Wednesday, 4 January 2017
KIGOMA SISTERS FC YAIBAMIZA PANAMA FC YA IRINGA 2-1
Kigoma Sister FC ya Kigoma (jezi la bluu) yaichapa Panama FC ya Iringa bao 2-1 katika mechi iliochezwa katika Uwanja wa Kumbukumbu wa Samora mjini Iringa leo, katika Ligi ya Wanawake inayoendelea nchini .
Katika kipindi cha kwanza timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufanya goli 1-1, lakini katika kipindi cha pili upepo ulibadilika kwa timu ya Kigoma Sister kuongeza goli la pili.
Timu zingine zinazoshiriki ligi hiyo ni Viva Queens ya Mtwara, Fair Play FC (Tanga), Mlandizi Queens (Pwani), Marshi Academy (Mwanza) na Baobao Queens (Singida).
Zingine ni JKT Queens (Bukoba), Mburahati Queens na Evergreen Queens zote za jijini Dar es Salaam.
Chama cha soka la wanawake Tanzania (TWFA)kwa kushirikiana na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kinaendesha ligi hiyo.
LIPULI FC, ‘YATEMBEZA BAKULI’
Baadhi wa wachezaji wa Klabu kongwe ya Lipuli Football Club yenye makazi yake katika Mji wa Iringa wakiwa katika kambi yao iliyopo katika Hoteli ya Sambala mjini Iringa jana. Kushoto ni nahodha wa timu hiyo Ally Sonso, timu hiyo ipo kambini kwa ajili ya mechi yao dhidi ya timu ya Mshikamano ya jijini Dar es Salaam Jumamosi wiki hii.
Duru la Kwanza
Lipuli FC vs African Sports 1-1
Lipuli FC vs Kiluvya 1-0
Lipuli FC vs Pamba 2-0
Mshikamano vs Lipuli 0-1
Polisi vs Lipuli 0-1
Friends Rangers vs Lipuli 3-0
Ashanti vs Lipuli 1-1
Duru la Pili
African Sports vs Lipuli 0-1
Kiluvya vs Lipuli 2-3
Zimebaki timu nne za nyumbani
1. Mshikamano
2. Polisi
3. Ashanti
4. Friends rangers
Na nje mechi moja kule Mwanza kucheza na Pamba,
Timu ya Lipuli ina jumla ya pointi 20.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
Habari ndugu msomaji wetu wa blog, Natumaini unaendelea vyema. Leo tutaanza kujifunza kilimo cha bora cha nyanya, na tutaanza kufahamu vit...