Meja Dora Kawawa wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa 831 KJ Mgulani (kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula, Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, Dar es Salaam leo jioni , ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambapo kilele chake kitakuwa Septemba Mosi mwaka huu.
Maofisa wa Jeshi wa kikosi hicho wakifurahi na watoto wa kituo hicho baada ya kutoa msaada wao.
Msaada ukitolewa.
Hapa ni furaha pamoja na watoto hao.
Watoto wakipata msaada huo.
Watoto wakipokea msaada.
Hapa ni furaha tupu kwa watoto kwa kupokea msaada kutoka kwa wazazi wao hao.
Picha ya pamoja na watoto hao na viongozi wao.
Na Dotto Mwaibale
JESHI la Kujenga Taifa Kikosi 831 Kj Mgulani limetoa msaada wa vyakula na sabuni kwa watoto waishio Makao ya Taifa ya Watoto Wenye Shida Kurasini jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo kwa niaba ya mkuu wa kikosi hicho Dar es Salam , Meja Dora Kawawa alisema ni moja ya sehemu ya maadhimisho ya kusherehekea miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
"Tumeamua kushiriki shughuli za kijamii kama kutoa msaada na kufanya usafi ikiwa ni kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa jeshi letu ambapo kilele chake kitakuwa Septemba mosi mwaka huu" alisema Kawawa.
Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance alishuru JKT kwa msaada huo na kueleza ni muhimu sana kwa watoto hao na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kujenga taifa bora la kesho.