MJUMBE
wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Abri Asas,
amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 29, huku akiwatoa hofu juu ya uvumi unaoenezwa mitandaoni kuhusu uwepo
wa vurugu siku ya uchaguzi huo.
Asas
amesema kumekuwepo na taarifa zisizo sahihi kutoka kwa baadhi ya watu, ndani na
nje ya nchi, wanaotumia mitandao ya kijamii kuhamasisha maandamano na kuchochea
vurugu ambazo zinaweza kuhatarisha amani na kuathiri zoezi la uchaguzi.
Akihutubia
maelfu ya wanachama na wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM Jimbo
la Mafinga Mjini, uliofanyika katika kijiji cha Ugute, kata ya Isalavanu,
Halmashauri ya Mji Mafinga, Asas aliwahakikishia wananchi kuwa nchi ipo salama
na vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kikamilifu kulinda amani.
“Nataraji
katika siku hizi mbili mtajitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Oktoba 29.
Msiogope wala kuwa na hofu, amani ipo na kutakuwa na ulinzi wa kutosha. Nchi
yetu imetulia — hayo yote ni maneno ya mitaani,” alisema Asas.
Amesisitiza
kuwa Tanzania ipo kwenye mikono salama ya vyombo vya ulinzi na usalama, hivyo
wananchi wanapaswa kutumia hali hiyo kama motisha wa kushiriki uchaguzi na
kutimiza haki yao ya kikatiba.
Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Dickson Lutevele maarufu kama Villa, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kama ishara ya shukrani kwa Serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika eneo hilo.
Aidha, aliwasisitiza wananchi wote—bila kujali itikadi za kisiasa au imani za kidini—kudumisha amani ambayo ndiyo msingi wa maendeleo endelevu.
“Ni imani yangu kuwa Mufindi kwa mara nyingine tena tutaongoza kwa wingi wa kura kukichagua Chama Cha Mapinduzi kama kawaida yetu,” alisema Villa.
Asas
urges voters to turn out in large numbers, dismisses election violence fears
Iringa. A member of the CCM Central
Committee (MCC), Salim Abri Asas, has urged Tanzanians to turn out in large
numbers to cast their votes in the upcoming General Election on October 29,
assuring them that the country remains peaceful and well-secured.
Mr. Asas dismissed circulating
rumours on social media suggesting that there might be violence on election day,
saying such claims are being spread by individuals with ill intentions to
create fear and discourage voter participation.
He said in recent weeks, there have
been coordinated attempts by certain groups, both within and outside the
country, to incite youths and other sections of the community to engage in
demonstrations and acts that could disrupt peace and affect the election
process.
Speaking during a well-attended CCM
rally to close the party’s campaigns for Mafinga Urban Constituency,
held at Ugute Village in Isalavanu Ward, Mr. Asas assured
citizens that the security organs are fully prepared to maintain order and
safety throughout the election period.
“I expect all of you to turn out in
large numbers to vote on October 29. Do not be afraid or worried — peace
prevails, and there will be enough security everywhere. Our country is calm;
those stories are just rumours,” said Asas.
He added that Tanzania is in safe
hands under its security institutions, urging citizens to take advantage of the
prevailing peace to fulfil their constitutional right to vote.
On his part, Dickson Lutevele,
popularly known as Villa, who is vying for the Mafinga Urban
parliamentary seat, expressed confidence that residents will show up in large
numbers to vote as a sign of appreciation for the government’s development
efforts in the area.
He emphasized that regardless of
political affiliation or religious belief, citizens should prioritize peace,
which he described as the foundation of inclusive and sustainable development.
“I strongly believe that once again,
Mufindi will lead with overwhelming votes in favour of the CCM, as has always
been our tradition,” said Villa.





No comments:
Post a Comment