Monday, 2 November 2015

AMKA NA MAGAZETI NA SIMBAYABLOG





MBUNGE MTEULE JIMBO LA MANONGA AWASHUKURU WANANCHI






Mbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) akiwashukuru wananchi wa Kata ya Ndebezi katika jimbo hilo kwa kumpa kura za kishindo, madiwani na Dkt. John Magufuli aliyekuwa anawania kiti cha urais.





Wananchi wa Kata ya Ntobo wakishangilia kwa furaha mara baada ya Mbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) alipowasili eneo hilo kwa kutoa shukrani kwa wananchi hao kwa kumchagua katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.



Akizungumza na wakazi wa Kata ya Choma, Mbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) alisema ushindi wa kura 31,485 sawa na asilimia 67. 65 aliopewa na wana Manonga dhidi ya Ally Nguzo wa Chadema aliyepata kura 14,420 sawa na asilimia 30.96. Amesema atahakikisha anawapa wananchi hao ushirikiano, usimamizi na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakalibi.“ 

Mke wa Mbunge Mteule Bi Sarah Abdallah akitoa shukrani kwa wananchi wa kata ya Choma kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Mbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) akiwapungi amkono pamoj a na kuwashukuru wananchi wa kata ya Mwashiku kwa kuonesha upendo wa dhati baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo ilo

Hakika ilikuwa ni siku ya furaha kwa wakazi wa jimbo la Manonga




Watahiniwa 15,818 mkoani Iringa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari leo



Picha/Maktaba



Kaimu afisa elimu mkoa wa Iringa, Euzebio Mtavangu amesema kuwa jumla ya watahiniwa 15,818 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari mwaka huu.

Mgawanyo wa watahiniwa hao katika halmashauri ni halmashauri ya Manispaa (4,785), halmashauri ya wilaya ya Iringa (3,368), halmashauri ya wilaya ya Kilolo (2,784) na halmashauri ya wilaya ya Mufindi (4,881).

Akiongelea matarajio ya ufaulu katika mkoa, Mtavangu alisema kuwa mkoa unatarajia kufanya vizuri na kupindukia matarajio ya BRN ya 80%.

Alisema kuwa matarajio hayo yanatokana na mkoa kuwa uliboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Sababu nyingine alizitaja kuwa ni wanafunzi wa masomo ya sayansi kufanya majaribio halisi baada ya kuwa na maabara za kutosha na kufanya ufaulu kwa masomo ya sayansi kuwa mzuri.

Aidha, wingi wa walimu wenye shahada umeongeza chachu ya mafanikio katika sekta ya elimu mkoani Iringa.

Mkoa wa Iringa umekamilisha maandalizi ya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2015 na mitihani yote imefikishwa vituoni.

Kauli hiyo ilitolewa na kaimu afisa elimu mkoa wa Iringa, Mwalimu Euzebio Mtavangu alipokuwa akiongelea maandalizi ya mitihani ya kumaliza kidato cha nne kwa mkoa wa Iringa ulionza leo nchini kote ofisini kwake.

Mwalimu Mtavangu alisema kuwa mkoa wa Iringa una jumla ya vituo 196 vya kufanyia mtihani huo.

Alivitaja vituo hivyo kwa kila halmashauri kuwa ni halmashauri ya Manispaa ya Iringa (44), halmashauri ya wilaya ya Iringa (33), halmashauri ya wilaya ya Kilolo (49), halmashauri ya wilaya ya Mufindi (70) na mitihani yote imefikishwa katika vituo husika.

Akiongelea idadi ya wasimamizi, alisema kuwa mkoa unao jumla ya wasimamizi 527.

Alisema kuwa kwa mujibu wa muongozo wa mitihani hiyo msimamizi mmoja anatakiwa kusimamia wastani wa watahiniwa 40.

Aliongeza kuwa wasimamizi hao miongoni mwao ni walimu kutoka katika shule za mkoa wa Iringa.

Utaratibu wa kuwapata wasimamizi hao ni pamoja na kuwafanyia upekuzi wa kina na kula kiapo cha kutunza siri kwa mujibu wa sheria Namba 3 ya mwaka 1970.

Alisema kuwa semina kwa wasimamizi wa mitihni hiyo zilianza kutolewa kwa halmashauri zote kuanzia tarehe 28-30/10/2015. 

(Na Friday Simbaya, Iringa)  

SHINDANO KUBWA LA KUSAKA VIPAJI VYA 'FREESTYLE FOOTBALL CHAMPIONSHIP'





Tanzania Freestyle football championship (TFFC2016) ambalo ni shindano la kutafuta/kusaka vipaji vya kuchezea mpira yaani freestyle soccer/Freestyle Football wengi hupenda kuita hivyo ambalo linatarajiwa kuendeshwa kama vile mashindano mengine ya kutafuta vipaji kwa njia mbalimbali ikiwemo ile ya TV show.

Waweza wasiliana nao kupitia anuani hapa +255 654 955 825/ +255 655 049 647












KAMA ULIKOSA KIPINDI CHA MKASI CHA SALAMA JABIR NA MO DEWJI TAZAMA HAPA

IMG-20151030-WA0039
: Kipindi extended na bonyeza play hapa chini




WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...