KWA HISANI YAMJENGWABLOG.COM
Sunday, 27 April 2014
Ukawa wapata pigo
'Bunge Maalumu la Katiba, jana liliridhia azimio la kuzifanyia marekebisho kanuni zake saba bila kuwapo kwa wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambao wamesusia Bunge hilo.
MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR YAFANA
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi
katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.Rais Banda kwa sasa ndiye
mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC.(PICHA:FREDDY MARO)
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Jakaya Mrisho
Kikwete akiingia kwenye uwanja wa Uhuru kuwaongoza watanzania katika
maadhinimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kila mwaka
Aprili 26 kusherehekea muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili mwaka
1964 watanzania wengi wamejitokeza katika maadhimisho hayo wakiwemo
viongozi mbalimbali na marais wa nchi mbalimbali za Afrika na
wawakilishi wa nchi mbalimbali pia katika mataifa mbalimbali ya Ulaya,
Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Yoweri Mseveni wa Uganda katikati nI
King Mswati wa Swaziland na kushoto ni Rais Piere Nkurunzinza wa
Burundi.
Kikosi
cha Makomandoo kikionyesha ukakamavu na kuonyesha uwezo wake katika
mapambano ya Karatee na mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete.
‘Ushirikina’ Wakwamisha Mapambano ya Mimba kwa Wanafunzi Mbeya Vijijini
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Usoha Njiapanda iliyopo Mbeya Vijijini.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, , Willson Mwamunyila (katikati)
akizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini kwake.
Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Usoha Njiapanda wakiwa katika mkutano na mwanahabari hizi.
VITISHO
na hofu ya vitendo vya ushirikina imebainika kuwa vikwanzo vya mapambano
ya baadhi ya watu wanaowatia mimba wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari katika Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini, mkoani Mbeya.
(CCM) kimepanga mkakati wa kuengua wataka urais wanaume
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga mkakati mpya wa kuengua wataka urais
wanaume kwa kuingiza hisia za kijinsia kama walivyofanya kumdhibiti
aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta, alipotaka kugombea tena
nafasi hiyo mwaka 2010.
Wachunguzi
wa masuala ya kisiasa wameliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa mkakati
huo unalenga zaidi kumng'oa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ambaye
anaonekana tishio kwa wenzake wanaotajwa kutaka urais.
Kwa
mkakati huo, kundi la wana CCM walio karibu na Rais Jakaya Kikwete,
wameanza kuzungumzia jinsi ya kumpitisha Dk. Asha-Rose Migiro agombee
urais katika uchaguzi mkuu ujao 2015.
WAZIRI WA ARDHI PROF.TIBAIJUKA AKUTANA NA WAZIRI MAMBO YA NJE YA USHELISHELI FAURE
Katibu
wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure (Kulia)
akitia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka jijini Dar
es Salaam kwa mazungumzo.Kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje
ya Tanzania.
Katibu
wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure (Kulia)
akizungumza na Wazirii wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof.
Anna Tibaijuka (Kushoto) wakati alipotembelea Wizara hiyo jijini Dar es
Salaam.Pembeni yao ni Maafisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Mambo ya Nje.
Wazirii
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka
akizungumza (Kushoto) wakati Katibu wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Ushelisheli, Barry Faure (Kulia) wakati alipotembelea Wizara hiyo
jijini Dar es Salaam.Pembeni yao ni Maafisa kutoka Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Mambo ya Nje.Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO (FS)
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
Habari ndugu msomaji wetu wa blog, Natumaini unaendelea vyema. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vit...