Tanzania ina ungana na dunia kusherehekea siku ya kuzaliwa mkombozi wa ulimwengu. Hapa ndipo mtoto Yesu alipozaliwa katika zizi la ng'ombe Bethlehemu.
Kutoka kushoto kwenda kulia ni Kris Simbaya (Jr) na Ken Simbaya (Jr) wakiwa katika pozi ya picha maeneo ya Peramiho Songea, Mkoa wa Ruvuma.
Kutoka kushoto kwenda kulia ni Friday Simbaya, Kris Simbaya, Ken Simbaya na Lina Changwa wakiwa katika picha ya pamoja siku ya Krismas.
Mama Simbaya ambaye ni mke mpendwa wa mmiliki wa blog hii akiwa na watoto wake walipokuwa wa kisherekea siku kuu ya Krismas leo jioni.
Saturday, 25 December 2010
ZAWADI YA MKESHA WA NOELI
Muuguzi wa Zamu wa St. Joseph's Mission Hospital Peramiho akiwa anawaangalia watoto ambao walizaliwa kabla ya umri yaani 'Premature babies' katika Chumba cha Joto 'Premature Unit or Incubator Room' Jumamosi kuangalia kama wanaendelea vizuri lakini hawakuzaliwa kwenye Mkesha wa Krismasi wako wanne.
Na Friday Simbaya,
Peramiho
JUMLA ya watoto 13 wamezaliwa, wakiwemo wakike tisa na wakiume wanne katika Hospitali ya Mission ya Mtakatifu Joseph Peramiho mkoani Ruvuma katika Mkesha wa Noeli (Krismasi) usiku wa kuamkia LEO.
Akiongea na BLOG HII, Muuguzi wa Zamu (Nursing Office in charge), Bi. Sirah Nchimbi alisema kwamba watoto wote walizaliwa kwa njia ya kawaida isipokuwa watoto watatu ndiyo waliozaliwa kwa njia ya upasuaji (surgical operation) lakini hali zao zinaendelea vizuri pamoja na mama zao.
“Watoto hao walizaliwa na uzito wa kawaida, hali zao zinaendelea vizuri sana pamoja mama zao. Wakina mama wengine wameruhusiwa baada ya kujifungua lakini wamebaki wale walioji fungua kwa opresheni ambao wako katika uangalizi maalumu,” alisema muunguzi wa zamu.
Aidha, alisema kuwa yapo matatizo wanayokubiliana nayo kama vile kina mama kutofika mapema hospitalini pindi wapatapo uchungu wa uzazi kunako sababisha wengi wao kinamama kujifungulia njiani kabla ya kufika hosptali na wengi wao hujifungua watoto waliokufa katokana na kuchelewa kufika hospitali mapema.
Tatizo jingine ni kwamba wa kinamama walio wengi maeneo haya hutumia dawa ya mitishamba kuongeza uchungu wa kujifungua kabla ya kuletwa hospitali, matokeo yake wengi wao kina mama wanashindwa kujifungua kwa njia ya kawaida (normal delivery) au hujifungua watoto waliokufa kutokana na dawa hizo wanazozitumia.
“Yaani ni tatizo kubwa sana kwa kina mama wanaokuja kujifungua hapa kutokana kutumia dawa za kienyeji za uchungu lakini huwatunawapa elimu wanapofika na kuwapa ushauri wakina mama wajawazito waweze kufika hospitalini mapema na kuacha kutumia dawa hizo za kuongeza uchungu, ambapo mara nyingi hutiwa kwenye chain a uji,” alisema muunguzi huyo wa zamu.
Lakini pamoja na hayo, hakuweza kuelezea ni dawa ya aina gani mara nyingi wa kina mama hao hutumia kama dawa ya kuongeza uchungu, na kuongeza kuwa wanatumia mizizi Fulani Fulani ambayo hakutaja aina gani ya mizizi hiyo.
Mwisho
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
Habari ndugu msomaji wetu wa blog, Natumaini unaendelea vyema. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vit...