Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake katika kombe hilo zitatoka shule za upili za Iringa Girls, Klerruu, Mawelewele, Mtwivilla, Tangamenda na Kihesa zote za Manispaa ya Iringa. Kombe la Julius Kambarage Nyerere linatarajia kufanyika tarehe 14-10-2010 kwa ajili kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere.
Aidha, Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira Miguu Wanawake cha Mkoa wa Iringa (IRWFA), Mwanaheri Kalolo amesema kuwa maadalizi mashindano ya kombe la Julius Kambarage Nyerere linasuwasuwa kutokana na ukata wa fedha na vitaa na pia kutojitokeza kwa wadhamini.