Wednesday, 16 March 2016

RUNGU LA MAGUFULI LAWAANGUKIA WAPIGA DEBE,SASA WATAKIWA KUKAMATWA MARA MOJA


Waziri nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane



NA KAROLI VINSENT

SIKU moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuwaagiza wakuu wa mikoa wapya kuwakamata vijana wote ambao wanacheza (poolTable) nyakati za asubuhi,kwa madai kuwa wajiingize kwenye shughuli za ufanyaji kazi,


Naye,Waziri nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhakikisha anawaaondoa wapiga “debe” wote kwenye vituo vya mabasi kwa madai kuwa wanafanya vitendo vya kiharifu.

Waziri Simbachawene ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam,wakati wa semina kwa wakuu wa mikoa wote nchini ambao waliapishwa jana na Rais Magufuli,


Ambapo alitumia nafasi hiyo kwa kusema kazi ya kupiga debe sio rasmi na aina kipato kitachoweza kumkwamua kijana kuondokana na tatizo la umasikini,


“Yaani hata hapa Dar es salaam namuomba mkuu wa mkoa ahakikishe anawondoa hawa wapiga debe kwenye vituo vya mabasi kwani wamekuwa wakichangia kutokea kwa uharifu,kipato cha mpiga debe kwa siku hakiwezi kumkwamua kimaisha sana sana wanatumia nafasi hiyo kufanya uharifu wanatakiwa kuondolewa haraka waende kwenye kazi hata za kilimo”amesema Simbachawene.


Hata Hivyo Waziri Simbachane ametumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa mikoa kufanya kazi kwa ufasaha na kuwatumikia wananchi ikiwemo kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.

BALOZI JUMA MWAPACHU AREJEA CCM



Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba 2015, nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yangu ya uanachama kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni. Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo hayo pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook). Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima haki ya kugombea mcha mungu Edwad Lowasa. Nikasema Edwad Lowasa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la Watanzania. Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edwad Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe Magufuli.

Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowasa, nililewa ahadi ya Lowasa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowasa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.

Leo natangaza kurudi CCM kwasababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye. Nilihama kwa kwasababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi kwasababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama. Usemi wa CCM kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana yake. Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.

Naomba mnisamehe kwa kulifanya jambo langu la kujitoa CCM na kurudi CCM kuwa jambo la kitaifa ukizingatia kwamba sikuwa na nafasi yoyote ya uongozi wa CCM wakati nahama na pia sijawahi kuwa hata Mjumbe wa NEC ya CCM na nilikuwa nje ya ulingo wa siasa za CCM kwa miaka 20. Niliamua kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.

Naomba radhi kwa familia ya baba wa taifa Mwalimu Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14 Octoba) na kutumia msiba wake kutoa kauli za kisiasa zidi ya chama chake alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa mwanachama.

Wananchi wote tumuombee Magufuli na tumsaidie kwani tumepata nyerere mpya.

Mungu Ibariki Tanzania 
mungu Ibariki Afrika

Balozi Juma Mwapachu

“Mwanamke wa Afrika bado anakabiliwa na changamoto” - Waziri Ummy Mwalimu



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ( Mb) ametoa hutuba kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Mkutano huu wa wiki mbili unawakusanya wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubalishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.

Wakati mamia ya wanawake kutoka serikalini na Asasi za Kiraia wakiwa wanakutana hapa Umoja wa Mataifa kwa mkutano wao unaojadili hali yao katika maeneo mbalimbali. Mamia mengine ya wanawake hususani wale wa Afrika wanaendelea kukumbana na changamoto lukuki zinazowarudisha nyuma kimaendeleo.

Ni wanawake hao wanaoishi katika nchi zenye migogoro, vita visivyokwisha, wenye kukabiliwa na uhaba na ukosefu mkubwa wa chakula, maji safi na salama, matatizo yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, ndio ambao Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu(Mb) ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya ushirikiano ili malengo mapya ya maendeleo endelevu (Agenda 2030) yaweze kuwafikia.

Waziri Mwalimu ametoa wito huo jana jumatatu, wakati alipotoa hutuba kwa niaba ya nchi za Afrika katika siku ya kwanza ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya wanawake (CSW) ambao umeanza hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akitoa hotuba katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). 

Changamoto hizo pamoja na nyinginezo nyingi zikiwamo kutopata fursa ya huduma za afya ya uzazi salama, elimu na usawa wa kijinsia zinamfanya mwanamke wa Afrika ashindwe kushindana na wanawake wenzie hususani wale walioko katika mataifa yaliyoendelea. 

Waziri Mwalimu ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu wa wiki mbili, alitoa hotuba hiyo kwa niaba ya nchi za Afrika kutokana na kwamba Tanzania kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ni Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika kwa mwezi huu wa March.

Amewaeleza washiriki wa mkutano huo waliofurika katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwamba ingawa pamekuwapo na makubaliano na mapendekezo mengi kuanzia yale yaliyofikiwa huko Beijing, bado mwanamke anayeishi katika nchi zenye migogoro na vita barani Afrika ataendelea kuachwa nyuma na hivyo kukosa fursa ya kushinda na wenzie.

“ Ingawa vita, ukame wa kutisha, ukosefu wa chakula, ukosefu wa maji safi, ukichanganya na ukosefu wa fursa za kiuchumi, kijamii na kisiasa ni matatizo yanayowakabili watu maskini lakini mwanamke ndiye anayeathirika zaidi,” alieleza Waziri Mwalimu.

Na kuongeza kwamba Afrika inaendelea kutilia mkazo hoja ya kuwashirikisha wanawake katika majadiliano na utoaji wa maamuzi katika masuala yanayowagusa yakiwamo masuala yanayohusu mabadiliano ya tabia nchi na usuluhishi wa migogoro. 

Alieleza kwamba, nchi zinazoendelea na zilizoendelea zinapashwa kuongeza kasi ya ushirikiano na ubia baina yao ili kufanikisha utekelezaji wa Agenda 2030), Makubaliano juu Mabadiliko ya Tabia nchi yaliyofikiwa huko Paris Ufaransa mwaka jana na makubaliano yaliyofikiwa na waafrika wenye kupitia Ajenda 2063 , ili katika umoja wake dunia basi iweze kumwondoa mwanamke na jamii nzima kutoka hapa ilipo na kufikia hali bora zaidi ya maisha.

Kama hiyo haitoshi Waziri alisema, Afrika inaamini pia katika uwezeshwaji wa Sekta binafsi, kupanua wigo wa ujasiliamali kama njia mojawapo ya kukuza uchumi endelevu , usawa wa kijamii, usawa wa jinsia, ulinzi wa mazingira na uwezeshaji wa mwanamke. 

Mada kuu ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake, ni “Uwezeshaji wa Wanawake na uhusiano wake na Ajenda 2030.

Awali akizungumza mwanzoni mwa mkutano huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amasema tangu alipoingia madarakani mwaka 2006 amejjitadi kuongeza nafasi za viongozi wanawake katika Idara za Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akiwa katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Tanzania wa Kudumu Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manong.

Akitilia msisitizo hoja na haja ya kupanua wigo wa wanawake kushika nafasi katika ngazi za juu za maamumizi, Ban Ki Moon amesema, ingawa nchi nyingi zimejitahidi sana kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za juu za uongozi bado kuna Nchi Tano ambazo hazina wanawake katika Mabunge yao ili hali Nchi nyingine 7 hazina mawaziri wanawake katika serikali zao.

Naye Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa Bw Monges Lykketoft, akizungumza wakati wa mkutano huo, pamoja na kusisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Agenda 2030 ambayo ameitaja kuwa ni jumuishi ameendelea kupigia chapuo la kutaka Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa awe Mwanamke.

Na Mwandishi Maalum, New York


A big night for Clinton, as she wins in four states

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...