Saturday, 27 February 2016

MAUAJI YA MBAGALA-RANGI TATU; WAZIRI KITWANGA AOMBA JWTZ IWAPIGE "TAFU" POLISI


Askari wa JWTZ, wakiwa na zana zao, sasa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, atamuomba mwenzake wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ili "wazee wa kazi" waingie kwenye mapambano kuwasaka majambazi waliosababisha mauaji ya watu 7 pale Mbagala Rangi-Tatu jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa sa nane mchana baada ya kuvamia na kupora benki ya Access.

NA K-VIS MEDIA
KUFUATIA mauaji ya watu 7 wakiwemo majambazi watatu pale Mbagala Rangi-Tatu, Ijumaa Februari 26, 2016, waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema atawasiliana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi al Kujenga Taifa, ili wanajesi wa JWTZ, wawasaidie polisi kuwasaka majambazi waliotorokea kwenye msitu wa Kongowe.

Waziri ameyasema hay oleo Februari 27, 2016 wakati akizungumzia tukio hilo ambapo majambazi wasio na idadi, wakiwa na silaha nzito nzito walivamia benki ya Acces tawi la Mbagala na kuiba kiasi kikubwa cha fedha ikiwa ni pamoja na kufanya mauaji ya askari polisi mmoja, mlinzi mmoja wa benki hiyo na mfanyakazi.

Pia majambazi hayo yaliua raia wawili kabla ya raia nao kuyaua majambazi matatu huku emngine yakikimbilia kwenye msitu wa Kongowe ulio jirani na eneo la tukio.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga
Waziri wa Ulinzi na Jeshio la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi

KAMPUNI YA ASAS GROUP YAJENGA KITUO CHA UCHANGIAJI DAMU IRINGA







KAMPUNI ya Asas Group yenye makao yake makuu mjini Iringa, imejenga kituo cha kisasa cha uchangiaji wa damu ndani ya hospitali ya mkoa wa Iringa ili kuboresha huduma hiyo.


Kituo hicho ambacho haikuelezwa kimejengwa kimeanza kutoa huduma hiyo hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kupokea wasamalia wema wanaotaka kutunisha benki ya damu ambayo mahitaji yake ni makubwa yakiongezeka siku hadi siku.

Mkuu wa Kitengo cha Damu Salama Mkoa wa Iringa, Hubert Swallo amesema idadi kubwa ya watu wanajiotokeza kuchangia benki hiyo ya damu ni wale ambao ndugu zao wanahitaji huduma hiyo.


“Ombi letu ni kwa wananchi bila kujali wana wagonjwa wanaohitaji huduma ya damu au hawana wajitokeze kuchangia damu katika benki hii, ili ituwezeshe kuwa na akiba ya kutosha kulingana na mahitaji,” alisema.

uthibitishia mtandao huu kuwepo kwa changamoto kubwa ya wananchi kufika kwa ajili ya kujitolea damu pasipo kuombwa na jamaa zao.

Swallo alitoa wito kwa taasisi zikiwemo za dini, vyuo na shule mbali mbali kujitokeza kuchangia damu.

MWANAHABARI NA BLOGGER GEORGE BINAGI ASHEREHEKEA MIAKA YAKE YA KUZALIWA



Kila ifikapo February 26 ya Kila Mwaka Mwanahabari na Blogger George Marwa BinagiGB Pazzo(Kulia) Mzaliwa wa Kijiji cha Kenyamanyori,Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Kikazi Jijini Mwanza, huadhimisha siku yake ya Kuzaliwa.


Jana wadau mbalimbali waliungana na GB Pazzo kusherehekea siku yake ya Kuzaliwa, ambapo katikati alikuwa ni Mgeni Rasmi ndug.Dede Petro ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Kanda ya Ziwa na Kushoto ni Loyce Nhaluke kutoka Kampuni ya Uuzaji Sola ya M-Power.

Picha Zaidi BONYEZA HAPA


NAPE MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA MWANZA




Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka jijini Mwanza Machi 27.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maaandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Waziri Nape amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litaanzia Geita Machi 26 na kumalizia Kahama Machi 28.

Msama alisema kamati yake inaendelea na maandalizi ya kuelekea tamasha hilo ambalo litashirikisha waimbaji mbalimbali hapa nchini.

“Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema Msama.

Msama alisema baadhi ya waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ambao ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Sifael Mwabuka, Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro na Kwaya ya Wakorintho Wapili.

Aidha Msama alisema viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na kwa watoto shilingi 2000.

Tafrija ya mchapalo wa uzinduzi wa intaneti ya kasi zaidi ya Tigo 4G Mkoani Kilimanjaro yafana




Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi. 






Mkuu wa Kitengo cha Biashara kampuni ya Tigo(B2B), Rene Bascope akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi. 





Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makala(wa pili kulia) akimkabidhi Emmanuel Kilaga, zawadi kutoka Tigo wakati wa hafla uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Mtaalam wa mtandao kutoka Tigo Samira Baamar. 






Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi. 





Mtaalam wa mitandao ya kijamii kutoka Tigo Samira Baamar(wa tatu kulia), akimkabidhi zawadi mmoja kati ya washindi waliojishindia zawadi mbalimbali. 






Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mjini Moshi juzi. 





















MBEYA CITY YATUPWA NJE KOMBE LA SHIRIKISHO BAADA YA KUFUNGWA NA TANZANIA PRISONS BAO 2-1




Wachezaji wa Tanzania Prisons wakimdhibiti mchezaji wa Mbeya City FC, Joseph Mahundi mwenye jezi namba kumi wakati michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup 2015/16) inaendelea kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini. Mbeya City ilifungwa goli 2-1 na Tanzania Prisons katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo. (Picha na Friday Simbaya)






Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup 2015/16) inaendelea wiki hii mzunguko wan ne katika hatua ya 16 bora, kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.

Leo Jumamosi Februari 27, Mwadui FC imemenyana na maafande wa Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga wakati jijini Mbeya Tanzania Prisons wamecheza na Mbeya City kwa bamizwa bao 2-1 katika uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine jijini hapa. Kwa mantiki hiyo Mbeya City FC imefungishwa virago na Tanzania Prison na kuaga michuano hiyo leo.

Hata hivyo mzunguko huo wa nne utakamilika kesho Jumapili ambapo Simba SC watakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Panone FC dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto Africans wakicheza dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.

VURUGU ZA MACHINGA ZAZUA TAFRANI LEO JIJINI MBEYA


Baadhi ya Vibanda vya Biashara vya Wafanyabiashara Ndogondogo Maarufu kama Machinga Vikiteketea kwa Moto mara baada ya Wafanya Biashara hao wa Eneo la Sido na Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya kuanzisha Vurugu Baada ya Kubomolewa Vibanda vyao vya Biashara katika maeneo waliyokuwa wakifanyia Biashara Zao.

Jitihada za kuzima Moto ulio washwa na Wamachinga wa Kabwe na Sido zikifanyika kutoka kwa Jeshi la Zima Moto Jiji la Mbeya katika Vurugu zilizo Dumu kwa Muda kuanzia Asubuhi ya Leo na kupelekea Wamachinga hao Kuchoma Matairi Barabarani na Baadhi ya Masalia ya Vibanda vyao mara baada ya Kubomolewa Vibanda vyao vya Biashara.

Jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza Ghasia kikiwa Ngangari kuhakikisha hali ya Usalama ina kuwa Shwari na Vurugu 
kutoendelea...

Baadhi ya wapiga Debe wa Stendi ya Kabwe wakiwa hawana nongwa na Mtu bali wakiendelea kutimiza agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli kufanya Usafi kila Juma Mosi ya mwisho wa Mwezi na hapo wakiwa Sambamba na Vifaa vyao vya kufanyia Usafi mbele ya Jeshi la Polisi kama waonekanavyo katika Taswira.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...