Monday, 11 January 2016

LEITCIA NYERERE KUZIKWA BUTIAMA

SUMAYE 'ASHANGAZWA' NA RAIS MAGUFULI KUMJULIA HALI HOSPITALINI



Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam jana.


Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye na Mama Esther Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam jana.

MESSI MCHEZAJI BORA DUNIANI ASHINDA KWA MARA YA TANO TUZO YA BALLON D’OR 2015


Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona, na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, ametwaa tuzo ya mchezo bora wa dunia.

Messi mwenye miaka 28 alishinda kwa 41.33% kwa kura zote zilizopigwa, huku Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili kwa 27.76% na Neymer akipata 7.86%.

Hii ni mara yake ya tano kutwaa tuzo hiyo.

Kwa upande wa wanawake nyota wa Marekani Carli Lloyd, ameibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake.

Goli bora la mwaka likifahamika kama Puskas limwendea Wendell Lira anayekipiga katika Atletico Goianiense ya Brazil.

Kocha wa Barcelona Muhispania Luis Enrique amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa kuiongoza barca kufanya vizuri barani Ulaya kwa kutwa mataji matano msimu uliopita.

Jill Ellis kocha wa kikosi cha taifa cha Marekani amekuwa kocha bora wa wanawake baada ya kuongoza timu ya taifa ya Marekani kufanya vyema katika michuano ya kombe la dunia

PAMBAZUKA NA SIMBAYABLOG NA MAGAZETI YA LEO JUMANNE


KIWIA AONDOA KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA ILEMELA



Agrey Laban ambae ni Katibu wa Highness Kiwia akizungumza na Wanahabari nje ya Mahakama.


Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG


Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imetupilia mbali kesi ya Kupinga Matokeo ya ubunge katika Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza, iliyofunguliwa na aliekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
Haighness Kiwia.

Katika kesi hiyo ambayo ni namba mbili ya mwaka 2015 iliyofunguliwa Novemba 25 mwaka jana, Kiwia alikuwa akipinga ushindi wa mbunge wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kutokana na madai ambayo ni pamoja na kuendesha kampeni za ubaguzi wa kikabila sanjari na kupata kura ambazo hazikuendana na idadi ya wapiga kura walioandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura. 

Kesi hiyo imefutwa baada ya Kiwia kupitia kwa mwanasheria wake Paul Kipeja kuiomba Mahakama kufuta kesi hiyo kwa madai ya kwamba mteja wake ameshindwa kulipia gharama za Mahakama ambazo ni Shilingi Milioni 10 na kwamba washtakiwa walikuwa ni Angelina Mabula pamoja na Mwanasheria wa Serikali ambapo gharama ya kufungua kesi hiyo kwa kila mlalamikiwa ilikuwa ni shilingi Milioni Tano.

Kufuatia ombi hilo, Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Eugenia Gerald Rujwauka alitoa maamuzi ya kuifuta kesi hiyo kama ambavyo mlalamikaji alivyoomba.

Baada ya kesi hiyo kufutwa, Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea mlalamikiwa, amebainisha kuwa baada ya maamuzi hayo anatarajia kukutana na mteja wake ili kujadiliana hatua za kuchukua na huenda akafungua kesi ya madai dhidi ya Kiwia kutokana na kufungua kesi na kisha kuiondoa mwenyewe na hivyo kumuingiza mteja wake katika gharama zisizo za lazima.

Ifahamike kwamba Angelina Mabula pamoja na Highness Kiwia hawakuhudhuria Mahakamani hapo na hakukuwa na wafuasi wengi wa vyama vya siasa kama ilivyozoeleka ambapo nje ya Mahakama hiyo, Agrey Laban ambae ni Katibu wa Kiwia ameilalamikia Mahakama kutokana na kushindwa kupunguza gharama za kesi
hiyo jambo ambalo limepelekea haki kupotea.

Wakati hali ikiwa hivyo, Kheri James ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula, amepongeza maamuzi ya kesi hiyo kufutwa na kuongeza kuwa hatua hiyo inatoa wigo wa mbunge huyo kuwatumikia wananchi.

Akiwa ofisini kwake, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akapata fursa ya kuzungumzia Maamuzi ya Mahakama juu ya kesi hiyo ambapo amempongeza Mabula kwa uvumilivu wake kwa kuwa kiongozi akiwa na kesi Mahakamani anakosa uimara wa kuwatumikia wananchi.

Katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka jana, Angelina Mabula (CCM) aliibuka mbunge wa Jimbo la Ilemela kwa kupata ushindi wa kura 85,425 na hivyo kumshinda mpinzani wake wakaribu kutoka Chadema Highness Kiwia aliekuwa akitetea jimbo hilo ambae alipata kura 61,679.


Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea Angelina Mabula akihojiwa na Wanahabari nje ya Mahakama


Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea Angelina Mabula akihojiwa na Wanahabari nje ya Mahakama


Katibu wa Mbunge wa Ilemela Kheri James (mwenye miwani) akiwa katika mahojiano na wanahabari nje ya Mahakama


WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama


WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama


WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama


Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akieleza namna alivyopokea maamuzi ya Mahakama.


MSIBA DMV NA TANZANIA LETICIA NYERERE HATUKONAE TENA


Leticia Nyerere enzi ya uhai wake


Familia ya Leticia Nyerere ya Lanham, MD inasikitika kutangaza kifo cha mama Yao mpenzi kilichotokea tarehe 10 January 2016 nchini marekani. Mipango na utaratibu wa kusafirisha mwili inafanywa.

Msiba upo 9004 brightlea court, Lanham MD 20706.

Kama mila na desturi zetu tufike kuwafariji familia. Kwa maelezo zaidi wasiliana na :

Margareth mageni 240 462 9138

Emmanuel muganda 240 447 2801

Ramadhani kamguna 202 459 3838











Bwana ametoa. Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe


SERIKALI KUTOA BURE MBEGU ZA MTAMA KWA WENYE UPUNGUFU WA CHAKULA


Mkurugenzi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amewataka wananchi waliokumbwa na uhaba wa chakula nchini kufuata ushauri wa wataalam kwa kupanda mimea inayostahimili ukame ikiwemo mtama na uwele ili kuondokana na adha hiyo kila mwaka. 

Akizungumza jana na wananchi wa vijiji vya Iguluba na Mkulula vilivyopo kata ya Malenga Makali, Tarafa ya Isimani ambayo imeathirika zaidi na upungufu wa chakula wilayani Iringa, Brigedia jenerali Msuya amesema serikali itawapatia wananchi hao mbegu za mtama za bure ili wapande msimu huu.

Mkurugenzi wa Idara ya Maafa amefuatana na ujumbe wake kutathmini hali ya upungufu wa chakula wilayani Iringa na kujiridhisha na ugawaji wa msaada uliotolewa na serikali na kujua ni maeneo gani yanahitaji msaada zaidi.

Brigedia Jenerali Msuya anawahakikishia wananchi kuwa hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa.

Wakielezea hali halisi ya upungufu wa chakula wananchi wameishukuru serikali kwa kupelekea chakula lakini wakaomba kujengewa mabwawa ya umwagiliaji, maghala ya kuhifadhi chakula pamoja na mbegu zinazostahimili ukame.

Brigedia Jenerali Msuya na timu yake pia, wameshuhudia zoezi la ugawaji wa chakula kwa kaya zilizokumbwa na upungufu ukiendelea katika kijiji cha Igingilanyi na kusema kuwa serikali inatambua chakula hicho hakitoshelezi mahitaji yote.

Zaidi ya watu elfu 76 wilayani Iringa wanakabiliwa na upungufu wa chakula uliosababishwa na mvua chache zilizonyesha msimu uliopita.


Wiki mbili iliyopita serikali ilitoa tani 200 kwa kaya zilizokubwa na njaa kutokana na ukame.
 #####################################

IRINGA: Director of the Department of Disaster from the Office of the Prime Minister, Brigadier General Mbazi Msuya has urged citizens affected by food shortages in following the advice of experts to plant drought resistant crops including sorghum and millet to overcome the persecution every year.

Speaking yesterday to citizens at Iguluba and Mkulula villages in Malengamakali Ward, Isimani Division which is most affected by food shortages in Iringa district, Brigadier General Msuya said the government will give the citizens sorghum seeds free to plant into this season.

Director of the Department of Disaster his delegation came to assess the state of food insecurity in Iringa district, Iringa Region and assurance and distribution of the support given by the government to know what areas need more support.

Brigadier General Msuya he assured the public that no citizen will die of hunger.

Explain the real situation of food insecurity, citizens have thanked the government for giving them food but asked the government to build up dams for irrigation, food storage facilities and provide them with drought-resistant seeds.

Brigadier General Msuya and his team have also witnessed the distribution relief food to the households affected by food shortage in the Igingilanyi village and said the government is aware that food was not enough to cover all needs.

Over 76 thousand people Iringa District faced with food shortages caused by low rainfall last season.


Two weeks ago the government brought 200 tons of relief food to affected households in the villages of Isimani Division, Iringa district.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...