Friday, 23 October 2015

WAHUKUMIWA JELA MMOJA KILA MOJA KWA KWA KUJIANDISHA MARA MBILI BVR



WAKATI wananchi wanajiandaa kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imewahukumu Majuto Kisumbe (22)na Zawadi Mdegela (33) kulipa faini ya laki moja au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kukiri kosa la kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura .

Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Andrew Peter Scout alisema Kisumbe na Mdegela wamehukumiwa kulipa faini au kenda jela mwaka moja kwa kosa la kujiandisha mara mbili kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura (BVR) kinyume na Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

Alisema kuwa katika nyakati tofauti Kisumbe, mkazi wa Mahenga wilayani Kilolo, Mkoa wa Iringa na Zawadi Mdegela wa Ifunda wilayani Iringa walijiandikisha mara mbili katika BVR katika vituo viwili tofauti. 

Hakimu Mkazi Andrew Peter Scout alisema Kisumbe alitenda kosa hilo tarehe 04 Aprili mwaka huu katika Kijiji cha Mahenge, Wilaya ya Kilolo.

Alisema kuwa mtuhumiwa Kisumbe alikutwa na kadi mbili za kupigia kura zenye namba T-1000-7557-236-8 na T- 1000-1387-385-4 alizojiandikisha katika sehemu tofauti eneo la Mahenge.

Naye Mdegela alikutwa na kadi mbili zenye namba T-1001-3631-728-2 na T-1001-2848-874-4.

Hata hivyo hakimu mkazi huyo alisema kuwa Majuto Kisumbe na zawadi Mdegela wamepoteza sifa ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu kutokana kujiandikisha mara mbili kwenye daftari

Kesi hizo ziliendeshwa katika mahakama isiyo wazi na washitakiwa waliomba wapunguziwe adhabu na hakimu alizingatia hilo kwa vile washitakiwa walitenda kosa hilo kwa kutojua na ni mara yake ya kwanza alisema kuwa walipa faini y laki mmoja au jela mwaka moja. 

Wananchi wengi waliofikisha miaka kumi na nane (18) na kuendelea tayari wameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. 

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni hitaji la Kikatiba. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imepewa jukumu la kisheria la kuandikisha wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura pamoja na kuliboresha kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani. 

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Iringa aliongeza kuwa mfumo mpya wa BVR utasaidia kupunguza au kuondoa matatizo yaliyomo kwenye daftari lililopo ikiwamo kuzuia mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja.

Hivi karibuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilibaini kuwa jumla ya wananchi 231,955 nchini walijiandikisha zaidi ya mara moja katika daftari la kudumu la wapiga kura.



Baada ya kuchakata daftari, mchakato wa mwisho wa kuhakiki daftari, hatimaye idadi halisi ya wapiga kura ni 23,154,485 ambapo 22,651,292 waliandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na 503,193 waliandikishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

RIPOTI MAALUM: MABADILIKO YA TABIANCHI YAATHIRI VISIWA VYA MAFIA NCHINI TANZANIA



Moja ya eneo lililoaribika kutokana na hali ya mabadiliko ya tabianchi (Climate Change) katika fukwe ya Kilindoni, katika Kisiwa cha Mafia, Mkoani Pwani, nchini Tanzania. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).


Na Andrew Chale

[MAFIA-ISLAND] Kisiwa cha Mafia kijografia kipo karibu na mlango wa Mto Rufiji kusini mwa Tanzania.

Hata hivyo, Kisiwa hichi ambacho ni Wilaya moja wapo ya Mkoa wa Pwani inakabiriwa kwa kiwango kikubwa na changamoto za Mabadiliko ya tabianchi hasa baada ya wananchi wake wengi kutopata elimu hiyo sahihi.

Imeelezwa kuwa, elimu juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika Kisiwa cha Mafia ambacho pia kinaunda visiwa vidogovidogo zaidi ya vitano, wananchi walio wengi katika kisiwa hicho bado hawajapata elimu sahihi ya kukabiliana na mabadiliko ya kimazingira (Climate Change).

Mtandao huu ambao ulipiga hodi katika kisiwa hicho cha Mafia ili kupata habari za mabadiliko ya tabianchi na namna ya Mabadiliko ya tabianchi yanavyo athiri Kisiwa hicho (How Climate Change effects Mafia Island in Tanzania) ambapo iliweza kuzungumza na maafisa Ardhi, Mazingira na wananchi wa Wilaya hiyo, na kueleza haya:

Kwa upande wa Afisa Mazingira wa Wilaya hiyo, Gideon Zakayo (pichani juu) amebainisha kuwa, Kisiwa cha Mafia kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za Kimazingira ikiwemo hali ya Mabadiliko ya tabianchi huku suala la elimu kwa wananchi likiwa dogo kutokana na kutokuwa na fungu la kutosha.

“Kwa sasa bado hatuna fungu la kutosha kuwafikia wananchi na kutoa elimu ya Mabadiliko ya tabianchi. Ila bado milango ipo wazi kwa mashirika na taasisi binafsi kufika na kutoa elimu hiyo kwa sasa” anasema Zakayo.

Zakayo ameongeza kuwa, Suala la Mazingira ni pana kwani limejumuisha Afya, Maji, Kilimo, Misitu, ardhi na mazingira yote kwa ujumla hivyo wadau wanahitajika kujitokeza kusaidiana na Serikali katika kutoa elimu, kuelimisha sera na taratibu zinazotakiwa kufuatwa na wananchi katika maeneo husika.

Aidha, ameongeza kuwa, katika miongoni mwa visiwa vidogo vidogo ndani ya Mafia, kuna baadhi ya visiwa vimeanza kuharibiwa kutokana na Mabadiliko ya tabianchi.

“Vipo visiwa baadhi tayari vimeanza kuathirika na mabadiliko hayo kwani maji yamekula ardhi. Pia baadhi ya maeneo maji yameweza kuingia katika ardhi na kubadilisha maeneo hayo tofauti na awali.” amebainisha Zakayo, Afisa Ardhi Wilaya ya Mafia.



Mahojiano na wananchi kisiwa cha Jibondo:

Modewjiblog imeweza kufanya mahojiano kadhaa na wananchi wa kisiwa cha Jibondo ambapo wameweza kueleza kuwa kisiwa hicho kimeanza kulika katika baadhi ya maeneo kwani kwa sasa maji yameweza kuingia katika ardhi.

Kwa mujibu wa wakazi wa Jibondo ambapo maana ya jina hilo ni jiwe kubwa na ndivyo kilivyo kisiwa hicho, kwani kipo juu ya mwamba mkubwa kwa sasa baadhi ya maeneo maji ya bahari yameingia baharini.

Zahoro Swed mkazi wa Jibondo amemweleza mwandishi wa habari hizi kuwa, awali katika eneo wanaposhushia vyombo vya usafiri lilikuwa mbali na majini, lakini sasa eneo hilo limemezwa na maji yamesogea zaidi.

“Wasiwasi wetu ni ujaaji wa maji. Zamani vyombo vyetu tulikuwa tunapaki eneo la nyuma kabisa, lakini sasa tunasogea hadi huku mbele haya ni mabadiliko na hali ikizidi hivi basi tutakuja kushuhudia maji yakiingia katika makazi ya watu” alibainisha Swed alipozungumza na Modewjiblog katika kisiwa hicho cha Jibondo.

Aidha, kwa upande wao baadhi ya wananchi wa eneo hilo la jibondo wamebainisha kuwa, kutokana na suala la uvuvi kushamiri wapo wavuvi wasio waaminifu wanaotumia mabomu kiasi cha kuharibu mazingira ya bahari hata kupelekea kisiwa hicho kupata matatizo ya maji kuingia kwenye ardhi.

Wakazi hao wameeleza kuwa, elimu ndogo ndio chanzo cha wavuvi hao kuendelea kutumia mabomu kufanya shughuli zao za uvuvi haramu ambapo mabomu hayo yanapelekea kisiwa hicho ambacho ni cha miamba ama jiwe (Mafiwe) kuathirika zaidi huku Mabadiliko ya tabianchi yakipata nafasi ya kuongeza uharibifu huo.



Kisiwa cha Chole:

Kwa upande wa wananchi wa kisiwa cha Chole ambacho ni kisiwa kidogo na ndio kisiwa chenye utalii na urithi wa kale ikiwemo magofu na majumba ya zamani, wananchi wengi wa kisiwa hicho wamelalamikia juu ya elimu ndogo ya Mazingira kutolewa licha ya kuihitaji mara kwa mara.

Wakazi hao wa kisiwa hicho walipaza sauti kwa kueleza kuwa, wengi wao wanajishughulisha na shughuli za baharini ikiwemo uvuvi na suala la kilimo cha mwani ambapo wamekuwa wakishuhudia matatizo ya kimazingira yanayotokea baharini mara kwa mara.

Swaumu Mohammed ambaye ni mkazi wa kisiwa hicho cha Chole anayefanya shughuli za kilimo cha zao la mwani anaeleza kuwa wamekuwa wakishuhudia mabadiliko kadhaa ndani ya bahari hiyo ikiwemo baadhi ya maeneo kuwa tofauti na awali.

“Maji yamekuwa yakiongezeka mara mbili zaidi. Wakati mwingine tunapofika kuvua mwani hapa kipindi cha nyuma maji yalikuwa ni ya kiasi, lakini kuna wakati hali hiyo inakuwa haipo kabisa na maji yanakuwa ni mengi zaidi na hata kutupa hofu.

Hivyo elimu zaidi inahitajika katika kujua mabadiliko ya tabianchi ni yapi na namna ya kujikinga nayo hasa sisi tunaoshinda baharini muda mrefu” alieleza Bi. Swaumu alipoulizwa kama anafahamu juu ya hali ya mabadiliko ya tabianchi ama .

Mbali na wananchi wa visiwa hivyo, kwa upande wa wananchi wa Kisiwa cha Bwejuu kwa upande wao wameonyesha wasiwasi wao kuwa baadhi ya maeneo yanayozunguka kisiwa hicho yamekuwa yakiliwa na maji kwa muda mrefu huku kukiwa hakuna juhudi za haraka kunusuru hali hiyo.

Wananchi hao wameonyeshwa kusikitishwa na kasi ya hali hiyo kwani imekuwa ikiongezeka mara kwa mara na hakuna hatua ya haraka iliyochukuliwa.

“Kwa kawaida ukiwa unatoka sehemu moja ama nyingine hali hii hutoiona kwa harakaharaka. Ila kwa sie tuliozoea ndio tunajua kama ardhi imeliwa na bahari” anaeleza mmoja wa wavuvi anayefanya shughuli zake katika eneo la kisiwa hicho aliyefahamika kwa jina la Salum Mwinyikame.

Aidha, Mwinyikame ameongeza kuwa, kisiwa hicho ambacho ni asili ya mchanga. Kimekuwa kikipata changomoto nyingi ya kimazingira huku akiomba mamlaka husika kufika na kutoa elimu hiyo ya mazingira.

Hata hivyo, Modewjiblog ilipowasiliana na viongozi wa Serikali wa Kisiwa hicho cha Mafia, wamebainisha kuwa, karibu visiwa vyote vinavyokaliwa na watu wamekuwa wakijitahidi kufikisha elimu mbalimbali huku akisisitiza wito wa wadau binafsi kujitokeza kusaidia na serikali katika swala hilo la utoaji wa elimu ya Mazingira na mabadiliko ya tabianchi hasa katika kukabiliana na majanga yatokanayo na masuala hayo.


Moja ya vyombo vya uvuvi na usafirishaji abiria vikiwa vimepaki katika fukwe za Kisiwa cha Chole huku vikisubiria maji kurejea katika eneo hilo kama vilivyokutwa na mwandishi wa makala haya. (Andrew Chale).



Pichani ni katika eneo la Fukwe za Wavuvi kama linavyoonekana lilivyoharibika kulikosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo la Kilindoni wameeleza kuwa, miaka ya nyuma hapo palikuwa na minazi huku maji ya bahari yakiwa mbali, lakini kwa kadri mabadiliko yalivyotokea, eneo hilo limeweza kuliwa na kufanya minazi kupotea hali iliyosababisha kuweka mfereji/mto mdogo ambao unapitisha maji kutoka baharini na kuchanganyika na yale ya mvua ya kwenye makazi ya watu. (Picha na Andrew Chale)


Taswira ya kisiwa cha Chole kinavyoonekana..


Baadhi ya fukwe za kupendeza za kisiwani Mafia zinavyookena kwa picha hii iliyopigwa juu

eneo la Mafia.. 


Moja ya sehemu za eneo la Kisiwa cha Jibondo kama inavyoonekana pichani ambapo kisiwa hicho kipo juu ya mwamba ama jiwe kama inavyofahamika Jibondo ama jiwe kubwa. (Picha ya kwa hisani ya Mafia Island page ya fb).


Pichani Mwandishi wa Makala haya akiwa katika boto maalum kwa safari za visiwa vilivyo ndani ya Mafia ambavyo Kisiwa hicho kinakadiliwa kuwa na Visiwa vidogovidogo zaidi ya vitano. Picha ya chini Mwandishi akiwa katika Kibao cha Shule ya Kijiji cha Chole katika Kisiwa cha Chole ambacho ni kisiwa pekee chenye magofu ya Kale na vitu vya thamani vya enzi za zamani vikiwa vimehifadhiwa huko.


Kisiwa cha Chole


Moja ya visiwa vidogo na vya kuvutia ndani ya Kisiwa cha Mafia.






WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...