Saturday, 26 May 2018

DC URGES YOUNG PEOPLE TO DISASSOCIATE FROM BAD MORALS IN THE SOCIETY




  • Mufindi District Commissioner (DC) Jamhuri William has urged young people who have graduated from basic military training through national service program (JKT) to use their training they received in various camps in the country for national benefit. 

Speaking to the graduates during that pass out parade dubbed as ‘Operation Merrerani’ yesterday, DC William urged them to take advantage of the training and knowledge they gained in bringing national development. 

He added that youth who were receiving basic military training through national service program to use them to increase employment opportunities through self employment, hence reduce youth unemployment in the country. 

“Tanzanian government announced plans to revive compulsory national service to combat moral decay and to teach patriotism…,” said DC William. 

Earlier on, service man (SM) Ramadhan Mohamedi who was assisted by service girl (SG) Magdalena Mniko on behalf their graduates congratulated the government for restoring the JKT training and saying it will help to restore the national unity that has been in recent years lost. 

Service man Mohammedi said that Mereani's military training was officially opened on January 22, 2018 by the 514 KJ Captain JL Kashinde, with 1,185 youth including 815 boys and 370 girls. 

Mohamedi said until last week of the training the number of 1,179 youth graduated but six others did not manage to finish the race due to various reasons including the lack of patience, laziness, hopelessness and patriotism in their country. 

He said that during the course of training they learned life skills such as agricultural activities, livestock, construction and other productive activities and various social activities. 

In turn, the acting commander of Mafinga JKT Captain Victor Nkya explained the training for the young people in the camp was a great success in the new techniques that were used to ensure that all young people who joined the training are safe. 

Capt. Nkya said that the training aimed at building or teaching things such as nationalism, love, unity, solidarity and cooperation, patience and perseverance, discipline and entrepreneurships. 

He said that in general their young people were cooked well and had been trained in accordance with the National serving training program. 

The Tanzania National Service was established on July 10, 1963 with the government aimed at bringing together the youth of this country and providing them with the formation of patriotism and unity in society after independence. 

Some of the reasons for the introduction of JKT were to convert the thinking of young people of this country from the colonial situation to depend on other countries to develop. 

DC MUFINDI: VIJANA WA JKT MSITUMIE MAFUNZO MLIOPATA VIBAYA



Kikundi cha Singe cha vijana wakijitolea kundi Mererani 2018 wakipita mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William wakati wa mahafali ya kumaliza mafunzo ya awali ya jeshi la kujenga taifa (JKT) kikosi cha Maginga JKT wilyani Mufindi, Mkoa wa Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)





MUFINDI: MKUU wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William amsema vijana wanaohitimu mafunzo ya awaliya kijeshi la jeshi la kujenga taifa (JKT) kuyatumia mafunzo wanayoyapata katika kambi mbalimbali hapa nchini kwa faida ya Taifa. 

Hatua hii inaelezwa kuwa kama itazingatiwa na vijana wanaohitimu mafunzo ya muda mfupi ya JKT upo uwezekano mkubwa wa taifa kuwa na vijana ambao watakuwa waadilifu pindi watakapokuwa wakilitumikia taifa. 

Akizungumza na wahitimu hao jana Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam aliwataka kuyatumia vizuri mafunzo na maarifa waliopata katika kuliletea taifa maendeleo. 

Awali, wakisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi wahitimu hao waipongeza serikali kwa kuyarudisha mafunzo ya JKT na kusema kuwa yatasaidia katika kurudisha umoja wa kitaifa ambao kwa siku za karibuni umekuwa ukilegalega. 

Akisoma risala hiyo kwa niaba ya wahitimu, Ramadhan Mohammedi akisaidiwa na Magdalena Mniko alisema kuwa mafunzo hayo ya awali ya kijeshi ya kujitolea kundi- Mererani, yalifunguliwa rasmi tarehe 22 Januari, 2018 na kamanda kikosi 514 KJ makambako kanali J.L Kashinde, ikiwa na vijana 1,185 kati yao wavulana 815 na wasichana 370. 

Mohamedi alisema mpaka kufikia jana kosi imefikia wiki ya 24 ambayo ni wiki mwisho ya mafunzo hayo ya awali idadi ya kuruta 1,179 na wengine sita (6) hawakufanyiwa kuhitimu mafunzo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kushindwa uvumilivu, uvivu, kukosa ustahimilivuwa moyo na uzalendo kwa nchi yao. 

Alisema kuwa katika kipindi cha cha mafunzo walijifunza stadi za maisha kama vile shughuli za kilimo, ufugaji, ujenzi pamoja na shughuli zingine za uzalishaji mali na kazi mbalimbali za kijamii. 

Kwa upande wake, kaimu kamanda kikosi Kikosi cha Mafinga JKT Kapteni Victor Nkya alielezea kuwa mafunzo ya awali kwa vijana waliohitimu katika kambi hiyo kuwa yenye mafanikio makubwa kutokana na mbinu mpya zilizotumika katika kuhakikisha vijana wote waliojiunga na mafunzo hayo wanayamaliza salama. 

Nkya alisema kuwa mafunzo hayo yalilenga kuwajenga ama kuwafundisha mambo mbalimbali kama vile uzalendo kwa nchi yao, upendo, umoja, mshikamano na ushirikiano, uvumilivu na ushapavu, nidhamu na ujasiriamali. 

Alisema kuwa kwa ujumla wao vijana wamepikwa na wameiva na wamepata mafunzo na malezi kwa mujibu wa muongozo wa mafunzo ya kujitolea. 

Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa Julai 10, 1963 na serikali kwa lengo la kuwaweka pamoja vijana wa nchi hii na kuwapa malezi kuhusu uzalendo na umoja ili kuondoa dalili za matabaka zilizoanza kujitokeza katika jamii baada ya uhuru. 

Baadhi ya sababu za kuanzishwa kwa JKT ni: Kubadili fikra za vijana wa nchi hii kutoka ile hali ya ukoloni kutegemea nchi nyingine kuleta maendeleo. 


WAZIRI WA MAKAMBA AANDAA MDAHALO NA VIONGOZI WA DINI




Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano January Makamba ameandaa mjadala wa Kitaifa kuhusu nafasi ya Dini na uhifadhi wa mazingira utaohusisha Viongozi wa Dini, Wananchi na Viongozi wa Serikali.


“Itakuwa ni mjadala wa Kitaifa kuhusu nafasi ya Dini na uhifadhi wa mazingira, tumealika Maaskofu wa dini zote, Waislam pia, sisi tunaamini Watanzania wote tunamuamini Mungu ndo mana tumeona tuwatumie Viongozi wa dini kuelimisha” amesema January Makamba

MPACHIKA MABAO SALAMBA DAU LAKE NI TISHIO



Baada ya kuwabania Yanga kuwapatia mshambuliaji wao hatari kabisa, Adam Salamba, uongozi wa Lipuli FC umetangaza kiasi cha fedha kwa klabu yoyote inayohitaji kumnyakua mchezaji huyo.


Taarifa zinaeleza kuwa Lipuli wanahitaji kiasi cha shilingi milioni 50 pekee ili kumuachia mchezaji huyo aliyekuwa kwenye fomu nzuri msimu huu.

Awali Yanga walituma maombi ya kumuhitaji Salamba kwa ajili ya kuwapiga tafu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini yaligonga mwamba kutokana na kanuni za TFF, CAF na FIFA kutoruhusu mchezaji kucheza zaidi ya timu mbili ndani ya msimu mmoja.

Inaelezwa kuwa klabu za Simba na Azam FC ndizo zilizoweka nia ya dhati kumsajili mchezaji huyo na mazungumzo yanaendelea mpaka sasa.

Wakati huo Yanga ambao walihitaji nia ya kuwa naye bado hawajazungumza chochote mpaka sasa kama wana lengo la kumsajili au la.

MAWAKILI WA BILIONEA WA ESCROW WACHACHAMAA MAHAKAMANI,WALIA NA UPANDE WA SERIKALI



Didas Respicius, wakili wa utetezi katika kesi inayomkabili Harbinder Seth na mfanyabiashara James Rugemalira, wamekiamsha baaada ya kuwasilisha malalamiko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa washtakiwa hao wamefikisha mwaka mmoja gerezani na upelelezi wa kesi inayowakabili bado haujakamilika.

Wakili huyo ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 24, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Iman Mizizi kueleza upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Didas amedai kuwa washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Juni 19, 2017 wakiwa na mashtaka ambayo yanadhaminika lakini wakiwa katika kuwasilisha maombi ya dhamana, walibadilishiwa mashtaka ambayo hayana dhamana.

Amesema tangu mwaka jana hadi sasa upande wa mashtaka unadai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, kwamba kuwa kwa mujibu wa hati ya mashtaka washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo, mwaka 2013. 

Amebainisha kuwa walifikishwa mahakamani miaka minne baadae lakini mpaka sasa bado inadaiwa upelelezi haujakamilika.

Ameomba upande wa mashtaka ufanye kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na Katiba kwa kujali haki za washtakiwa ili kesi iendelee mbele, kuutaka upande wa mashtaka ndani ya siku 14 ueleze upelelezi umekamilika, kama haujakamilika washtakiwa waachiwe huru.

Wakili Mizizi alidai suala la Seth kupatiwa matibabu bado linashughulikiwa na kwamba wanasubiri jopo la madaktari litakapokamilika atapatiwa matibabu.

Amesema Katiba ndiyo inayotumika kutunga sheria na ndiyo iliyotumika kuwafunguliwa mashtaka washtakiwa .

Baada ya kusikiliza hoja zote, Hakimu Shaidi amesema amezingatia hoja zote na akashauri upande wa utetezi kupeleka maombi Mahakama Kuu kwa ajili ya kupata maelekezo ya sheria ambazo zinalalamikiwa na zile zinazowafunga mikono.

Hakimu Shaidi aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 7, 2018 kwa ajili ya kutajwa.

Sethi na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola 22 milioni za Marekani.
Chanzo ni Mcl Online

MINOTI YAENDELEA KUMWAGIKA KWA SHOMARI KAPOMBE



SHOMARI Kapombe ambaye ni beki kisiki wa Timu ya Simba,amemwagiwa fedha na kundi la Spora kupitia WhatsApp linaloshabikia klabu ya Simba ambo ni Mabingwa wa ligi kuu ambayo inafikia tamati.

Kapombe amepewa zawadi ya kiasi cha shilingi laki tano (500,000) kama mchezaji bora wa mwezi Aprili 2018.


amekabidhiwa kiasi hicho cha fedha na Kiongozi Mkuu wa kundi hilo, Ally Masaninga pamoja na fremu iliyo na picha yake katika Uwanja wa Bocco Vetarani unaotumiwa na wekundu hao wa Msimbazi kujifua kwa ajili ya mechi za ligi.


Spora wametoa zawadi ya fedha hizo kama sehemu ya kutoa motisha na hamasa kwa wachezaji wa Simba kujituma zaidi Uwanjani ili kuipigania timu iweze kupata matokeo.


Tangu msimu wa 2017/18 uanze, imekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa kundi hilo kutoa zawadi ya mchezaji bora kwa kila mwezi inayolenga kutia morali kwa wachezaji.


Zawadi hiyo imetolewa ikiwa Simba ambao ni mabingwa wapya wa ligi msimu huu wakijiandaa kuhitimisha ratiba ya mechi za ligi Kuu Bara ambapo watacheza dhidi ya Majimaji FC Jumatatu ya wiki ijayo.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...