Thursday, 8 June 2017

HABARI KUHUSU UTAMBUZI NA USAJILI WA WAKAZI WA MANISPAA YA IRINGA


Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa tumeanza zoezi la Kutambua na Kusajili wakazi wa Manispaa ya Iringa.
Zoezi limeanza tarehe 07/06/2017 na linatarajiwa kukamilika tarehe 05/07/2017. Zoezi linaanza saa 1 asubuhi hadi saa 11 Jioni. Zoezi litafanyika katika Vituo vya Usajili vilivyopo katika Kata zote 18 za Manispaa ya Iringa kwa mujibu wa Ratiba ilivyopangwa kila Kata imepangiwa siku 3 za usajili.   

Zoezi za usajili litahusisha wananchi wote raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.

Vitu vya Msingi anavyotakiwa kwenda navyo Mwananchi Raia wa Tanzania katika kituo cha usajili ni:-

1.   Nyaraka halisi (original) na vivuli vya kuthibitisha uraia na umri wa Mhusika,
2.   Cheti cha Kuzaliwa,
3.   Pasi ya Kusafiria,
4.   Vyeti vya Elimu ya Msingi na Sekondari,
5.   Leseni ya Udereva,
6.   Kitambulisho cha Bima ya Afya,
7.   Kitambulisho cha Mpiga kura.

Kwa kuwa zoezi hili linahusisha upigaji wa Picha, kwa ajili ya ubora wa picha, Tunaelekeza yafuatayo kwa wananchi:-
· kutovaa nguo Nyeupe, Kijivu, Bluu mpauko, Pinki, nguo zenye kung’aa sana, Jezi, nguo zenye nembo, kofia aina yeyote ama kupaka Hina mikononi.

Matarajio katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni kusajili wakazi 130,000 kwa ajili ya Vitambulisho vya Taifa.

Mwananchi jitokeze Usajiliwe ili Upate Kitambulisho cha Taifa kwa Maendeleo yako na Taifa kwa Ujumla
Imetolewa na:

Dennis Gondwe,
Afisa Habari- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
IRINGA8/6/2017 

RATIBA YA USAJILI KATIKA KATA NI KAMA IFUATAVYO:
SN
JINA LA KATA
TAREHE ZA USAJILI
1
KITWIRU
7-9/6/2017
2
RUAHA
7-9/6/2017
3
IGUMBILO
10-12/6/2017
4
MSHINDO
10-12/6/2017
5
KITANZINI
10-12/6/2017
6
MIVINJENI
10-12/6/2017
7
MLANDEGE
13-15/6/2017
8
KWAKILOSA
13-15/6/2017
9
ILALA
13-15/6/2017
10
MWANGATA
18-20/6/2017
11
ISAKALILO
18-20/6/2017
12
MKWAWA
21-23/6/2017
13
MAKORONGONI
24-26/6/2017
14
GANGILONGA
24-26/6/2017
15
KIHESA
27-29/6/2017
16
MTWIVILA
30/6-02/7/2017
17
MKIMBIZI
30/6-02/7/2017
18
NDULI
3-5/7/2017


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...