Friday, 12 June 2015

MAHAMOD MGIMWA ANOGESHA ZAWADI ZA MSHINDI WA KOMBE LA MUUNGANO







naibu waziri wa maliasili na utalii mahamod mgimwa ambye pia mbunge wa jimbo la mufindi kasikazini.



hapa mabingwa wa kombe hilo wakishangia ushindi pamoja na mgeni rasmi pamoja na viongozi mbalimbali.



mratibu wa mashindano hayo aliyetangaza kustahafu kuratibu mashindano hayo. 




na fredy mgunda,iringa

akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya kombe la muungano mratibu wa kombe hilo DAUDI YASSIN alimpongeza mbunge wa mufindi wa jimbo la mufindi kasikazini ambaye pia ni naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMOD MGIMWA kwa kisaidia kutoa zawadi.

UN YATAKA KUWEZESHWA ZAIDI KWA SERIKALI ZA MITAA





Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) wakikagua mitaala ya kufundishia kwenye ofisi za walimu katika shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi wa awamu ya pili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika kijiji cha Chasimba, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani humo huku Afisa Program Kitengo cha Uahulishaji Fedha (TASAF), Edith Mackenzie (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa ugeni huo.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo

MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania Alvaro Rodriguez ametaka serikali za tawala za mikoa na serikali za mitaa kuwezeshwa zaidi ili kuweza kuwatumikia wananchi.

Aliyasema hayo wakati alipozuru kijiji cha Chasimba mwishoni mwa juma akiwa na Balozi wa Hispania Luis Cuesta Civis kuona miradi ya maendeleo inayofadhiliwa kwa pamoja kati ya serikali ya Tanzania, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Hispania.

Mratibu huyo alisema kwamba mafanikio makubwa yanayoonekana katika kijiji cha Chasimba ni matokeo ya ushirikiano mzuri wa wadau wa maendeleo na wanakijiji.

Alisema ushirikiano huo ni muhimu katika kutokomeza umaskini uliokithiri katika jamii.

Alisema pamoja na mafanikio hayo Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo wangelipenda kuona serikali za mitaa zinawezeshwa zaidi ili kuweza kusaidia jamii kama inavyofanyika sasa katika kijiji cha Chasimba.

Kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji kadhaa nchini vinavyofaidika na mpango unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF, ambao nao unachangiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo.

Alisema anapenda kuona kwamba maisha ya wakazi wa kijiji hicho yanabadilika na kuwa kama ya mama Kicheko ambaye ameondoka katika umaskini uliokithiri baada ya kutumia vyema mradi uliofikishwa kijijini hapo.

Alitoa wito kwa wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kusaidia kuwezesha serikali za mitaa na mashirika yanayoapambana na umaskini nchini kuwezesha miradi ya kuondoa umaskini kufanikiwa.

Bi. Kicheko ambaye mwaka mmoja uliopita alikuwa hohehahe kwa sasa anatengeneza sabuni, ameboresha nyumba yake kwa kuiwekea bati na ana kula mlo zaidi ya mmoja sasa.

Katika ziara hiyo, Mratibu huyo alitaka kujua wananchi wa Chasimba katika miaka mitano hadi saba ijayo wanataka kuwaje na kujibiwa kwamba wanataka kuwa na hali bora zaidi ilivyo sasa na kuanzisha viwanda vidogo.


Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) wakipitia baadhi ya kurasa za mwongo wa kufundishia kitabu cha Uraia wakati wa ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga, alisema mpango huo wa miaka 10 ambao umeingia katika mwaka wa tatu umelenga kuwezesha afya, elimu na lishe na sasa wanafanya kuwajengea uwezo wa kuweka akiba na kuwekeza.

Alisema uwekaji akiba huo unawezekana kwa kutoa ajira wakati wa vipindi vigumu.

Alisema mpango huo wa kukabili umaskini uliokithiri unachangiwa pamoja na Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo la Uingereza, Shirika la maendeleo la Sweden na serikali ya Tanzania.

Alisema kuna kaya milioni moja zinazokula mlo mmoja ambazo zinatakiwa kubadilishwa kuwa katika hali bora.

Aidha alisema wameshakamilisha kutengeneza ramani ya umaskini baada ya kumaliza kuandikisha kaya maskini zilizopo nchini.

Diwani wa kata ya Yombo ambapo kijiji cha Chasimba aliyejitambulisha kwa jina la Idd alisema kwamba ni matarajio yao katika miaka 10 ijayo kubadilika kabisa kutokana na kijiji hicho kuwa na umeme na maji ya kutumia.

MEMBE: TUMCHAGUE RAIS MWENEYE HEKIMA NA BUSARA


WAGOMBEA urais waendelea kumiminika mkoani Iringa kusaka wadhamini wakutia saini fomu za udhamini kwa ajili ya kuteuliwa uwania urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepata wadhamini 380 mkoani Iringa katika harakati zake za kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...