Tuesday, 12 July 2011

MICHEZO YA KITOTO BWANA!

Watoto wa Kijiji cha Lipinyapinya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma wakiigiza kupika kwenye makopo bila kujali hatari ya kuungua na moto kama walivyokutwa na mpigapicha leo mchana. Ni jukumu la wazazi na walezi  kuhakikisha kwamba  watoto hawachezei vitu vya hatari kama moto ili kulinda usalama wao wakati wowote.

USALAMA BARABARANI HUKO WAPI?

Hatari! Wakazi wa Manispaa ya Songea wakianagalia Kipanya kilichopakia kitanda na godoro bila kuwa na kelia ambapo ni kinyume na sheria za usalama barabarani leo mchana. Kipanya hicho hufanya safari zake katoka Stendi Kuu ya Mabasi hadi Peramiho kwa nauli ya 1,000/- kwa kichwa.


ASAS AWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU VURUGU ZA UCHAGUZI

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Abri Asas , amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchagu...