WAGOMBEA urais waendelea kumiminika mkoani Iringa kusaka
wadhamini wakutia saini fomu za udhamini kwa ajili ya kuteuliwa uwania urais
katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe amepata wadhamini 380 mkoani Iringa katika harakati zake za kuomba
kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa
Mwaka huu.
Wadhamini hao kutoka wilaya zote tatu za mkoa wa Iringa
walianza kukusanyika katika ukumbi wa chama hicho mjini Iringa majira ya saa
saba mchana na wakaendelea kumsubiri mgombea huyo hadi saa nne usiku
alipowasili akitokea mkoani Njombe.
Akiwashukuru wadhamini hao, Membe alisema; “miongoni mwa
ngome zangu kubwa sana za kisiasa nchini ni mkoa wa Iringa. Katika Uchaguzi wa
Halmashauri Kuu ya Taifa, wajumbe wa mkoa wa Iringa walinipa kura zao zote.”
Alisema CCM ina utaratibu mzuri sana wa kuchuja na kupitisha
viongozi wa kitaifa na kwa ukubwa wake ndio sababu kuna wagombea wengi wa urais
wanaojitokeza kuwania nafasi hiyo.
“Watanzania msikiache chama hichi, tuna marafiki duniani
kote, ni chama ambacho kimesaidia kupatikana kwa Uhuru kwa nchi zaidi ya nane
barani Afrika.
Akizungumzia nafasi anayoiwania, Membe alisema; “urais
haujaribiwi wala sio kazi ya kukurupuka, ni lazima uwe umejipanga na wenzako
waamini kwamba wewe unaweza kugombea na lazima uwe na hekima na busara.”
Huku hotuba yake ikikatizwa mara kwa mara na shangwe na
vifijo toka kwa wadhamini hao, Membe alisema uzoefu wa uongozi alionao ndani na
nje ya nchi umemsukuma kuomba nafasi hiyo.
“Nikijaariwa kuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,
angalieni timu nitakayojenga, baraza la mawaziri nitakalochonga, litakuwa na
vijana, wanawake na wazee kwasababu wazee ni dawa,” alisema.
Alisema anataka kuiondoa nchi hapa ilipo na kuipeleka kwenye
uchumi wa viwanda vitakavyotegemea kilimo na akawaponda wagombea wasiojua nini
wanatakiwa kufanya endapo watachaguliwa kwa kisingizio kwamba wanategemea
vipaumbele vyao vipo kwenye Ilani.
Pamoja na mambo mengine Membe alisema akichaguliwa kuwa rais
atahakikisha atajenga uchumi wa viwanda ili mazao ya kilimo ya wezekusindiwa
nchini.
Alisema kuwa atataka kujenga uchumi wa kiviwanda wakitegemea
ambao utawezesha wakulima wapate soko ya mazao yao ndani ya nchi.
Alisema kuwa kwa muda mrefu nchini inasifika kwa namba moja
kwa kuzalisha malighafi ambayo inanufaisha nchi zingine ambao wanapata faida
kubwa kuliko sisi.
Aliongeza kuwa akiwa rais atahakikisha anafufua viwanda
vikiwemo vya Iringa ili viwezekuajiri watu wengi na hatimaye kupunga umaskini.
Aidha, Membe waliwa atahadhilisha wananchi kuwa makini na
wagombea wanaotumia magunia ya fedha kuwanunua wapigakura kwa hawanania njema
na nchi.
Alisema kuwa mgombea yeyote anayetumia nguvu ya fedha
kuwanunua wananchi ataona haya kuwakemea wenzake wanaopatikana na hatia ya
rushwa.
Mgombea mwingine aliyefika mkoani hapa ni Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambaye pia ni Mbunge wa
Bumbuli (CCM) aliyepokeliwa na wanachama na mashabiki wengi na kujizolea
wadhamini 680 waliyotia saini kwenye fomu zako na hatimaye kuelekea mikoa ya
Njombe na Mbeya.
Aliwaomba wananchi wa Iringa na nchi kwa ujumla wape ridhaa
ya kuteuliwa na chama chake ili aweze kupeperusha bendera ya Jumhuri ya
Muungano wa Tanzania (JMT).
Wengine ambao wanakuja mkoani Iringa kusaka wadhamini ni pamoja
na Waziri wa Kilimo na Chakula, Steven Wassira na aliyekuwa mkuu wa Mkoa
Iringa, Monica Mbega.
IDADI ya wagombea nafasi ya Urais kupitia CCM sasa imefikia
28 baada ya makada wengine sita kuchukua fomu.
No comments:
Post a Comment