Monday, 15 August 2011

HII NDIO HALI HALISI YA USAFIRISHAJI WA NYAMA MJINI LUDEWA

Wakazi wa Mjini Ludewa mkoani Iringa wakisafirisha nyama  kwa kutumia
mkokoteni kutoka Machinjio ya Ibani kwenda mabuchani kwa ajili ya
walaji kuweza kununua nyama hiyo jana.

VIONGOZI WA DINI MBALIMBALI LUDEWA WAPATA MAFUNZO JUU YA AFYA YA UZAZI NA MTOTO

Ludewa


ZAIDI YA VIONGOZI 53 wa dini mbalimbali wanawake kwa wanaume kutoka katika maeneo mbalimbali wilayani Ludewa, Mkoa Iringa wamehudhuria mafunzo ya siku tatu kuhusu Afya ya uzazi na mtoto.
Shirika lisilokuwa la kiserikali la IMA WORLD HEATH la jijini Dar es Salaam limetoa mafunzo hayo maalum kupitia mradi wa Maisha Program uliofadhiliwa na shirika la maendeleo la kimataifa la watu wa marekani USAID.
Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Mratibu wa mradi huo  Bw Joel Lubebe alieleza kuwa sababu ya kuwapa elimu hii viongozi wa dini mbalimbali ni kutokana na viongozi hao kuaminiwa na jamii, pia jamii kuwa tayari kupokea maagizo na mafundisho yao sanjari na ushawishi na vipawa walivyopewa na Mungu mwenyewe.
Bw Lubebe alisema mradi wa Maisha Program unalenga kupunguza vifo vya uzazi vinavyotokana na sababu za moja kwa moja kama kutokwa damu kupita kiasi kwa wajawazito baada ya kujifungua pia kupunguza vifo vya watoto wachanga na kupunguza kiwango cha watoto waliozaliwa na uzito pungufu kwa kuhakikisha akina mama wanatibiwa Malaria mapema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bi Hilda Lauo katika hotuba yake kwa washiriki wa mafunzo hayo alisema Tanzania imeandaa mpango mkakati wa kitaifa wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya uzazi na mtoto kufikia robo tatu ¾ na 2/3 kwa vifo vya watoto ifikapo 2015.
Bi Lauo aliongeza kuwa mkakati huu unatoa fursa kwa wadau wote katika miradi yote kusisitiza katika maeneo mawili, utoaji wa huduma katika vituo, na huduma ya Afya ya jamii ili kufikia malengo ya mpango wa Taifa wa kupunguza umaskini na kuongeza uchumi Tanzania (MKUKUTA) na mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi( MAAM).
Kwa upande wake Bi Velonica Mkusa mwezeshaji kutoka Ima World Heath alisema mradi umelenga kuwafundisha viongozi wa dini ili watumie miongozo yao kuhusu afya ya uzazi na mtoto katika kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.
Mkusa alisema tatizo la vifo vitokanavyo na uzazi kwa akina mama na watoto ni kubwa kwani kati ya akina mama 100,000 watakaojifungua watoto hai 454 wanafariki dunia sababu ya uzazi na kuongeza kuwa kuna umuhimu kwa akina mama kuwahi cliniki mapema anapohisi ujauzito kwani husaidia kupata msaada mapema.
Naye Mratibu wa hudum za Afya ya uzazi na mtoto wilayani Ludewa Bi Imelda Mtemi (Mama Mnyagala) akitoa takwimu ya Wilaya yake alisema mwaka 2008 akina mama 139 walifariki dunia kutokana na vizazi hai 100,000 ambapo mwaka 2009 akina mama 85 walifariki na  2010 akina mama 108 walifariki dunia kutokana na vizazi hai 100,000.
Bi Mnyagala Mtemi aliongeza kuwa vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja (IMR) mwaka 2008 vifo 26 vilitokea ambapo mwaka 2009 ilikuwa 25/1000 na mwaka 2010 vifo 25 kwa 1000 vilitokea.
Aliongeza kuwa akina mama waliojifungua katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa mwaka 2008 ilikuwa asilimia 67 ambapo 2009 ilifikia asilimia 68 na mwaka 2010 ilifikia asilimia 69 na akina mama wanaojiunga na cliniki kabla ya miezi minne ya ujuzito mwaka 2008 ilifikia asilimia 68 ambapo mwaka 2009 ilishuka na kufikia asilimia 58 na mwaka jana ilifikia asilimia 59.
Hata hivyo, Mtemi alisema anakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo uelewa mdogo wa jamii katika kufanya maamuzi ya haraka juu ya kuwawahisha hospitali akina mama wenye matatizo ya uzazi, uelewa mdogo juu ya akujiunga na cliniki kabla ya miezi minne, juu ya lishe kwa wajawazito na muda wa kupumzika sanjari na kutumia dawa za Malaria kwa mjamzito
Akifunga mafunzo hayo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Dr. Happenes Ndosi aliwashukuru wawezeshaji kutoka shirika la Ima World Heath kwa mafunzo hayo na kuwataka washiriki hao viongozi wa dini mbalimbali kufikisha elimu waliyoipata kwa waumini wao ili kupunguza vifo vya uzazi na mtoto wilayani mwake.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...