Thursday, 26 March 2015

JEMBE FM YA MWANZA YAPEWA LESENI



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi leseni kwa redio ya Jembe FM ya jijini Mwanza kwenye ofisi za makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma ametaka matumizi sahihi ya masafa ya radio yanayatumiwa kurusha vipindi vya radio kwa ajili ya maendeleo ya umma.

TAHARIRI: TABIA HII YA WAUZA MITUMBA SOKO LA MCHIKICHINI NI UDHALILISHAJI WA KIJINSIA




Baadhi ya wateja wa nguo wakichagua nguo kwenye soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam.

Na Andrew Chale wa Modewji blog

Miongoni mwa mambo ya aibu katika jamii ni pamoja na masuala ya udhalilishaji wa kijinsia ukiwemo ule wa maungoni hasa kwa wanawake.

Kwa muda mrefu mtandao huu umekuwa ukifuatilia vitendo hivyo vibaya kwa jamii vinavyofanywa na watu waliokosa ustaarabu hasa jamii ya vijana katika maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi karibu maeneo mengi ikiwemo jiji la Dar es Salaam. 

Miongoni mwa eneo linaloongoza kwa kuwadhalilisha wanawake ni eneo la soko la Mchikichini lililopo Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

Mtandao huu umekuwa ukishuhudia vitendo hivyo vibaya kwa jamii ambapo wengi wa vijana wamekuwa wakifanya kwa makusudi kuwadhalilisha wanawake hasa wasichana wadogo kwa kuwashika maungoni (makalio, kifua/maziwa) huku wakiwalazimisha kununua bidhaa zao.

Vitendo hivi vimekuwa ni kama mchezo wa kawaida kwani vijana hao wamekuwa wakiendeleza hali hiyo kwa muda mrefu sasa huku wasichana/wakike hao wanaofanyiwa vitendo hivyo wakiwa hawana wa la kufanya, Mtandao huu tunasema huo ni udhalilishaji na unatakiwa kuchukuliwa hatua za haraka kukomeshwa kwani unakiuka maadili na utu wa mwanamke.


Modewji blog tunatambua ipo mamlaka husika zinazoweza kulichukulia hatua suala hili basi kama zipo zianze sasa kwani udhalilishaji huu huko mbele unaweza kuleta madhara makubwa kwa mtendewa na hata anayetenda kwani akiachwa sasa baadae anaweza kufanya tukio kubwa na likafumbiwa macho ikiwemo kubaka.

Nachelea kuamini kama vijana hawa wanafanya hivi kwa kujiamini ama kuna nguvu ya msukumo nyuma yake? Kipindi cha nyuma sote tumekuwa tukishuhudia vijana hao wakiwachania nguo wanawake waliokuwa wakivaa vimini waliokuwa wakipita katikati ya mitaa ya Kariakoo wakati huo huo wamesahau kuwa nguo hizo wamewauzia wao, tukiacha hilo pia wapo hawa Makondakta wa daladala nao ni miongoni mwa watu wanaoongoza kufanya vitendo vya kidhalilishaji wanawake.

Mtandao huu umeweza kuliona hilo kwa upande wa Makondakta wa Daladala nyingi hasa nyakati za abiria wa kike anapopanda hatua ya kwanza wao wanapeleka mkono kwenye ‘Makalio’ ya Mwanamke na kumvutia ndani ya daladala, yaani kama sapoti ya kumuingiza ndani.

Kondakta anafanya hivyo wakati huo amekaa mlangoni mwa daladala yake, lakini anapopanda mwanaume usogea ndani ama hushuka chini bila hata ya kumshika, lakini akipanda Mwanamke tu utakuta Konda anamshika makalio kuona kwamba ni jambo la kawaida, Hivyo ni wakati sasa wa kubadilika jamani vitu vingine hivi ni kushusha utu wa mwanamke hivyo tubadilike na tuchukue hatua, Asante.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...