Monday, 7 December 2015

WAFANYAKAZI WA BARABARA MAFINGA WAGOMA KUDAI STAHIKI ZAO...!




Tukio lililotoka kujili mda si mrefu hapa Mjini Mafinga, hawa ni wafanyakazi wa kampuni ya kichina ambayo inaitwa ccce inayojenga kipande cha barabra kuanzia Mafinga Hosptal mpaka Nyololo kwa kiwango cha lami. wafanyakazi hawa wamegoma kwa siku ya pili leo wakadai stahiki zao, ikiwa ni pamoja na mikataba yao ya kazi, kiwango duni cha mishahara yao pamoja na ukosefu wa sera za usalama mahala pa kazi, nilikuwa nikipita eneo hili jioni nikitokea jijini Mbeya, watu hawa waliona na kunisihii niambatane nao kusikiliza kero zao.......



MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA



Hawa ni baadhi ya vikundi vya washiriki wa semina ya majadiliano ya namna ya ushiriki wa jamii katika kupinga ukatili wa kijinsia wakiwa katika tafakari leo mjini Iringa. Semina hiyo imewezeshwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Engender-Health chini ya ufadhili wa serikali ya watu wa marekani kupitia USAID.



Mmoja ya wawezeshaji kutoka UZIKWASA- Pangani, Tanga Joseph Peniel ambaye ni programu meneja wa mawasiliano na kujenga mahusiano akiendesha semina ya majadiliano ya namna ya ushiriki wa jamii katika kupinga ukatili wa kijinsia kwa washiriki wasemina ambao ni watendaji wa kata, mtaa, wanasheria na wanaharakati.


Wawezeshaji wa UZIKWASA -Pangani Tanga Novatus Urassa ambaye pia ni Programu Meneja wa Jinsia na uongozi wenye Mabadiliko na Joseph Peniel ambaye pia ni Programu Meneja Mawasiliano na Kujenga Mahusiano kwa pamoja wakibandika karatasi zenye masuali kuhusu filamu ya AISHA, filamu hii  ni kwa heshima ya wanawake wote waliowahi kubakwa na kwamba baada ya mkasa huo waliochukua hatua gani.






Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwa katika igizo la kusikiliza na kusikia baada ya kuangalia filamu ya AISHA. AISHA, mwanamke mfanyabiashara mwenye matamanio ya mafankio anayeishi mjini anarudi kijijini kwao kuhudhuria harusi ya mdogo wake. wakati anajikumbusha maisha yake ya zamani, na kukutana na familia yake na marafiki, kunatokea mkasa wa kubakwa wenye athari kubwa katika maisha yake. AISHA anaamua kupambana nao vikali ili kupata haki yake.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...