Tuesday, 24 April 2018

Uchukuzi, Tanesco soka zakaribia nusu fainali


Mchezaji Erick Mpunga wa Uchukuzi (kulia) akijaribu kuzuia mpira unaotaka kupigwa na Kassim Mdee wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAO) katika mchezo wa mpira wa miguu wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).



IRINGA: TIMU za soka za Uchukuzi na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zilizopo kundi ‘A’ na ‘B’ zinakaribia kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mei Mosi baada ya jana kushinda michezo ya iliyofanyika kwenye uwanja wa Samora, ambapo kila mmoja zinaongoza kundi lake kwa kujikusanyia pointi sita. 

Uchukuzi inafuatiwa na mabingwa watetezi Geita Gold Mine (GGM) wenye pointi mbili, NAO na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yenye pointi moja kila mmoja; wakati Tanesco inafuatiwa na Tumbaku nayo inapointi sita lakini imezidiwa magoli ya kufunga, huku RAS Iringa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa hawana pointi. 

Katika mechi hizo za jana Uchukuzi waliwafunga Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAO) kwa magoli 3-1. Nao ndio walikuwa wa kwanza kupachika bao katika dakika ya 45 kupitia kwa Peter Dihoko aliyeunganisha kona ya George Mlelwa. 

Uchukuzi walisawazisha katika dakika ya 60 kupitia wa Kado Nyoni, huku bao la pili lilifungwa na Omary Kitambo dakika ya 63 na bao la tatu dakika ya 68 lililofungwa na Issack Ibrahim. 

Nao Tanesco waliwachapa RAS Iringa kwa magoli 4-0, ambapo matatu yaliyofungwa na Kurwa Mangara katika dakika ya 19, 34 na 59 huku Salehe Bakari alifunga bao la nne dakika ya 66. 

Katika mchezo wa netiboli timu ya RAS Iringa iliwafunga Tanesco kwa magoli 27-14. Washindi walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 9-7. Nayo Ikulu walipewa ushindi wa mezani wa magoki 40 na pointi mbili baada ya Malaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kushindwa kufika uwanjani Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCU) kwa kuwa na majeruhi wengi waliotokana na kuvuta kamba. 

Katika mchezo wa kuvuta kamba kwa wanawake timu ya Uchukuzi ilivutwa na RAS Iringa 1-0 baada ya mvuto wa awali kutoka sare; huku kwa upande wa wanaume wa Uchukuzi waliwavuta Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAO) kwa mivuto 2-0. 


Wachezaji wa timu ya wanawake ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kulia wakiongozwa na Neema Mbuja wakiwavuta wenzao wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) jana kwenye michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika uwanja wa Samora. Tanesco walishinda kwa mivuto 2-0. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).


Michezo mingine ya kamba wanawake walivutwa na MUHAS mivuto 2-0; nayo NAO waliwavuta Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mvuto 1-0 kwa upande wa wanaume. 

Michuano hiyo inaendelea leo kwa upande wa netiboli timu ya Uchukuzi itacheza na RAS Iringa uwanja wa RUCU; huku katika soka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro watgakuna na Tumbaku ya Morogoro, na GGM watacheza na Uchukuzi kwenye uwanja wa Samora; wakati katika kamba RAS Iringa kuumana na Tanesco kwa wanawake. 


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...