MWENYIKITI wa kijiji cha Nduli, Ayubu Mwenda amedai kuwa Diwani wa kata mpya ya Nduli iliyopo Manispaa ya Iringa amekuwa akimtishia kumwondoa madarakani na pia kumnyang’anya ardhi na kuikabidhi kwa serikali ya kijiji kutokana na chuki za kisiasa.
Chuki zilizotokana na wote kuomba kuteuliwa katika kura za maoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi ya Udiwani kwenye kata hiyo ambapo mwenyekiti huyo hakubahatika kupata nafasi na kukata rufaa ya kupinga matokeo ya kura za maoni lakini rufaa yake ilikataliwa na Idd Chonanga kupita kuwania udiwani.
Mwenda amedai kuwa vitisho hivyo alianza kuvitoa mara baada ya kupita kwenye kura za maoni pamoja na kwenye kampeni ya kujinadi kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu (Oktoba 31, 2010).
“Pamoja na kuwa kampeni meneja wa CCM wa kata ya Nduli lakini nimeonekana kuwa mpinzani kwake kwani alihisi kutokana na kushindwa kwangu ningesaidia vyama vya upinzani dhana ambayo si kweli kwa kuwa mimi ni kada wa CCM” alisema Mwenda.
Alisema mbali na yeye kupata vitisho vya kuondolewa madarakani mara baada ya kupita kwenye kinyang’anyiro cha Udiwani, diwani huyo pia alisema atahakikisha eneo analolimiliki linalokadiriwa kuwa na ekari 60 kumnyang’anya na kulikabidhi serikali ya kijiji ili lijengwe sekondari ya kata kwa lengo la kumkomesha.
“Eneo hilo lilikuwa mali ya baba yangu mzazi Abdallah Athumani Mwenda……..ambalo awali kabla ya kumiliki baba lilikuwa mashamba ya Wagiriki ambalo walikuwa akilima tumbaku na baadaye wagiriki kuondoka na kumwachia baba ambaye alikuwa akifanya kazi kwao” alisema mweyekiti huyo wa kijiji cha Nduli.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nduli, Idd Chonanga alidai tuhuma hizo alizozitoa mwenyekiti huyo si za kweli hajawahi kusema labda ni kwa vile walikuwa wakichuana katika kura za maoni za CCM hivyo anahisi atamfanyia hivyo.
“Serikali ya kijiji ndiyo yenye mamlaka ya kumnyang’anya mkazi ardhi na kuimiliki na kuamua eneoe hilo litumike kwa shughuli zipi, hivyo mimi siwezi kumnyang’anya eneo hilo ” alisema Diwani Chonanga.
Aidha kwa upande wake Mohamed Mwenda (kaka yake Ayubu) alidai kuwa hajawahi kusikia eneo hilo kutaka kuchukuliwa na kukabidhiwa kwa serikali ya kijiji na kudai kuwa eneo hilo lenye jumla ya ekari 159 lilimilikishwa kwa mjukuu wa baba aitwae Ahamadi Mzola kwa kushirikiana na mimi (Mohamed Mwenda) kupitia wosia aliouandika Abdallah Athumani Mwenda.
Naye Afisa mtendaji wa kata ya Nduli, Hamid Mfalingundi alisema anamshangaa mwenyekiti huyo kwa kudai kunyang’anywa eneo ili lijengwe sekondari ya kata mbali na kufahamu kuwa tayari kikao kilishaamua eneo la kujenga sekondari ya kata na yeye alishiriki katika kikao hicho.
Mfalingulindi alisema makubaliano ya kujenga sekondari kwenye kikao hicho yalikuwa ni kitongoji cha Kisowele ambacho kipo kati kati ya kijiji cha Mgongo, Nduli na Kigonzile.
Thursday, 11 November 2010
TANGA BATHING CLUB BEACH
Mzee Rashid Abubakari Mokiwa (Kulia) akibadilishana mawazo na mmiliki wa blog hii Bw. Friday Simbaya alipotembelea 'Tanga bathing Club' jijini Tanga leo, huku 'Kisiwa cha Tanga' kikionekana kwa mbaaaali katika Bahari ya Hindi. Mzee Mokiwa ni moja ya wahudumu wa club hiyo kwa muda mrefu sana na mwenye historia nzuri ya mahala hapa tangu enzi za wajerumani hadi leo. Ijulikane kuwa wazee kama hawa ni hazina kubwa kwa taifa letu. 'Kitunze kidumu'
MARALIA INAKUBALIKI KWA MTINDO HUU?!
Matumizi mabaya ya vyandarua haya hapa, badala ya kutundikwa Vitandani ili kujikinga na mbuu sasa vyatumika kuvulia dagaa na samaki, kama watoto wadogo alivyokutwa wa kitumia chandarua cha 'Malaria Hakubaliki' wakivulia samaki katika bahari ya Hindi maeneo ya 'Tanga bathing Club Beach' karibu na Kisiwa cha Tanga jijini Tanga mchana leo. (PICHA. FRIDAY SIMBAYA)
CHAVITA YAOMBA SERIKALI KUBORESHA MAISHA YA WALEMAVU
CHAMA cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mkoa wa Iringa chaiomba serikali kuboresha mazingira na maisha ya watu wenye ulemavu nchini za kupata huduma za elimu, afya na usalama wa raia kama watu wengine.
Mwenyekiti wa CHAVITA Mkoa wa Iringa Zawadi Sumani alisema jana katika warsha ya ushawishi na utetezi kwa watendaji wa idara za serikali na viongozi wa serikali za mitaa Mkoa wa Iringa, kuwa watu wenye ulemavu ni waathirika wakubwa wa umaskini na UKIMWI hapa nchini kutokana na mitazamo potofu ya jamii inayoizunguka.
Alisema kuwa huduma na sheria mbalimbalinzilizopo hapa nchini hazikidhi maitaji ya watu wenye ulemavu na wemekuwa wakiacwa nyuma katika mchakato mzima wa maendeleo ya taifa ingawa zipo jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata huduma za elimu, afya na usalama wa raia.
Lakini bado inaelekeza dhana kuwa mtu mwenye ulemavu anastahili kuishi maisha tegemezi ambapo dhana hii ina kwenda kinyume na tamko la umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu na azimio kuhusu fursa sawa na ushirikishaji wa watu wenye ulemavu la mwaka 1983.
Lengo mahususi la warsha iyo ilikuwa ni kuwapatia mwako watendaji kutoka idara mbalimbali kama polisi watendaji wa mahospitali na uongozi wa serikali za mitaa kutoka ngazi ya Mkoa hadi wilaya kutambua umuhimu wa ushiriki wao katika kufanyikisha mchakato wa uimarishaji wa sera na sheria za watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya mtaa, kata, tarafa hadi wilaya.
Aidha, alisema kuwa serikali hivi sasa inatekeleza awamu ya pili ya mpango wa miaka mine wa kuondoa umaskini, maarufu kama mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA, mpango huu pamoja na mambo mengine unatambua wenye ulemavu.
Warsha ya utetezi na ushawishi kwa watendaji idara mbalimbali uliaandaliwa na CHAVITA kwa kushirikiana na shirika la ‘The Foundation for Civil Society’ kwa kutoa ruzuku ambayo imefanyikisha uendashaji wa warsha ya siku nne.
Mkoa wa Iringa una kadiriwa kuwa na idadi ya walemavu wasiosikia yaani viziwi zaidi ya 2,000 wanaotabulika na chama cha viziwi Tanzania Mkoa wa Iringa.
Kwa upande wake, Mgeni Rasmi Kaimu Mkuu Mkoa wa Iringa Kapteni mstaafu Aseri Msangi, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa alisema serikali ipo bega kwa bega kuhakikisha watu wenye ulemavu hasa viziwi wanaendelea kuimarishwa kwa misingi ya kuboresha hali za maisha yao.
Alisema kuwa Chama cha tawala (CCM) kwa kuboresha ilani ya uchaguzi imeangalia mahitaji ya watu wenye ulemavu kwa kuwawekea mikakati mabalimbali ya maendeleo ya taifa, mikakati hii itasaidia sana katika kuwakomboa watu wenye ulemavu kwenye umaskini na majanga mbalimbali yanayokithiri miongoni mwa jamii ya watu wenye ulemavu hapa nchini.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kapteni (mstaafu) Aseri Msingi mwenye Kaunda suti ya bluu kutoka kushoto mstali wa mbele ya watu walioketi akiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) na washiriki wa warsha ya siku nne ya ushawishi na utetezi kwa watendaji wa idara za serikali na viongozi wa serikali za mitaa Mkoa wa Iringa jana. (PICHA. FRIDAY SIMBAYA)

Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...