Saturday, 13 February 2016

Hali tete Iringa



Hali tete Iringa: Inakadiriwa kuwa takribani watu 3000 wakiwemo wagonjwa wa kipindupindu wamefungiwa na Maji ya Mto Ruaha Mdogo yaliyohama mkondo wake na kutengeneza njia tofauti tatu. 

Watu hao ambao wengi wao wapo vitongoji tofauti vitatu vya kilimo ya mashamba makubwa ya mpunga Tarafa ya Pawaga Iringa vijijini, hawajala chochote kwa siku pili leo kutokana na kutokuwepo kwa njia ya kuwapelekea chakula kama awali. 

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, Mchana huu amekiri hali hiyo na kueleza kuwa wameomba Helikopter ya Polisi kwa lengo la kwenda kudondosha chakula maeneo hayo ambayo yamegeuka kama bahari baada ya kujaa maji lakini pia kuanza kuwaokoa. 

Amesema Helikopter hiyo itaondoka Dar Es Salaam muda wowote kuanzia sasa, kuja Iringa kwa kazi hiyo.

SACIDS na OHCEA zawakutanisha wataalamu wa Afya kujadili mpango kazi wa pamoja


Dk. Deo Mtasiwa Naibu Katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI akizungumza katika mkutano wa Afya Moja ulioshirikisha wadau mbalimbali wa Afya ya Mifugo, Binadamu na Mimea kutoka katika vyuo mbalimbali hapa nchini.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).

Mhadhiri na mtafiti mtoa huduma katika chuo kikuu cha Sokoine, Profesa Robson Mdogera akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kuhusu mafanikio pamoja na changamoto wanazozipata kwenye mango wa Afya Moja wanapotaka kufanya kazi kwa pamoja kati ya madaktari wa afya ya mifugo, binadamu pamoja na aafya ya Mazingira.



Dk. Kitua kutoka SACIDS akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Wataalamu wa Afya kutoka vyuo mbalimbali hapa nchi ili kujadili nikwa jinsi gani wanaweza kushirikiana katika kufanya kazi bila kuangalia kuegemea upande wowote wa Afya.


Profesa Mamuya kutoka MUHAS akiwasilisha mada kwenye mkutano uliowashirikisha wataalamu mbalimbali wa afya ya mifugo, binadamu pamoja na afya ya mazigira uliofanyika Bagamoyo.

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine kitengo cha Tiba ya Afya ya Jamii Dk. Helena Ngowi akiwasilisha mada mbele wataalamu mbalimbali wa Afya kutoka kwenye vyoa vya hapa nchini waliokuwa wanajidilini kwa jinsi gani wanaweza kushirikiana katika kufanya kazi.

Profesa Rudovick Kazwala kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) akichangia mada kwenye mkutano wa wadau wa Afya moja uliowashirikisha wataalamu mbalimbali wa Afya kutoka vyuo mbalimbali vya Tanzania.


Mhadhiri na mtafiti mtoa huduma katika Chuo Kikuu cha Sokoine, Profesa Robson Mdogera akizungumza jambo walipokuwa wanajadili mpango kazi wa pamoja ili kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kufanya bila kubagua upande wowote.

Profesa Mark Rweyemamu akizungumza jambo wakati wa kuwasilisha mpango kazi wao ili kuweza kuutumia kwa pamoja na kuachana na mpango wa kila kundi.





Makundi ya wataalamu mbalimbali wa Afya Moja wakijadili pamoja na kubuni mpango utakaowasaidia wataalamu wa Afya ya Mifugo, Binadamu pamoja na Mazingira kufanya kazi kwa pamoja yaani Afya Moja.

Profesa Rudovick Kazwala akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasimi aliyefika kufunga mkutano huo.




Picha ya pamoja.














Taasisi za SACIDS na OHCEA wameandaa mkutano uliowakutanisha wataalamu mbalimbali wenye ujuzi tofauti wa Afya hasa Afya ya Mifugo, Afya ya Binadamu pamoja na Afya ya Mazingira kutoka kwenye vyuo mbalimbali vya hapa Tanzania.


Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuweza kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kufanya kazi kwa pamoja bila kubagua upande wowote ili kutatua tatizo lililokuwepo kwa miaka mingi hapa nchini Tanzania hasa pale yanapotokea magonjwa yanayowapata mifugo pamoja na binadamu.


Mgeni rasmi aliyefika katika mkutano huo alikuwa Dk. Deo Mtasiwa ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI ambaye alisema kuwa serikali iko pamoja na wataalamu wa Afya ya Mifugo, Afya ya Binadamu pamoja na Afya ya Mimea.


Pia amesema mpango ulioandaliwa na wataalamu hao wa afya wa kufanya kazi kwa pamoja utachukuliwa na serikali ili kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuutumia ili ikitokea ugonjwa kwa mifugo kwenda kwa binadamu iwe ni rahisi kutatua tatizo hilo.


"Magonjwa ya kuambukia yanayotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu yanaleta changamoto kubwa sana lakini kwa sababu umekuwepo mpango wa Afya mmoja basi utatusaidia na pia tutawatumia wataalamu bila kuangalia yuko kundi gani," alisema Naibu Katibu Mkuu


Pia alisistiza kuwa umoja wao ndio mafanikio yao kwani wasipoungana na kufanya kazi kwa pamoja itakuwa ni vigumu kufikia yale malengo waliyojiwekea. "Napenda kuona mnatoa elimu katika jamii kuhusu magonjwa ya kuambukizwa ambayo yanatoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu ili kuweza kunusuru maisha ya wananchi walio wengi.


Pia alisema serikali iko tayari kuwasaidia kwa pale watakapohitaji msaada wao kwa sababu afya ni kitu cha msingi kwa wanyama pamoja na binadamu na kuongeza atashirikiana bega kwa bega na wizara kama vile Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Wizara ya Kilimo na Ufugaji ili kuweza kufikisha kile walichomtuma kama mtendaji wa serikali.


Pia ameshukuru taasisi zilizofanikisha mkutano huo ambazo ni OHCEA na SACIDS zimetengeneza mipango mizuri kwa wataalamu wa afya na kuwaleta karibu kwa ajili ya kushirikiana.


Akizungumza Profesa Robson Mdogera ambaye ni mhadhiri na mtafiti mtoa huduma katika Chuo Kikuu cha Sokoine amesema mkutano huu umekuja wakati muhafaka kwani kumekuwepo tatizo kubwa la kutoshirikiana katika hali zote.


“Huu mpango waliokuja nao wa Afya moja unaweza kuleta mafanikio makubwa maana kuna viwatilifu vinavyowekwa kwenye mifugo au mazao ili kukinga magonjwa hivyo kunapelekea viwatilifu hivyo kuliwa na binadamu bila kujua na kupeleka adhari kubwa katika mwili wa binadamu. Hivyo kunahitaji kuwa na ushirikiano katika nyanja zote za afya ili kuweza kutatua tatizo pale tu linapotokea,” alisema Prof. Mdogera.




DK. KINGWANGALLA ATOA SIKU 60 KWA HOSPITALI YA KANDA YA RUFAA MBEYA, KUNUNUA MASHINE YA CT-SCAN

Zikiwa zimepita siku chache tangu  Simbayablog kupiga kambi jijini Mbeya na kugungua kuwa  Hospitali ya Rufaa Kamda ya Mbeya haina mashine ya CT Scan imezaa matunda baada ya Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla kufanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo jana na kutema cheche.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Februari 12, 2016 katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya, na kutoa maagizo mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mashine CT-Scan ndani ya siku 60 huku akibainisha kuwa endapo watazembea basi watawachukulia hatua kali na kuwajibishwa watendaji na uongozi wa Hospitali hiyo.


Dk. Kigwangalla alifika hospitalini hapo majira ya saa tisa alasiri na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi ambapo ndipo alipobaini ukosefu wa mashine hiyo ya CT-Scan pamoja na vifaa vingine muhimu ambavyo alibainisha kuwa hata uongozi wa Hospitali hiyo walikuwa na uwezo wa kuvinunua bila kutegemea Serikali.


Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na kitengo cha kutolea huduma kwa wagonjwa (OPD), Kitengo cha upasuaji, wodi ya upasuaji, duka la dawa la hospitali hiyo, wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, watoto na kitengo cha Maabara ambapo kisha alipata kuongea na wafanyakazi pamoja na uongozi mzima wa Hospitali.


Dk.Kigwangalla alitoa wasaha mwingi kusikiliza kero za wafanyakazi hao kuongea lile linalowakabili bila kuogopa ili aweze kujua matatizo na changamoto zinazowakabili.


"Hospitali kubwa kama hii hapa Mbeya na wataalam wote mlionao mnashindwa kufanya biashara!, Mnategemea tu Serikali? lini mtakuwa na CT-scan kwa upande wenu? wakati mnaingiza Milioni 500 kwa mwezi?" alihoji Dk. Kigwangalla.


Dk.Kigwangalla aliwaambia uongozi wa hospitali hiyo ina fursa na uwezo wa kufanya jambo kubwa kwani pia ina uwezo hata wa kukopa fedha kutoka mashirika ya bima ya afya.


Aidha, Dk Kigwangalla amewataka uongozi wa Hospitali hiyo kuwa wabunifu katika uendeshaji wao ikiwemo kutengeneza jengo la kisasa la matibabu ya kulipia, kujenga nyumba za wafanyakazi ambapo amewapa mikakati hiyo imeanza na pindi atakaporejea tena hospitali hiyo.



Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisisitiza suala la Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya kununua mashine ya CT-scan ndani ya siku 60, huku akiahidi kuwachukulia hatua kali ya kuwawajibisha watendaji watakaozembea katika hilo.




Baadhi ya wafanyakazi na madaktari wa hospitali hiyo wakifuatilia mkutano huo wakati Naibu Waziri Dk.Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa alipofanya ziara Februari 12,2016. Wafanyakazi hao waliweza kutoa maoni yao mbalimbali ikiwemo suala la motisha na uboreshaji wa mishahara pamoja na ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo kitengo cha maabara.


Mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo ya rufaa Mbeya akiuliza akitoa maoni yake kwa Naibu Waziri Dk.Kigwangalla.




Kaimu Mkurugenzi wa hospitali ya Kanda ya rufaa Mbeya, Thomas Isidori akitoa fursa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (kulia) kuzungumza na wafanyakazi katika mkutano wake huo. 
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipita katika moja ya maeneo ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya sambamba na wenyeji wake...




Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akitazama moja ya kipimo cha mgonjwa ambacho hata hivyo ilieleza kuwa kilipimwa nje ya Hospitali hiyo na kuletwa hapo ambapo alipotaka kujua kwa nini imekuwa hivyo kwa hospitali kubwa kama hiyo alielezwa kuwa hawana mashine ya CT-Scan ndipo alipoutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha mashine hiyo inapatikana ndani ya siku 60 kuanzia hiyo Februari 12.




Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipata maelezo ya moja ya mashine ndani ya maabara ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya. Hata hivyo ameelezwa mashine hiyo ni ya zamani sana hivyo ufanisi wake ni mdogo huku wakimweleza kuwa inatakiwa wapatiwe mpya ilikuendana na kasi.




Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akimjulia hali Mtoto Edger Emmanuel (2) anayepatiwa matibabu ya mguu wake katika wodi hiyo ya watoto kitengo cha upasuaji.




Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori wakimjulia hali Mzee Lazaro Mwakapunga aliyelazwa hospitalini hapo.




Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipatiwa maelezo namna ya mfuko wa malipo wa ki-elektroniki unaotumiwa hospitalini hapo na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori. Hospiatli hiyo inatumia mfumo huo ambapo imeweza kufanikiwa katika ukusanyaji wake wa mapato.



Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipokelewa na Katibu wa Hospitali hiyo, Maryam Msalale wakati wa kuwasili katika ziara hiyo. (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog, Mbeya).


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...