Monday, 10 January 2011

MUHULA WA KWANZA WA MASOMO

Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Peramiho 'A' Wilayani Songea, Mkoani Ruvuma wakiwa wamebeba nyenzo mbalimbali kutoka nyumbani kwa ajili ya kwenda kufanyia usafi wa mazingira shuleni kwao, ikiwa ni kuanza kwa muhula wa kwanza wa masomo jana. Wanafunzi hao wanasoma darasa la tatu, tano na la sita katika shule hiyo.

NADHIRI ZA DAIMA


Baba Abate wa Abasia ya Peramiho Benedictine, Anastasius Reiser OSB (Mwenye Kofia) akitoa Nadhiri za Daima kwa mabruda watatu katika Kanisa la Abasia Peramiho, Jimbo Kuu la Songea mkoani Ruvuma Jumamosi. Kutoka kushoto kwenda kulia ya mabruda waliyopiga magoti ni  Br. Xaver Mteleke OSB kutoka Parokia ya Kasulu, Jimbo la Kigoma, Br. Ludoviko Komba OSB kutoka Parokia ya  Mjimwemw, Jimbo Kuu la Songea na Br. Martin Mrope OSB Parokia ya Ndanda katika Jimbo la  Mtwara.

Wakiwa na mataji ni mabruda watatu waliopata Nadhiri za Daima katika Kanisa la Abasia Benedictine Peramiho Mkoani Ruvuma Jumamosi. Kutoka kushoto kwenda kulia ni Br.Xaver Mteleke OSB, Parakia ya Kasulu, Jimbo la Kigoma , Br.Martin Mrope OSB Parakia ya Ndanda katika Jimbo la Mtwarana Br. Ludoviko Komba OSB Parakia ya Mjimwema katika Jimbo Kuu la Songea mkoani Ruvuma.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...