Monday, 8 November 2010

MANISPAA YA IRINGA


Raia wa wakigeni wakikatisha mitaa ya Soko Kuu katika Manispaa ya Iringa huku wakiangalia vitu mbalimbali zikiwemo nguo leo  mchana. Mkoa wa Iringa upenda sana kutembelewa na raia wa kigeni wengi kutokana na kuwa hali ya hewa nzuri ya kuvutia pamoja na kuwa na vivutio vingi vya utalii.

MWANDISHI AJITOSA KUWANIA USPIKA

Na Friday Simbaya,
Iringa
Mwandishi wa habari wa Shiriki la Utangazaji Tanzania (TBC-Taifa) Bw. Adeladius Makwega Kazimbaya amejitosa kuwania Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuchukua fomu Ijumaa iliyopita na kurudisha Jumamosi.


Aliwahi kuaandikia magazeti ya THISDAY na KULIKONI ya Media Solution ya Dar es Salaam akiripoti kutoka Mkoa wa Iringa kwa Mwaka mitatu wakati yuko chuoni hapa mkoani kabla ya kupata kazi TBC.






Bw.Makwagaambayekwasasa nimtayarishaji vipindimwandamizi wa shirika la utangazaji tanzania.kwa sasa ni mtangazaji wa TBC-Taifa alizaliwa tarehe 19 September,1974 Mlali , Mpwapwa ,Dodoma. Alipata elimu ya msingi katika shule ya Msingi Mtoni Kijichi na sekondari 1-3 Tambaza Sekondari, kidato cha 3-4 Same Sekondari kidato cha 5-6 Ndanda Sekondari.


Pia alipata Diploma ya Ualimu- Chuo cha Ualimu Kasulu, Kigoma, Shahada ya kwanza ya habari Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa na ni mwanafunzi wa shahada ya udhamili ya uongozi wa biashara (MBA) Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa.


Uzoefu wa Uongozi


1996-1998,-Mwenyekiti Afya na Usafi Ndanda Sekondari
2002-2003- Rais serikali ya wanafunzi Chuo cha Ualaimu Kasulu
2005-2006- Mwakilishi wa wanafunzi wanaosoma shahaba ya habari kwenye bunge la wanachuo Tumaini -Iringa
2006-2008-Makamu rais wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa.
2005-2008- Katibu wa siasa na unenezi wa Tawi la CCM chuo kikuu cha Tumaini Iringa.
2009-2010- Mwenyekiti wa CCM Tawi la Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa.


2010 -Miongoni mwa wagombea Ubunge Jimbo la Kigamboni Dar es salaam.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...