa maeneo mbali mbali na waziwasilishe kwa Wakuu wa Wilaya (DC) ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu na Serikali.


“ Huu sio wakati wa kusubiri taarifa zinazohusu Changamoto za Chama, Jumuiya na Serikali ziletwe Ofisini, badala yake mtoke na kuzitafuta wenyewe ili kuwasaidia wanachama na wananchi kutatuliwa kero zao kwa haraka kupitia Mamlaka husika.”, alisisitiza Vuai.


Alisema Viongozi wanatakiwa kufahamu kwamba suala la kuwatumikia wananchi sio jambo la hiari bali ni lazima watekeleze kwa vitendo ahadi walizotoa wakati wa kampeni kwani wasipotekeleza Wajibu wao vizuri kwa jamii mwisho wa siku kitakacho hukumiwa ni Chama na sio kiongozi husika.


Aidha aliwakumbusha viongozi hao kwamba Chama na Jumuiya zake wanatarajia kufanya Uchaguzi mwaka 2017, hivyo waanze mapema kuwaelimisha, kuhamasisha na kuwaandaa kisaikolojia wanachama wa Chama hicho juu ya matumizi sahihi ya kanuni za UChaguzi ili kuepuka lawama zisizokuwa za lazima.


Alisema Wanachama wanatakiwa kuwachagua viongozi wenye sifa na wasiokuwa na Mukhari( kuoneana haya) katika kusimamia mambo ya msingi ya CCM na waumini wa kweli wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Muungano wa Serikali mbili wenye vigezo hivyo ndio wanaofaa kuwa viongozi.


Hata hivyo aliwapongeza Rais wa Zanzibar, Dkt. Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli kwa juhudi na kasi zao za kufanikisha mipango ya maendeleo ya nchi kwa ufanisi mkubwa hali inayoongeza hamasa kwa jamii kuendelea kuwaamini.

SAKATA LA KATIBA MPYA: JUKWAA LA KATIBA WAMNG'ANG'ANIA RAIS MAGUFULI




Mratibu wa Jukwa la katiba Tanzania JUKATA Ndugu Hebron Mwakagenda Pamoja na Viongozi wengine wa mashirika yanayoshirikiana na Jukata wakionyesha Kitabu maalum ambacho kimezinduliwa Leo kwa ajili ya kuhamasisha Upatikanaji wa katiba mpya baada ya mchakato huo kukwama kusikujulikana. Kitabu hicho kinaeleza Mwelekeo wa katiba Mpya Tanzania,Tulikotoka,Tulipo,na Tuendeko (Picha na Exaud Mtei)

Jukwaa la katiba Tanzania (JUKATA) Rais Magufuli hawezi kukwepa kuhusu suala la kupatikana kwa katiba mpya kwani yeye si Rais wa mgombea huru bali amepelekwa na chama ambacho kimewaahidi watanzania kuwa katiba mpya ni miongoni mwa sera zao.


Kauli hiyo ya jukwaa la katiba imekuja huku kukiwa na sintofaamu kuhusu kupatikana ama kutokupatikana kwa katiba mpya mchakato ambao ulisimama na kupisha uchaguzi mkuu mwaka 2015 na kuacha katika hatua ya Katiba Pendekezwa.




Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam Mratibu wa jukwaa la katiba Tanzania Ndugu Hebron Mwakagenda alisema wameshtushwa na kauli ya serikali ya Tano kuwa mchakato wa Katiba mpya sio kipaumbele cha serikali ilihali katika Ilani ya chama cha mapinduzi ndio Ilikuwa moja ya ahadi zao za kuhakikisha kuwa katiba hiyo inapatikana.



Mratibu wa JUKATA Ndugu Hebroni Mwakagenda akizungumza na wanahabari leo.

DC HAPI AIBUA MADUDU KINONDONI,NI YALE YA TASAF



MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi amemuagiza Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Aron Kagurumjuli kumvua nyazifa za uongoni mratibu wa Mfuko wa Kusaidia kaya masikini(TASAF) katika wilaya kinondoni Onesmo Oyango baada ya kubainika kuwaingiza kwenye malipo watu 1,397 ambao hawana sifa ya kuwalipwa fedha za hizo ambao wameghalimu zaidi ya milioni 266.9. Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo...


Hata hivyo,Hapi amewaomba viongozi wa Mfuko huo, ngazi ya taifa kumchukulia hatua pia mlipaji mkuu wa Taifa kwa hatua yake ya kuhusika kuwalipa watu hao, huku akijua hawana sifa ya kulipwa stahiki hizo.


Pamoja na hayo,Hapi pia ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupamba na Rushwa (TAKUKURU) katika wilaya yake kufanya uchunguzi wa kina kwa wanufaika wote na TASAF ili kujilizisha kama wsanafuaika hao wanasifa za kupewa fedha hizo.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Hapi amesema baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa kwa wanufaika wote wa fedha hizo ambao walitakiwa kunufaika ni watu masikini ambao hawana hata uwezo kuhudumia familia zao lakini wameshangazwa na hatua ya kulipwa watu wasiokuwa na sifa hizo.
,
“Wamelipwa watu wenye uwezo sio masikini au kaya masikini ambazo zilitakiwa kusaidiwa na mfuko huu “amesema Hapi.

Ameeleza kuwa mbali na watu hao wasikuwa na sifa pia wamebaini hata watu walionufaika na fedha hizo hawajulikana hata makazi wanapoishi jambo analodai limetia shaka ata fedha hizo, uwenda zilikuwa zinakwenda kwa wajanja wachache.

“Lazima tumsadia Rais John Magufuli kupambana watu wote wanaofanya ufisadi kwa watendaji ,kwa hiyo hapa naitaka (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa kina ,pamoja na taasisi za kinidhamu kwa wafanyakazi kwa watendaji hawa ili hatua zichukuliwe kwa wate waliohusika na kadhia hii,”ameongeza Hapi.

SERIKALI YAANZA KUAJIRI

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni anapenda kuwatangazia nafasi za kazi Watanzania wenye sifa kama ifuatavyo :-

1. DEREVA II – NAFASI 10.
SIFA:
Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II.

KAZI NA MAJUKUMU:
i)Kuendesha magari ya abiria na malori,
ii)Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa magari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo
iii)Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
iv) Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-Book” kwa safari zote.

NGAZI YA MSHAHARA - TGOS. A

2. KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III - NAFASI 4
SIFA:
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

KAZI NA MAJUKUMU.
Katibu Mahsusi Daraja la III atapagiwa kufanya kazi katika Tyiping Pool au chini ya Katibu Mahsusi mwingine mwenye cheo cha juu kumzidi kwenye ofisi ya Mkuu wa sehemu au kitengo.

i) Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
ii) kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
iii) Kusaidia kutunza taarifa aukumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
iv)Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
v) Kusaidia kufikisha maelezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
vi)Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo,na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
vii)Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi
NGAZI YA MSHAHARA – TGS. B

3. MTENDAJI WA MTAA II – NAFASI 55
SIFA
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha IV au VI aliyehitimu Stashahada (DIPLOMA) katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Jamii kutoka Chuo cha Serikakali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU
i) Katibu wa Kamati ya Mtaa;
ii) Mtendaji Mkuu wa Mtaa;
iii) Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa
iv) Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa;
v) Msimamizi wa Utekelezeji wa Sheria Ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa;
vi) Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama;
vii)Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umaskini katika Mtaa;
viii) Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote;
ix) Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa; na
x) Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
NGAZI YA MSHAHARA – TGS. C

MASHARTI YA JUMLA:
Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzani
Awe amehitimu na Kupata Cheti cha Taaluma cha Kidato cha Nne (IV) NB. Results Slip hazikubaliki
Awe na Cheti cha Kuzaliwa

·Barua zote ziambatane na nyaraka zifuatazo;-

i) Nakala za Vyeti vya Mwombaji vilivyothibitishwa,
ii) Maelezo binafsi ya Mwombaji (Curriculum Vitae),
iii) Picha ndogo za rangi (Coloured Passport size) mbili (2) za Mwombaji za hivi karibuni.

·Kila mwombaji lazima awe na Umri kati ya miaka 18 – 45
·Waombaji wenye Sifa Pungufu au zaidi na zilizotajwa hapo juu hawashauriwi kuomba kwani maombi yao hayatafanyiwa kazi.
.Watumishi waliopunguzwa kazi/kufukuzwa kazi Serikalini hawashauriwi kuomba.
.Waombaji ambao wameajiriwa wanashauriwa kupitishia barua zao za maombi kwa waajiri wao wa sasa
·Barua ambazo hazikuambatishwa na nyaraka zilizotajwa hapo juu (i – iii) hazitashughulikiwa.


JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono, zikiwa na anwani kamili ya Mwombaji, pamoja na namba ya simu na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

MKURUGENZI WA MANISPAA
MANISPAA YA KINONDONI
S. L. P. 31902
2BARABARA YA MOROGORO,
14883 DAR ES SALAAM.

TAREHE YA MWISHO YA KUPOKEA MAOMBI:
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 28.11. 2014 saa 9.30 Alasiri

MDAHALO WA MIGOGORO YA ARDHI KIJIJI CHA UGESA














Mkazi wa Kijiji cha Ugesa Kata ya Ihalimba wilayani Mufindi, mkoani Iringa akitoa maoni wakati wa mdahalo uliofanyika katika kijiji cha Ugesa wilayani humo ukilenga kutafuta suluhisho ili kupunguza migogoro ya ardhi leo. 

Shirika la TAGRODE la mkoani Iringa linaendesha midahalo hiyo katika vijiji vya Ikuka, Mbigili, Mawala, Mawambala na Masalali kwa wilaya ya kilolo na vijiji vya Usokami, Ugesa, Makungu, Magunguli na Isaula wilaya ya Mufindi kupitia mradi wake wa CEGO unaohusisha jamii ya vijijini katika uwajibikaji wa masuala ya ardhi ya kijiji. (Picha na Friday Simbaya) 






WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...