Sunday, 31 May 2015

Mashine 1,600 zaidi za BVR zawasili nchini


Dar es salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uandikishaji wa wananchi kwenye Daftari la Wapigakura nchini utamalizika mwishoni wa mwezi ujao baada ya mashine 1,600 zaidi za kielektroniki kwa ajili ya kazi hiyo kuwasili juzi.


Ofisa ugavi mwandamizi wa NEC, Datus Matuma alisema mashine hizo zinazotumia teknolojia ya utambuzi wa alama za mpigakura (Biometric Voter’s Registration), zitaanza kupelekwa mikoa ya Mara, Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

WASIRA ALIPUKA ,AMPIGA KIJEMBE KIAINA LOWASA ,ATANGAZA NIA YA KWENDA MAGOGONI


Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, amnabe pia ni Mbunge Bunda mkoani Mara, Steven Masato Wasira leo ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyikia baadae mwaka huu.


Katika hotuba yake ya takribani dakika 60 mh WASIRA ametumia muda mwingi kukemea vitendo vya rushwa huku akiwahmiza wananchi kumchagua kiongozi ambaye hatawaibia mali zao na badala yake wamchague mtu ambaye atawatumikia watanzania.



Amesema kuwa kiongozi anayekuja mbele za watu na kusema anaichukia ruswa wananchi wamwangalie usoni kama kweli anamaanisha anachokisema au anasema kama fashion kwa sababu ameambiwa akisema anachukia rushwa atachaguliwa.


Amesema kuwa yeye ni kiongozi ambaye tangu tanzania imeanza kukumbwa na kashfa za wizi wa mali za umma hajawahi kutajwa wala kuhisiwa katika wizi huo hivyo anadhani yeye ni msafi na anafaa kuiongoza tanzania kwa miaka miktano ijayo


Wasira ametangaza siku moja baada ya Kada wa CCM na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kuliteka jiji la Arusha wakati akitangaza nia kama hiyo. Miongoni mwa makada wa CCM ambao wanatarajiwa kutangaza nia kama ya Lowassa na Wassira ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba atakae tangaza nia hiyo baade leo, Charles Makongoro Nyerere, Lazaro Nyalandu, Bernard Membe, na makada wengine wengi wa chama hicho wametajwa kuwania nafasi hiyo.Wasira akitangaz nia hiyo hii leo katika Ukumbi wa BOT jijini Mwanza amesema yeye kauli mbiu yake ni Uadilifu. (HABARI24 BLOG)

TDBP TO CONSTRUCT 4000 BIO-GAS PLANTS

Mratibu wa Program ya Biogesi Tanzania (TDBP), Cyprian Shila (kulia) akibadilishana na mawazo na mmoja ya watendaji wa Mkoa wa Njombe baada yakumalizika kwa semina ya wakulima wa kilimo hifadhi pamoja na biogesi.

Dr. Rehema Nchimbi(katikati), ambaye pia ni Mkuu wa Njombe akiongea na wakulima wakati wiki ya wakulima watatifi katika kilimo hifadhi na biogesi jana. Waliyeketi toka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Waging'ombe, Frederick Mwakalebela na Mkuu wa Mradi Kilimo Hifadhi, Profesa Ndelilio Urio kutoka SUA.
    

Wakulima wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa wiki ya wakulima mkoani Njombe.



By Friday Simbaya, Njombe 

Tanzania Domestic Biogas Program (TDBP) has said this year it will construct 4,000 biogas plants countrywide in the effort of reducing greenhouse gases emissions like methane (CH4) which is brought by cow dung. 

According to the TDBP Country Director Cyprian Shila, the choice of biogas system depends on its cost, durability and ease of maintenance. 

TDBP KUJENGA MITAMBO YA BIOGESI 4000 NCHI NZIMA

Mratibu wa Program ya Biogesi Tanzania (TDBP), Cyprian Shila (kulia) akibadilishana na mawazo na mmoja ya watendaji wa Mkoa wa Njombe baada yakumalizika kwa semina ya wakulima wa kilimo hifadhi pamoja na biogesi.

Dr. Rehema Nchimbi(katikati), ambaye pia ni Mkuu wa Njombe akiongea na wakulima wakati wiki ya wakulima watatifi katika kilimo hifadhi na biogesi jana. Waliyeketi toka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Waging'ombe, Frederick Mwakalebela na Mkuu wa Mradi Kilimo Hifadhi, Profesa Ndelilio Urio kutoka SUA.
    

Wakulima wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa wiki ya wakulima mkoani Njombe.



Njombe: Mratibu wa Program ya Biogesi Tanzania (TDBP), Cyprian Shila amesema watasimika mitambo ya biogesi 4,000 kwa nchi nzima ukiwemo mkoa wa Njombe mwaka huu katika mpango wa utekelezaji kwa kushirikiana wadau mbalimbali katika sekta ya hiyo. 

Shila alisema kuwa lengo la kusimika mitambo ya biogesi nchi nzima sio tu kwa kuleta maendeleo kwa wananchi tu, lakini pia kutasaidia kusafisha hewa ya ukaa ya methane (CH4) inayotokana na kuwepo wingi wa mifugo.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...