Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Luckness Amlima Leo ameamuru mbolea iliyokuwa imeletwa wilayani humo kwa ajili ya wakulima wa zao la Tumbaku na madereva kuzuia kushusha mbolea hiyo wakidai walipwe gharama za usafirishaji wa mbolea hizo ameamuru zishushwe mara moja na wagawiwe wakulima.
Akiongea na madereva na wakulima hao katika viwanja vya ushirika wilayani humo mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa hakuna sababu ya kuendelea kubaki na mbolea kwenye magari huku wakulima wakilalamikia tumbaku inaharibika kwa kukosa mbolea.
“Shusheni mbolea kwani madai ya fedha ya kusafirishia mbolea hiyo yanafanyiwa kazi na chama kikuu cha Ushirika SONAMCU alisema mkuu wa wilaya huyo.
Aidha mwandishi msaidizi wa chama cha msingi Namtumbo bwana Nasoro Makomaye alisema kuwa mbolea ilifika wiki mbili zilizopita lakini madereva walikataa kushusha mbolea hiyo wakidai fedha ya kusafirishia mbolea hiyo.
Bwana Nasoro alimshukuru mkuu wa wilaya ya Namtumbo kwa kuwasikiliza kilio chao cha kushusha mbolea hiyo na wakulima wagawiwe mbolea hiyo na waweze kuitumia katika zao la Tumbaku.
Hata hivyo bwana Nasoro aliongeza kuwa kitendo cha mbolea hiyo kucheleweshwa itasababisha mapato ya uzalishaji wa zao la tumbaku kushuka na hasa ukizingatia muda wa kuweka mbolea kwenye zao hilo ulisha pita.
Naye Hamisi Rajabu Lyemo mkulima wa zao la Tumbaku alidai kuwa pamoja na mkuu wa wilaya kuwasaidia katika kuhakikisha mbolea hiyo inateremshwa na wanagawiwa wakulima bado mbolea hiyo haina tija sana kwa wakulima kutokana na namna ilivyochelewa kuletwa kwa wakati.
Bwana Hamisi alidai alipamba tumbaku shambani kwake tarehe 11.Desemba mwaka huu na alitakiwa kuweka mbolea siku saba baada ya kupanda yaani tarehe 18Desemba lakini tumbaku hizo zimekomaa bila mbolea na kuonesha wasiwasi wake katika uzalishaji wa zao hilo pamoja na kukosekana kwa ubora wa zao hilo.
Madereva wa magari yaliyoamriwa kushusha mbolea hiyo bwana Elieza Mshana na Hamza Shelukindo wakazi wa Dar-es-salaam walidai wanakubaliana na maamuzi ya mkuu wa wilaya kushusha mbolea na kumwomba mkuu wa wilaya huyo kusimamia malipo yao ya usafirishaji wa mbolea hiyo .
Katibu wa mbunge wa jimbo la Namtumbo Kalela Amimu ambaye ndiye msimamizi wa ugawaji wa mbolea hizo alisema kuwa mahitaji ya mbolea katika wilaya ya Namtumbo ni mifuko 11061 ikiwa mbolea ya NPK ni mifuko 6,617 mbolea ya CAN mifuko 2,222 na mifuko 2,222 ya UREA ambapo mpaka sasa mbolea iliyopokelewa ni mifuko 6000 pekee.