TIMU ya Abasia Peramiho FC jana waliitafuna Abasia Hanga FC mabao 2-0, katika mechi ya kirafiki iliyofanyika Uwanja wa Hanga Wilayani Namtumbo, Mkoani Ruvuma.
Timu hizo zote mbili ni za watawa ambapo Abasia Peramiho ni wa ‘Benedictine White Fathers’ wa Peramiho ya Wilaya Songea (V) na Abasia Hanga ni ya ‘African Benedictine Fathers’ wa Hanga wilayani Namtumbo., Mkoani Ruvuma.
Katika mechi hiyo, Abasia Peramiho ilingia kwa nguvu na kupeleka mashambulizi mfululizo na kufanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika chache za mwanzo kipindi cha kwanza, lilofungwa na Davis Komba baada ya kupata klosi kutoka kwa winga wa kulia wa timu hiyo.
Kama hivyo haitoshi, Abasia Peramiho waliaandika bao la pili kwa kupata penati baada ya mabeki wa Timu ya Hanga kumuangusha mshambuliaji wa Abasia Peramiho, Bro.Jerome katika eneo la hatari, na Mwamuzi Bro. Deogratias Komba kutoka Peramiho kuwazawadia penati.
Bada ya kufungwa mabao hayo, Hanga FC ilitulia na kuanza kupeleka mashambulizi langoni mwa Abasia Perahiho, lakini hata hivyo mabeki wa wapinzani wao walikaa imara kwa kuondoa hatari zote.
Kipindi cha pili kilianza timu zote zikafanya madiliko lakini haikuwa ni bahati kwa Timu ya Hanga FC mabeki wake tena walifanya madhambi kwa mshumbuliaji wa Abasia Peramiho FC, na Peramiho kupata penati ya tatu lakini bahati nzuri kipa wa Hanga aliipangua shuti kutoka kwa mpiga penati.
Penati hiyo ilipigwa na Mshambuliaji wa Peramiho, Bro. Gabriel ambao hata hivyo alikosa baada ya kipa wa Hanga kuutema mpira kutokana na shuti kali kutoka kwa mpiga penati.
Licha Hanga kufanya juhudi za kutafuta bao lakini bahati haikuwa yao baada ya mabeki wa wapinzani walikuwa imara. Dakika za mwisho, Hanga walikosa mabao ya wazi kwa kuwa kipa wa Peramiho aliyapanguwa kwa ustadi.
Timu ya Abasia ya Hanga ya Wilaya ya Namtumbo, Mkoani Ruvuma
Timu ya Abasia ya Peramiho ya Peramiho, Songea vijijini Mkoani Ruvuma
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...