Tuesday, 5 May 2015

CCM WAZOA WANACHAMA WAPYA 200 MKWAWA



KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Sixtus Mapunda amewataka vijana wa chama hicho kuwa wa kwanza kulinda amani hata pale chama chao kinapotukanwa bila sababu na wapinzani wao katika mikutano yao ya kisiasa.

Mapunda aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wake wa hadhara alioufanya nje ya Chuo Kikuu cha Mkwawa, mjini Iringa katika ziara yake ya siku tano aliyofanya mkoani Iringa kukiimarisha chama hicho.

TUNDU LISSU:WAKAZI WA IRINGA MJINI MJITOKEZE KWA WINGI KUJIANDIKISHA BVR




Wakazi wa Jimbo la Iringa Mjini wakimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu wakati wa mkutano wa hadhara wa Chadema leo uliofanyika stendi ya mabasi ya Mlandege mjini Iringa.

MNADHIMU Mkuu wa Kambi ya Upinzani ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (CHADEMA) amezungumza na Wakazi wa Jimbo la Iringa Mjini wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Stendi ya Mlandege mjini hapa. Mbunge huyo aliwataka wakazi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura ili kweza kupata kadi za BVR zitakazotumika kupigia kura katika uchaguzi mkuu oktoba mwaka huu.

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mch. Peter Simon Msigwa (CHADEMA) amezungumza na wakazi wa Jimbo hilo wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Stendi ya Mlandege mjini hapa.

ELIMU ZAIDI YATAKIWA KUBADILI JAMII KUTHAMINI MAALBINO



Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye akiwakaribisha mameneja wa Redio za jamii nchini (hawapo pichani) walioshiriki kwenye mafunzo ya siku moja ya kutoa elimu kwa Redio za jamii nchini juu ya kuandaa vipindi vyenye ujumbe sahihi wa masuala yanayohusu watu wenye Albinism iliofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema hivi karibuni. Katikati ni Afisa mtetezi na ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun (UTSS), Kondo Seif na kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.

Na modewjiblog team, Sengerema

Ofisa mtetezi na ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun (UTSS) Kondo Seif, ameitaka jamii kuungana kupiga vita imani potofu zinazosababisha mauaji kwa watu wenye albinism.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...