Friday, 4 December 2015

WAWILI WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI ILIYOBEBA MAGAZETI YA MWANANCHI





GARI iliyokuwa imebeba magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti ikitokea Dar es Salaam kuelekea Iringa na Mbeya, imepata ajali katika mlima wa Kitonga, wilayani Kilolo mkoani Iringa leo alfajiri.

Watu wawili wamekufa papo hapo na wengine sita kujeruhiwa, mmoja vibaya baada ya gari lililokuwa likisafirisha magazeti ya mwananchi kutoka Dar es Salaam kwenda Iringa na Mbeya kupata ajali eneo la mlima kitonga barabara kuu ya Dar-es-Salaam-Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 11 alfajiri gari hilo la magazeti kuingia nyuma ya roli likiwa katika mwendo kasi.

“Leo imetoka ajali mbaya sana hapa Iringa, ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Haice iliyokuwa imebeba magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communication LTD; gari hilo lilipata ajali baada ya kuganga lori lenye tela kwa nyuma:

“Dereva wa gari hilo lililopata ajali alitaka kulipita roli ambalo nalo lilikuwa linaelekea Mbeya; alipokuwa akitaka kulipita aliona gari likija mbele yake na wakati akifanya maamuzi ya kurudi upande wake aligonga roli hilo kwa nyuma,”alisema.


Mungi aliwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Eliud Ogwasa (40) na Godfrey Owino (34) wote wakazi wa mkazi Dar es Salaam.

Aliwataka majeruhi kuwa ni Baraka Shitindi (32) ambaye hali yake ni mbaya na Kevin Shitindi (30) wakazi wa Mbozi Mkoani Mbeya na Herold Shitindi (25) mkazi wa Morogoro.

Wengine ni Zabroin Izote (29) mkazi wa mbeya na Joseph Kayani (37) mkazi wa Mafinga mkoani Iringa.

“Kamanda Mungi aliwaasa madereva kuwa makini na kuendesha gari kwa kuzingatian sheria za barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuwapotezea maisha wao na abria wao,” alisema.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa, Alfred Mwakalebela alisema wamepokea maiti mbili ambazo wamehifadhi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo.

Dkt. Mwakalebela alisema pia wamepokea majeruhi wanne ambao wameumia maeneo mbalimbali mwilini ikiwemo kuvunjika mguu huku mmoja kati yao akiwa na hali mbaya zaidi kiasi cha kushindwa kuzungumza.

Majeruhi Kevin Shitindi ambaye ameumia mkono na kifuani alisema walitoka Dar es Salaam saa sita usiku wakiwa 10 kwenye gari hiyo na walipofika Morogoro saa nane watu wawili walishuka.

Majeruhi Kayani na Lisote walisema hiace hiyo ilikuwa inakwenda kasi na wakati ajali inatokea wao walikuwa wamelala walichosikia ni kishindo na baadaye kuona madereva wamekufa papo hapo.

HALMASHAURI YA IRINGA MJINI YATOA AHADI 15 KWA WANANCHI WA JIMBO HILO


Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe na Naibu wake Joseph Lyata,


Na Frank Leonard, Iringa

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe na Naibu wake Joseph Lyata, wote kutoka Chadema, wamekutana na wanahabari kwa mara ya kwanza ofisini kwao hii leo na kuainisha mikakati yao mbalimbali inayolenga kuharakisha maendeleo ya wananchi wa Jimbo la Iringa Mjini katika kipindi cha miaka mitano ijayo.


Viongozi hao wanaunda halmashauri hiyo baada ya chama chao, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujizolea viti 14 kati ya 18 vya udiwani mjini Iringa huku nafasi ya ubunge ikichukuliwa na chama hicho kwa mara nyingine tena kupitia kwa mbunge yule yule wa 2010-2015, Mchungaji Peter Msigwa.


Kuhusu watendaji wa kata, mitaa na vijiji
1. Ni marufuku kuchukua fedha kwa wananchi wakati wakihitaji huduma ya muhuri kwa ajili ya barua za utambulisho, mikopo na zinginezo. Huduma hiyo ni bure sio ya kibiashara
2. Ni marufuku kwa watendaji na wenyeviti kujishughulisha na uuzaji wa viwanja katika maeneo yasio rasmi kama milimani na mabondeni ili kutoelendelea kuwapa hasara wananchi pindi mamlaka zinapolazimika kuwaondoa


Kuhusu barabara
1. Kwa kuwa ina greda kwa ajili ya kazi hiyo, halmashauri hiyo itajenga barabara katika maeneo yote ambayo ramani ya mipango mingi inaonesha kuna barabara zinapita ili wananchi wasirubuniwe na kuuziwa maeneo hayo kwa ajili ya shughuli zao za maendeleo
2. Barabara ya samora, kijiweni hadi hospitali ya manispaa ya Iringa Frelimo imeanza kujengwa kwa kiwango cha lami


Mwaka wa masomo 2016
1. Wanafunzi wa darasa la kwanza wanatakiwa kuandikishwa bure na inawataka walimu wa shule zote za msingi hadi sekondari kidato cha nne wasithubutu kuwabugudhi wanafunzi kwa kuwadai michango yoyote ile kwasababu serikali imekwishatoa maelekezo kwamba elimu hiyo itatolewa bure bila michango yoyote


Iringa kuwa jiji
1. Halmashauri ya Chadema itahakikisha inazifanyia kazi taratibu zote zinazotakiwa ili mji wake upate hadhi ya jiji.
2. Ili kufanikisha ndoto hiyo sheria zote za mipango miji zitasimamiwa na kutekelezwa kwa umakini mkubwa
3. Halmashauri mji wa Iringa unakuwa mji wa maghorofa na kwamba wale wote waliopewa likizo ya kujenga maghorofa katika maeneo yanayotakiwa kisheria kujengwa nyumba hizo (katikati ya mji) watatakiwa kufanya hivyo kama muda waliopewa umekwisha. Vibali vya ujenzi wa maghorofa na nyumba nyingine za kisasa vitaendelea kutolewa
4. Ili malengo hayo yafikiwe, wafanyakazi wa halmashauri hiyo (wataalamu) watatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa majukumu yao, kuzingatia sheria kanuni na taratibu zote za kazi ikiwa ni pamoja na muda wanaotakiwa kuwepo au kuondoka kazini


Kuhusu kodi
1. Kodi za halmashauri zinazotozwa kwa wananchi wa halmashauri hiyo zitaangaliwa upya, ili zile zinazoonekana kuwa kero kwa wananchi wa kawaida zifanyiwe marekebisho
2. Kodi za lazima ambazo hazina kero kwa wananchi zitakusanywa kwa nguvu ili kufidia nakuongeza mapato ya halmashauri hiyo; kodi hizo ni pamoja na za majengo.


Kuhusu matumizi ya halmashauri
1. Halmashauri hiyo mpya imeahidi kusimamia na kupunguza matumizi yote ya halmashauri yasio ya lazima ili fedha zitakazookolewa zitumike kuboresha huduma za kijamii


Kuhusu Gari la kubeba wagonjwa na taka
1. Mapato yatakayokusanywa, yakiwemo yale kutoka kwa wale wanakwepa kodi za majengo yatatumika kununua gari la kubeba wagonjwa na hivyo kufuta ule mpango wa kuuza gari la Meya ili fedha zitakazopatikana zitumike kununua gari hilo
2. Mapato hayo pia yatatumika kununua gari lingine la kubeba taka ili kukidhi mahitaji ya kuung’arisha mji wa Iringa


Kuhusu Mikopo ya Vijana na Wanawake
1. Halmashauri hiyo ya Chadema itafuatilia marejesho ya mikopo yote iliyotolewa kwa makundi hayo ili makusanyo yake yaendelee kuwanufaisha wananchi wengine


Kuhusu uwekezaji
1. Maeneo yaliyopendekezwa kwa ajili ya uwekezaji vitega uchumi vitakavyoiongezea mapato halmashauri hiyo kama ujenzi wa miradi mikubwa ya vitega uchumi katika maeneo ya Tembo Bar na Kilabu cha Kijiweni yatafanyiwa kazi kwa haraka.


Mapema mwaka 2011, halmashauri hiyo kwa kupitia aliyekuwa Meya wa Manispaa hiyo, Amani Mwamwindi iliahidi kuyabomoa majengo hayo ili kupisha uwekezaji mkubwa utakaoongeza mapato ya halmashauri hiyo.


Wakati Tembo Bar ipo pembeni mwa stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, mjini Iringa, kilabu cha Kijiweni kipo karibu na Chuo cha Ufundi Stadi cha Veta.

Katika eneo la Tembo Bar, mpango wa halmashauri hiyo ulikuwa ni kujenga jengo la ghorofa tano na kituo cha mafuta huku katika kilabu cha Kijiweni mpango ulikuwa ni kujenga maegesho, ukumbi wa muziki, sherehe, bar, hoteli, maduka makubwa, ukumbi wa mazoezi na bwawa la kuogolea.


Kuhusu wamachinga
1. Halmashauri itakaa ili kuyapitia maamuzi ya halmashauri iliyopita yaliyowaondoa machinga katika gulio la Jumamosi na Jumapili katika eneo la mashine tatu ili wafanyabishara hao wapate fursa hiyo.
2. Ahadi hiyo itakwenda sambamba na kutafuta maeneo mengine kwa ajili ya wafanyabiashara hao


Kuhusu Michezo
1. Halmashauri itaangalia uwezekano wa kuwa na timu moja itakayosaidiwa kwa nguvu ya halmashauri na wadau wake ili kiu ya watu wa Iringa ya kuona wana timu inayoshiriki ligi kuu ifanikiwe


Kuhusu Mazingira
1. Halmashauri itatumia rasilimali zake, wakiwemo wananchi wenyewe kuhakikisha wanaufanya mji wa Iringa kuwa Mji wa Kijani kwa kupanda miti mingi huku mazingira yake yakiwekwa safi siku zote.


Kuhusu Biashara
1. Halmashauri ya Chadema itahakikisha wafanyabishara wanatengenezewa mazingira mazuri yatakayowafanya wafanye biashara zao bila kuvunja sheria, taratibu na kanuni zingine.


Kuhusu huduma za afya na maji
1. Halmashauri hiyo imeahidi kuziimarisha huduma hizo kwa kushirikiana na wadau wengine wote muhimu ili afya za wakazi wa Iringa ziimarike


Huduma zinginezo
1. Zitatekelezwa kwa kushirikiana pasipo kupindishwapindishwa na serikali ya awamu ya tano ya Dk John Pombe Magufuli


Kuhusu wanahabari
1. Halmashauri hiyo itahakikisha wanahabari wanashirikiana nao vyema ili kufikia malengo yao. Kutakuwepo na utaratibu wa kukutana na wanahabari wote kila baada ya miezi mitatu au pale inapohitajika kulingana na mahitaji yenyewe

World Soil Day



World Soil Day 2015 : ‘Soils a solid ground for life’


World Soil day celebrates the importance of soil as a critical component of the natural system and as a vital contributor to the human commonwealth through its contribution to food, water and energy security and as a mitigator of biodiversity loss and climate change. It is celebrated particularly by the global community of 60 000 soil scientists charged with responsibility of generating and communicating soil knowledge for the common good.

Soils have been neglected for too long. We fail to connect soil with our food, water, climate, biodiversity and life. We must invert this tendency and take up some preserving and restoring actions. The World Soil Day campaign aims to connect people with soils and raise awareness on their critical importance in our lives. 

The WSD 2015 will be celebrated on the 4th of Decemberat FAO headquarters in Rome and FAO regional offices. National events will also be organized so make sure to regularly check the map of the WSD2015 events and/or register your event. The theme for this year will be “Soils a solid ground for life”. 

Did you know? 

Soil is the basis for food, feed, fuel and fibre production and for services to ecosystems and human well-being. It is the reservoir for at least a quarter of global biodiversity, and therefore requires the same attention as above-ground biodiversity. Soils play a key role in the supply of clean water and resilience to floods and droughts. The largest store of terrestrial carbon is in the soil so that its preservation may contribute to climate change adaptation and mitigation. The maintenance or enhancement of global soil resources is essential if humanity’s need for food, water, and energy security is to be met. 

COSATO CHUMI AMALIZA TATIZO LA VITANDA HOSPITAL YA MAFINGA MJINI

Mbunge wa jimbo la Mafinga mji Cotato chumi akimkabidhi msaada wa vitanda ,magodoro pamoja na vifaa mbalimbali kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya juzi



baadhi ya waandishi wa habari wakifuatiliwa ugawaji wa vifaa hivyo wakati wa makabidhiano






mbunge wa mafinga mjini cosato chumi akikabidhi vifaa hivyo kwa vitendo







baadhi ya wadau na wanachama wa chama cha mapinduzi ccm walihudhulia tukio hilo




TATIZO la upungufu wa vitanda katika wodi ya akina mama na watoto katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambalo kwa muda mrefu limekuwa chanzo cha msongamano na uwalazimu
baadhi ya wagonjwa kulala sakafuni sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya uongozi wa hospitali hiyo kupokea msaada wa vitanda na vifaa tiba kutoka kwa mdau wa maendeleo katika sekta ya afya.
 
Mbunge wa Mafinga Mjini (CCM) Cosato Chumi alisema kuwa kwa muda mrefu hospitali hiyo ilikuwa ina upungufu wa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda hali iliyofanya kuandika maandiko mbalimbali kwa wahisani wa nje ya nchi ili kuweza kumsaidia kupata vifaa hivyo .

Alisema kuwa umefika wakati sasa wadau mbalimbali, mifuko ya kijamii na makampuni kujenga utamaduni wa kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wagonjwa hospitalini kwani kufanya hivyo ni sehemu ya kurudisha kile wanachokitapa kwa jamii.
 
“Unajua afya ni kila kitu katika maisha ya binadamu hivyo lazima nitekeleze ahadi zangu nilizotoa wakati wa kampeni na wanachi lazima tufanye kazi kwa kujituma ili tumuunge mkono rais wetu ambaye anania ya ya kutuletea maendeleo na kuwataka wadau mbalimbali kusaidia jamii zenye mahitaji na kuacha kutegemea serikali pekee “alisema
 
Chumi aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kuunga mkono kwa kufanya kazi kwa nguvu zote ili walete maendeleo kwa pamoja maana akifanya kazi pekee yake bila wao hawezi kuleta maendeleo
pekee yake.

Msaada huo wa vitanda 16 na magodoro 11 na vitu mbalimbali umetolewa na taasisi binafsi inayojishughulisha na masuala ya afya ya nchini Astralia ijulikanayo kama “Rafiki Surgical Mission” kwa uratibu wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Mafinga mjini

Alisema kuwa msaada huo aliopatiwa na rafiki zao hawajatoa hata
senti tano bali huwa marafiki hao wanachangishana fedha na kununua vifaa hivyo na kisha kuvisafirisha mpaka bandari kavu ambapo hapo ndio hutumia gharama kusafirisha vifaa hivyo mpaka sehemu husika

“Ndugu zangu nadhani kila mmoja alikuwa akifahamu machungu waliyokuwa wakipata mama zetu wanapokuja kujifungua kwa kukosa sehemu za kujifungulia lakini leo hii msaada huu utatusaidia sana na yoyote atakayeguswa na anaweza kuja na kuchangia chochote maana mufindi ni yetu sote na mufindi itajegwa na wanamufindi wenyewe”alisema

Alisema jambo kubwa lilokuwa likimuumiza kicha kila kukicha ni tatizo la vifaa katika hospital, elimu pamoja na tatizo la maji hivyo ni wakati wawanamafinga kushikana kwa pamoja katika kusumkuma mbele gurudumu la maendeleo ili kuendana na kauli mbiu ya sasa ya HAPA NI KAZI TU.

Akipokea msaada huo kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya alisema kuwa msaada wa vitanda hivyo na magodoro na vifaa mbalimbali utakuwa umemaliza kabisa tatizo la vitanda hospitalini hapo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kumalizika endapo kutatokea mdau mwingine kuwasaidi.
 
Kwa upande wake katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Jimsoni Mhagama alimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo huku akimwambia kuwa ni wakati wa kutekeleza kazi kwa vitendo na wala si maneno kwani wananchi wanapaswa kutatuliwa kero mbalimbali zinazowakabili badala ya kupiga porojo zisizo na msingi .

Mhagama alisema kuwa kila mmoja anapaswa kuwajibika ipasavyo katika nafasi yake kwani kasi anayokwenda nayo Rais John Magufuli si ya mchezo bali ni ya mchaka mchaka na ili nchi iweze kusimama katika mstari ulionyoka kila mmoja anapaswa kucheza wimbo wa mchaka mchaka.

‘’Huuu si wakati lelemama huu sio wakati mchezo mchezo ni wakati wa uwajibikaji,hakika Tanzania tumepata kiongozi mchapa kazi tazama sasa ni siku ya 27 nchi inaongozwa na watu wanne lakini kila sektaa imenyoka na mimi  nasemaa Magufuli wanyooshe tu kwa kuwa watu walikuwa wakifanya kazi kwa mazoeya bila ya kuangalia madhara wanayopata watanzania wengi

Hata hivyo Mhgama alisema kuwa kwa kuwa kipindi cha muda mchache nchi inaongozwa na watu wachache na nchi imesimama haoni sababu ya kuwa na baraza kubwa la mawaziri, bali Rais Magufuli achague baraza dogo kama la watu10 ili kupunguza mzigo kwa serekali yake ya kuwa na mawziri wengi wasiokuwa na tija .





WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...