Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mzingira) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makete, Dkt. Eng. Binilith Mahenge akisoma hotuba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mzingira) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makete, Dkt. Eng. Binilith Mahenge (mwenye tai ya bluu) akifurahia igizo wakati wa uzinduzi wa mradi wa mazingira wilayani Makete. Kulia kwake ni Diwani wa Iniho Jison John Mbalizi, Mkuu wa Chuo VETA-Makete Ramadhan Sebbo na Mwenyekiti wa Bodi wa CCDO Majaliwa Mayova.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mzingira) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makete, Dkt. Eng. Binilith Mahenge (mwenye tai ya bluu) akikabidhi vifaa vya michezo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Makete (MDFA), Bosco Godigodi Mazangalila (kulia) kwa timu za mazingira (Environmental Clubs) wanaoshuhudia ni Meneja Mradi Agnes Mahenge na Mwenyekiti wa Bodi CCDO Majaliwa Mayova
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mzingira) Dkt. Eng. Binilith Mahenge akionesha kitabu cha mazingira cha mwalimu cha kufundishia katika shule za msingi baada yakukizindua.
WAZIRI wa Nchi,
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Eng. Binilith Mahenge (MB) ametoa
wito kwa wananchi kuwa suala la usafi na utunzaji wa mazingira linaanza na mtu
mmoja na hatimaye jamii nzima.
Dkt. Mahenge alisema haya wakati wakuzindua miradi
miwili ya hifadhi ya mazingira inayofadhiliwa na UNDP na Tanzania Forest Fund
(TFF) kupitia Asasi ya Children Care Development Organization (CCDO) wilayani
Makete, mkoani Njombe jana.
Mradi wa kwanza
unaofadhiliwa na UNDP unalenga kuiwezesha jamii katika kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabianchi na mwengine unaofadhiliwa na TFF unalenga katika upandaji
miti ili kuboresha hifadhi ya misitu na chanzo cha maji eneo la Unyangogo
katika Kata ya Iniho.
Miradi hiyo
inatekelezwa na asasi ya CCDO, inayojishughulisha na kazi ya utoaji elimu ya
kupambana na mabadiliko ya tabianchi, utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji
katika wilaya za Iringa na Makete.
Alisema kuwa
ili kulinda afya zao wananchi hawanabudi kuyatunza mazingira kwa ajili ya
vizazi vijavyo.
“Sote
tumeshuhudia athari za mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame uliokidhiri,
mvua zisizotabirika, mafuriko, kuongezeka kwa joto, kuibuka kwa magonjwa kama
malaria katika maeneo ambayo huko nyuma hayakuwa na historia ya magonjwa hayo;
mfano katika baadhi ya maeneo ya Makete,” alisema.
Alisema kuwa
malaria kwa sasa imeripotiwa katika mikoa mingi ikiwemo mikoa ya Iringa,
Njombe, Mbeya na Kilimanjaro.
“Haya yote
ni ushahidi wa uwepo wa mabadiliko ya tabianchi na yanatukumbusha kwamba sote
tunao wajibu wa kuhifadhi na kulinda mazingira yetu ili kuilinda nchi yetu na
dunia kwa ujumla kutokana na majanga yatokanayo na uharibifu wa mazingira,”
aliongeza waziri huyo.
Alisema kuwa
serikali inaendelea na juhudi za kulinda na kuhifadhi rasilimali za mazingira
nchini kupitia utekelezaji na usimamizi wa sera, sheria, kanuni na miongozo.
“ Nitumie
fursa hii kuzielekeza mamlaka za serikali na mitaa na taasisi za serikali kutekeleza
kikamilifu matakwa ya sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 kwa
kuhuisha masuala ya hifadhi ya mazingira katika mipango yao ya maendeleo na
bajeti zao za kila mwaka,” alisema.
Pia alitoa
wito kwa asasi zisizo za serikali, taasisi za dini, na wadau wengine kushiriki
kikamilifu katika juhudi za kuhifadhi mazingira na kila mdau kwa nafasi yake.
Juma
lililopita tarehe 22 Aprili, 2015, serikali ilizindua ripoti ya pili ya hali ya
mazingira nchini. Ripoti hii inabainisha ongozeko la watu likiambana na
kuongezeka kwa kasi kubwa ya uharibifu wa mazingira hususan misitu na vyanzo
maji.
Ripoti pia
imeanisha athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta za kiuchumu kama vile,
kilimo, mifugo, uvuvi, miundombinu, wanayapori, uchukuzi, viwanda na afya.
Akisoma
risala kwa mgeni rasmi, Meneja wa Mradi, Agnes Mahenge alisema kuwa asasi ya
children care development organization imekuwa ikijishugulisha na kazi ya kutoa
elimu ya kupambana na athari za tabianchi, utunzaji wa mazingira na vyanzo maji
kwa watoto na wanawake kwa lengo la kufanya watoto kuyapenda mazingira wakiwa
bado wadogo na kuwa askari wema kwa nchi yao.
Pia alisema
kuwa watoto kuwafanya wawe walimu wazuri kwa vizazi vijavyo hususan katika
kutekelezaji wa sheria namba 20 ya mazingira ya mwaka 2004 katika kuwajengea
uwezo wa uelewa, kupanua ajira na namna ya kupambana na umaskini wa kifikra na
kipato.
Alisema kuwa
shirika hilo limefanyikiwa kuunda timu 16
za mpira wa miguu kwa wanaume,
wanawake na watoto.
Timu hizi za
mazingira ni za kudumu na lengo lake ni kuona timu hizi zinakuwa zikiendeshwa
kwa mfumo wa ligi na kuwa na timu moja mama ambayo itapiganiwa kupanda daraja
kwa kushiriki kwenye ligi kuu ya Vodacom huku ikifanya kazi ya kuhamasisha
jamii kuhusiana na elimu ya mabadiliko tabianchi.
Wakati huohuo,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mzingira) ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Makete, Dkt. Eng. Binilith Mahenge alitoa vifaa vya michezo zikewemo
jezi seti nne na mipra 20 kwa timu za mazingira (Environmental Clubs) kutoka
halmashauri za Iringa na Makete.
Alisema kuwa
lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuona vijana wengi wa maeneo ya vijijini
wanashirika kikamilifu katika kukuza vipaji vyao pamoja na kutoa elimu ya uhifadhi wa
mazingira.