Na Friday Simbaya, Songea
Mwenyekiti wa Kamati ya waratibu wa Mashindino ya Kombe la Ansgari
2013, Emeran Ndunguru akisoma taarifa ya maamuzi yao kuhusu kufutwa
kwa michezo ya mpira ya miguu kwa mshindi wa tatu na fainali leo.
Kamati ya mashindano ya Kombe la Pasaka (Ansgar Cup) Tarafa ya Ruvuma,
Wilaya Songea (V) mkoani Ruvuma hatimaye imefuta fanaili michezo ya
mpira wa miguu kwa mshindi wa tatu na fanaili kwa mwaka huu kutokana
na malumbano yanayoendelea kati ya timu za Kilagano na Peramiho B,
yaliyoanza wakati nusu fainali.
Akiongea na waandishi wa habari leo (Alhamisi) mwenyekiti wa kamati,
Emeran Ndunguru alisema, malumbano hayo yamepelekia kufutwa kwa
fanaili hizo michezo wa mpira wa miguu ni kati ya timu ya Kilagano na
Peramiho B, ambapo Kilagano walidai kuwa timu ya Peramiho B
ilichezesha baadhi ya wachezaji ambao ni mamluki l wakati wa mchezo
ya nusu fanaili uliyofanyika katika Uwanja wa Nanenane, Kijiji cha
Mgazini katika Kata ya Kilagano wilayani Songea.
Emeran Ndunguru anayefanya kazi ya ufadhili pamoja na kamati yake
badala ya mfadhili Dr. Ansgar Stuffe, alisema michezo ya mpira wa
miguu kwa mshindi wa tatu na fainali imefutwa ili kuwapa nafasi zaidi
kuendelea na malumbano hadi ukweli ujulikane.
Alisema kuwa wakati vilabu hivyo vya mpira wa miguu vikiendelea
kulumbana, fainali za mpira wa pete (Netball) na mshindi wa tatu
zitafanyika tarehe 16.06.2013 siku ya Jumapili katika Uwanja wa Ansgar
Peramiho.
Mfadhili wa Kombe la Ansgar ni Dr. Ansgar Stuffe OSB, mkurugenzi wa
Hospitali ya Peramiho aliamua kuwepo na michezo katika vijiji vya
Peramiho, shule za msingi za Peramiho na baadaye michezo ilipanuka
hadi tarafa ya Ruvuma.
“Michezo hii imechezwa kwa mafanikio zaidi ya miaka kumi na tano (15),
na ushindi umekuwa wa kupokezezana kata hadi kata hapakutokea usumbufu
kama huu wa kulumbana kati ya vilabu na vyama vya michezo yaani SORUFA
na FARU. Kama waratibu chini ya mfadhili hatuelewi nguvu ya malumbano
hayo yanatoka wapi!,” alishangaa Ndunguru.
Mwaka huu michezo ilianaza kwa ushindani mkali huko Kata ya Kilagano,
ambapo mashindano hayo yanashirikisha kata za Mpandangindo, Peramiho
,Litisha na Kilagano (wenyeji), tarafa ya Ruvuma wilayani Songea
Vijijini.
Mashindano haya yanadhaminiwa na Dr. Ansgar Stuffe OSB, Mkurugenzi wa
Hospitali ya Peramiho ambayo yalianza tarehe 21.04.2013 na
yalitarajiwa kuamalizika Siku ya Ekaristi Takatifu mnamo tarehe
02.06.2013.
Mashindino ya Kombe la Pasaka (Ansigar Cup) Tarafa ya Ruvuma (Soka na
Pete) yanafanyika kwa mara ya kwanza katika Kata ya Kilagano katika
Kijiji cha Mgazini, ambapo miaka yote mashindano hayo yalikuwa
yanafanyika katika kata ya Peramiho.