Saturday, 15 November 2014

MWAKALEBELA AMWAGA VIFAA VYA MUZIKI OFISI YA CCM ...!

 
Kamanda wa UVCCM Wilaya Iringa mjini na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, Frederick Mwakalebela (kushoto)  amekabidhi vifaa vya muziki vyenye thamani ya shilingi milioni nane (8m/-) kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa mjini Abedi Kiponza (wa pili kushoto) na Katibu wa CCM Zongo Lobo Zongo (wa pili kulia) kwa ajili ya kusaidia shughuli za chama katika masuala ya kunadi sera na ilani ya uchaguzi ya mwaka  2010. Shughuli hiyo ilikwenda sambamba na kumuaga aliyekuwa mkuu wa mkoa wa iringa Dkt. Christine Ishengoma kichama ngazi ya wilaya.

 Kamanda wa UVCCM Wilaya Iringa mjini na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, Frederick Mwakalebela akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukabidhi vifaa vya muziki vyenye thamani ya shilingi milioni nane (8m/-) kwa ofisi kuu ya CCM Wilaya ya Iringa mjini leo. Alisema kuwa ameamua kusaidia vifaa vya muziki ili viweze ksaidia kunadi sera za chama katika kata zote ya Manispaa ya Iringa na hatimaye kupunguzu gharama kwa chama ya kukodi vyombo kama hivyo kwa gharama. Alisema kuwa badala hiyo pesa ya kukodi vyombo vya muziki hivyo itumike kwa shughuli nyinge ya kujenga chama.


Wanachama  wakishangilia kwa shangwe wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa mkoa wa iringa Dkt. Christine Ishengoma kichama ngazi ya wilaya, wilaya ya Iringa Mjini CCM akimtakia heri na safari njema aendako leo mchana katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Iringa mjini. .

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma akifurahi jambo wakati wa hafla fupi ya kuagwa na wanachama wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini na kuwaasa kuwa na mshikamano na upendo wa kutoka moyoni ilikuweza kupata ushindi katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015. Hata hivo nafasi yake imechukuliwa na AminaJuma Masenza baada ya mabadiliko ya wakuu wa mikoa na wilaya yaliofanywa Rais Prof. Jakaya Kikwete hivi karibuni.



Magazeti Leo Jumamosi


1_e9e4d.jpg
2_ff1a6.jpg
3_e0b98.jpg
4_9909d.jpg
5_00812.jpg
6_b3aea.jpg
7_dd525.jpg
10_fc71a.jpg

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...